Kwa nini Umseme Vibaya EX wako?

Kwa nini Umseme Vibaya EX wako?

Decapitator

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
311
Reaction score
79
Nimekua nikiona na kusikia watu wakiwasema vibaya wapenzi wao wa zamani, na hata wakati mwingine kutoa hata siri za ndani ambazo hazipaswi kuelezwa kwa watu wengine.
Unaweza kuta labda ye ndio kaachwa , au kaacha haijalishi!.
Je ni kushindwa kuhimili maumivu?, au ndio siku zote lazima apatikane wa kulaumiwa.

Swali kwako mwana JF, kwa nini Utoe siri za Mpenzi wako wa zamani.
Kwa nini Umseme kwa Mabaya tuu ?.


Karibuni.
 
Hapo kitu kikubwa ni kushindwa kukubaliana na khali halisi hasahasa kama mtu ameachwa ndio hua tabu sana,kwa kumsema ex wake vibaya hasira huisha.
 
Mi nahisi ni mtu kukosa busara tuu, sidhani kama kumsema vibaya inahusiana na kupungua kwa hasira ..... Giti
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kwa nini muanze kuzungumzia mambo ya ma-ex...
Huo ni udhaifu, kutokubaliana na ukweli, kuumia nafsi. nk nk
 
  • Thanks
Reactions: MZK
kubwagwa inuma bwana wee...unaweza ua mtu unajua!! mtu unawaza ulivyomcare na kusacrifice alafu ghafla anakwambia chukua hamssini zako ni mbaya sana
 
@Eli79 wengine wanapenda sana kusema tena kwa kubwatuka,.... siwasemi vibaya watoto wa kike ila wengi wao hufanya hivyo though hata wanaume japo si sana.
 
Lakini mzabzab hizo hasira na kuwaambia watu siri zake za ndani zinahusiana nini?
Nakubali ndio inauma sana.
 
Last edited by a moderator:
Haina maana na haisaidii kumuongelea vibaya,sio Ex tu,mtu mwingine yoyote
 
Ukimuona mtu anasema vibaya x wake ujue bado anamtaka ila ndio kashapigwa kibuti tena...lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
hiyo ni kupunguza machungu tu ya kuachwa,pengine yanayosemwa huwa mengine ya uwongo
 
enhanced-buzz-14759-1368215268-18.jpg
 
hivi na yule aliyenyang'anywa laptop akaja kulia lia humu, hivi alinyonya hata maziwa kweli?

si aliishia kuliwa vingi bila msaada wowote?
 
mkuu Tyta naona umekuwa mzee wa kutupiamo mapicha. kazi kwao team weka picha
 
Last edited by a moderator:
mi kwa kweli nisiseme uongo!!

x wangu huwa namsema kabisaaaaaa!!!!!!!

ila kwa mazuri tu! nilishamjengea nyumba, nikamnunulia gari tatu za kutembelea nje na ndani,

wazazi wake nikawajengea japo nyumba ndogo si haba, nikawapa mtaji wa biashara, kila wiki anapata safari za dubai na oman kufanya shopping za duka lake la nguo za kike,nimemjengea ofisi yake ya filamu, mshahara wangu anaupokea yeye.. na mambo mengine meengi mazuri!!..

....by.. clement, to sepetunga!!!!
 
Back
Top Bottom