MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 496
- 768
Nimekuwa nikiona vitu vingi vinavyouzika nchi za Ulaya na uarabuni. Hasa parachichi, viazi mbatata, matunda mengine yakiwemo machungwa, tikiti maji nk. Bila kusahau maua.
Ukiangalia uhitaji wa hivi vitu, utagundua asilimia kubwa ya vyakula vya asili, vinavyouzika, kwa gharama kubwa, vinatoka Africa. Kampuni za ndege zinahangaika kupata ndege za mizigo, nchi nyingine huku zikihakikisha zinapata cold rooms( vyumba vya kutunza ubaridi), kwa ajili ya mavuno ya mboga mboga na matunda.
Hivi vitu, nchi zikiwemo Kenya na Rwanda, wanapiga sana hela. Watu hawa, hawana ardhi nzuri yenye rutuba kuliko Tanzania.
Je, wale wasomi, wale wanaoenda semina za kila kukicha, wale wanaoiwakilisha nchi kutafuta fursa kwa ajili ya raia, ni kwamba haya masoko hawayaoni?
Juzi limeongelewa swala la Veta, watu hawakulipokea vizuri. Kwa sababu mara nyingi, vitu watu wanavyolishwa darasani, havina uhalisia wa maisha ya nje.
Hizi Cold rooms, ni kwamba nchi haina uwezo wa kuwadhamini wakulima?
Je, Certificates zinazohitajika kupeleka vitu hivi nje,ndo hazipatikani?
Hakuna wale wasomi wa mambo ya kilimo waliopelekwa Israel kwa pesa ya serikali? Ujuzi waliopata huko umelisaidia nini taifa?
Mashirika ya misaada, yanayonunua vyakula, kwa nini Tanzania ibaki, wakati ina kila kitu!
Miaka ya nyuma nchi moja jirani, nilishuhudia watu wakija kukagua na kuelekeza wakulima namna ya kutunza mahindi yao hadi wakati wa mavuno. Watu hawa, walinunua mahindi,kwa kilo, bila kuyapukutua. Hakika ni faida kwa mkulima.
Kwa nini wakulima wasielimishwe, wafanye kilimo cha kibiashara, na hawa wasomi wasio na ajira, wajiajili kwenye kilimo!
Kampuni za bima zihusishwe pia.