Kwa nini Watanzania hatuwapendi polisi?

Wanachi wana machungu na serikali, hivyo wengi wanaojifanya kuwa ndio serikali wana nchi wanawachukia. Sio polisi tu hata mtendaji wa kijiji, kata nk.
Kwa polisi kuna kosa la ziada wanalofanya:

Mtuhumiwa akipelekwa kituoni wao wanamuona kama ana hatia tayari Mambo wanayomfanyia utadhani amekwisha patikana na hatia wakati sheria inasema mtuhumiwa hana hatia hadi mahakama ithibitishe hivyo.

Watampiga, watamlaza mahabusu (tena mahabusu zinaachwa kuwa chafu na kunuka ili ukiingia humo uombe kutoka haraka kwa gharama yoyote ile), na vimbwanga vingi tu.
 
NIMESOMA MICHANGO YA WATU MBALIMBALI....NGOJA NAMI NITOE MAWILI AU MATATU....!

1.RUSHWA:Hili ni tatizo kubwa lililopo katika vitengo mbalimbali vya wizara hii ya polisi(iite jina lolote ila ni wizara inayoshughulikia mabo yao tu) POLISI,TRAFFICK, ANT-ROBBERY, CID,FFU (tigo), DPP.

PASIPO KUJALI MAHUSIANO YAKO NA WAO (polisi mwezao,raia tu, hakimu,mwanajeshi, mstaafu wa jeshi, usalama, magereza, uhamiaji, na kadhalika) hupati iliyo haki kwako katika jambo lililokukutanisha nao pasipo kutoa chochote.

2.KUBAMBIKIA: Unaweza dhani kuna kitengo maalum cha kubambikia (KUPEWA CASE ISIYO YAKO). Traffick kwenye ajali atachora mchoro tofauti, atakusimamisha kukwambia umevuka kwenye taa nyekundu, daladala ataambiwa amepakia pasipo kituo.

POLISI wa kawaida(general duty) utapelekwa kituoni kwa kosa "say" la uzururaji, ukifika kituoni unaambiwa UMEKAMTWA NA SMG ILIYOKATWA KITAKO YENYE RISASI 80.

Mauzauza ni mengi

3.DHARAU/KIBURI/UBABE/NO USTAARABU: Pale unapofika kituoni kupeleka shida yako, say LOSS REPORT, PF3, RB nk lugha utakazo kutana nazo, kama si wewe mwenye shida unaweza ukaacha shida yako ukageuza kurudi uendelee na shughuli zako

YOTE HAYA NA MENGINE MENGI....YANAFANYA MAHUSIANO NA RAIA YAWE TETE........PAMOJA NA KUTAMBULISHA POLISI JAMII BADO NI ONE TRAFFICK SITUATION NA SI TWO TRAFFICK SITUATION.....!

YAANI CHAKO CHANGU NA CHANGU CHANGU


Wanapenda raia washirikiane nao lakini wao hawako tayari kushirikiana na raia INAPOFIKA KIPINDI SASA RAIA NAO WANAHITAJI MSAADA (WAJIBU) WAO
 
Hawa polisi wetu noma sana, ni heri mtu ukutane na kibaka wakati wa usiku kuliko polisi - we ni raia mwema umetoka kwenye mihangaiko yako hawakuelewi utakesha nao ukilinda kama huna chochote cha kuwapa !!! bora kibaka weza kukuruka na ukakimbia bila kukuibia !!!!
 
Jamani leo nimejionea mwenyewe kwa macho yangu polisi kapigwa na tofali, akadondoka chini, raia wakawa wanashabikia na wala wahakumsaidia polisi kuinuka wala kumkamata aliye mpiga. Nimeshangaa sana

skiliza wimbo wa icecube unaitwa **** tha police
 
wanapenda sana chai tena wanaomba kabisa bila aibu, ubabe, pia kutokusaidia ASAP inapotakiwa yani kujivuta kufika eneo la tukio, kusaidiana na majambazi/wezi, upepelezi usio na ripoti kila siku yaani ovyo kabisa..wengi wao hawajui 'ethics' za kazi zao na hawatilii maanani! hawana maana kwenye taifa.
 
Jamani leo nimejionea mwenyewe kwa macho yangu polisi kapigwa na tofali, akadondoka chini, raia wakawa wanashabikia na wala wahakumsaidia polisi kuinuka wala kumkamata aliye mpiga. Nimeshangaa sana
Jeshi lote?
Fafanua kaka/dada maana hawa maafande wana rank tafauti pia uelewa wao ni tafauti....japo sijui hivyo vyeo vyao wanapeana kwa vigezo gani?
Hata mimi hawa makonstebo siwapendi kabisa....
Wajitia wanajua kumbe hawajijui.
Rai wakakamavu hao!.
 
Back
Top Bottom