Kwa nini wanaume hamtukubali na watoto

Kwa nini wanaume hamtukubali na watoto

Na ukimshauri munagombana tena na siraha anabeba, sasa naisi kafanywa vibaya huyu kijana.. aaambiliki

Kapewa vitu adimu kadata. Ila kuna mkaka namjua kaoa mwanamke ana watoto watatu, na yeye kajiongezea wa NNE na life linasonga. Wanga tumeteta tumechokaa....
 
Ni swala la ajabu sana ambalo pengine ukilifukiria unaeza ukasikitika

ni kawaida sana wanaume kutuambiwa wana watoto hata watatu na wenyewe kuona kawaida sana bila hata kutushawishi kwamba utaishi na mwanangu

yaani wao uchukulia kawaida sana sisi kuishi na watoto wao bila kuuliza chochote na wao huona sinkikwazo chochote na pindi utakapokionesha basi unaonekana Mkatili unaonekana wewe sio mke mwema(JAPO KUNA WANAWAKE HUKATAA ) ila sio wengi

SASA IJE SISI NDO TUNA WATOTO
wanaume wengi hukataa kuoa mwanamke mwenye mtoto KWA MSISITIZO na hata kama akikubali husema basi mtoto wako akae kwa bibi au baba ake sijui atawajibika
na mambo mengi hapo katikati

SASA SWALI NI JE KWANINI NYIE MNAONA SISI KUKAA NA WATOTO WENU NI RAHISI LAKINI NYINYI KUKAA NA WETU NI ISSUE tena kubwa sana????

Kwetu bado uchumi ni mzuri uchumi ukiwa mbaya kazi hakuna ardhi haipatikani mbona wanaume watawaowa tu wanawake wenye wtt hatavwatano cha muhimu wewe mwanamke uwe na pesa za kutosha. Kuna nchi nimeishi wanawake wenye watt wanaolewa bila shida as long as u ve money!
 
Ukitaka ujue hawaongezi kitu omba upate matatizo ndo utajua.....



unafiki wa baadhi ya wanafamilia unakuja pale muhusika au kijana alieoa akiwa hana kitu na amepata matatizo kwenye huo uchaguzi wake lkn ikitokea kijana mambo safi familia nzima itakuwa upande wake na pia haiwezi kutokea familia nzima ikuchukie kwa jambo hilo tu la kuoa kana kwamba wewe ndo ulianzisha utamaduni huo
 
sioni sababu ya mama mkwe,mawifi kuchukia kisa kaka kaoa mke mwenye mtoto wajiulize nao ni wanawake na huyo mama ana mabinti ikitokea binti yake kaolewa bahati mbaya mume kafariki/kuachika na ana watoto bahat nzuri kaolewa tena atajisikiaje akiona binti yake anasimangwa kwaajili ya watoto aliokutwa nao? haya mambo yanahitaji hekma katika kuyamua endapo ikitokea

Wajane huwa hawapati tabu sana....tabu aliezalishwa kabla ya ndoa
 
sioni sababu ya mama mkwe,mawifi kuchukia kisa kaka kaoa mke mwenye mtoto wajiulize nao ni wanawake na huyo mama ana mabinti ikitokea binti yake kaolewa bahati mbaya mume kafariki/kuachika na ana watoto bahat nzuri kaolewa tena atajisikiaje akiona binti yake anasimangwa kwaajili ya watoto aliokutwa nao? haya mambo yanahitaji hekma katika kuyamua endapo ikitokea

kama hujaoa bado jaribu siku moja kuwaambia dada zako kuwa una mchumba ambaye untarajia kumwoa ila ana mtoto uone respond yao
 
unafiki wa baadhi ya wanafamilia unakuja pale muhusika au kijana alieoa akiwa hana kitu na amepata matatizo kwenye huo uchaguzi wake lkn ikitokea kijana mambo safi familia nzima itakuwa upande wake na pia haiwezi kutokea familia nzima ikuchukie kwa jambo hilo tu la kuoa kana kwamba wewe ndo ulianzisha utamaduni huo

Mkuu nna mifano ya watu na uwezo wao lakini wanatengwa kawaida tena wao inakua mbaya zaidi aseee,kwamba si anaringa vile anahela mwache......
Kuna familia zina misimamo balaaa hata uwe na Pesa lazima uende ktk miiko yao
 
Kwasababu aliyekuzalisha atakukula mda wowote
And siwezi kukaa na amani 100% wakat najua kuna mtu mkewangu hawezi kumnyima
Fullstop
 
Kuishi na mwanamke mwenye mtoto ni kazi sana, kwana wanawake wenzake watapinga kuona ndugu yao au mwanao anaoa mwanamke mwenye mtoto, hata ukiona mwanamke mkubwa umri ni shida wanawake hawapendani wao kwa wao, mwanamke ni rahis kurudisha mapenzi kwa aliyezaa naye hilo ndo linalowaumiza wengi ili hali matunzo yote yatakuwa kwa mwanaume, nitaoa mwanamke mwenye mtoto ambaye mzaz mwenzie hayupo duniani otherwise sitaoa mwanamke aliyezaa
 
Kila mtu atabeba msalaba wake, uroda umpe nan, me nije kulea toto
 
He hata km ni utafiti hii mada kweli imeconfirm, wanaume ni selfish individuals...
 
wanawake wengi ni wabinafsi ndiyo maana wanaume wengi wanawakwepa kuwaowa make ukiowa mwanamke mwenye mtoto hatataka hata umfokee mtoto wake akifanya makosa.
 
Kamwe siwezi ishi na mwanamke aliyezaa tayari kwengine huko

Kwanza wanawake wa siku hizi wengi wana akili za kushikiwa na rahic hata kupasha kiporo na baba mtoto wake

Pili dunia ya leo mzazi na mwanae na ndiye rafiki wa kweli, sasa utalea mtoto wa mwanaume mwenzio tena unaangaika kuchapa kazi kwa juhud na kumuendeleza mwisho wa siku thamani yako aiwez kuwa kubwa kuliko ya baba yake aliyemzaa ingawa akumtunza hata kidogo.
 
Suala hili linasababishwa na unafiki. Msingi makubwa wa ndoa pamoja na mambo mengine ni kumsitiri mwenza wako. Ukiona mwanaume anakataa mwanamke kisa amezaa ujue sababu sio kutunza mtoto bali ile fadhaa ya kujiona na kufikiri kachukua kitu "second hand". Pengine na utamaduni wetu unachangia kwani kwa wenzentu waganda huona fahari kuoa mtu mwenye mtoto. "Nothing is good or bad but your thinking make it so."
 
Back
Top Bottom