Kwa nini tunalia msibani?

dazu

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
365
76
Unapotokea msiba, tunalia sana. Hasa ndugu na jamaa wa karibu. Uchunguzi usio rasmi umeonesha kwamba, kila mmoja hulia kwa sababu tofauti na ni wachache sana ambao wanalia kwa mapenzi ya dhati waliyonayo kwa marehemu (wanaulilia utu wake). Wengi wanajililia wenyewe kwamba misaada au faida mbalimbali ambazo wamekua wanazipata kutoka kwa marehemu hawatazipata tena. Mfano, leo kuna taarifa kwamba 'babu' wa Loliondo amepata msiba. Huku kwetu taarifa hizo zilipotoshwa kwamba 'babu' amefariki. Watu wamesikitika na wengine kulia sana. Nimejiuliza; wanamlilia 'babu' au wanaililia dawa yake? ....Unapolia msibani, unamlilia marehemu au unalilia faida utakazozikosa kutokana na kifo chake? Tutafakari waungwana.
 
:rip:...majibu yenyewe si haya bana?;

Kumlilia marehemu na pia faida zitakazokosekana ambazo zingetolewa na marehemu!
 
Mbu hivi huwa unalia kwenye msiba? lol

...halafu unajua bro? ...kuamkia leo nimeota msiba bana. Mw'Mungu apishilie mbali.
Naelekea job mida hii, inabidi kwenye pedestrian crossings niwe extra careful!
Hujanijibu kule kwa 'watarajiwa wa ajabu' kuhusu Royal Wedding Coverage!
 
Halafu kwenye misiba mingi akina mama wanalia sana kuliko akina baba!
 
...halafu unajua bro? ...kuamkia leo nimeota msiba bana. Mw'Mungu apishilie mbali.
Naelekea job mida hii, inabidi kwenye pedestrian crossings niwe extra careful!
Hujanijibu kule kwa 'watarajiwa wa ajabu' kuhusu Royal Wedding Coverage!
Ngoja nikujibu nichungulie huko, Mungu akuepushe mkuu
 
huwezi amini mie nilienda msibani badala ya kumlilia yule merehemu nikawa nakumbuka kifo cha rafiki yangu mpenzi na kubwaga chozi has ,lakini jibu ndo hilo kila mtu analia kwa sababu zake
 
Unapotokea msiba, tunalia sana. Hasa ndugu na jamaa wa karibu. Uchunguzi usio rasmi umeonesha kwamba, kila mmoja hulia kwa sababu tofauti na ni wachache sana ambao wanalia kwa mapenzi ya dhati waliyonayo kwa marehemu (wanaulilia utu wake). Wengi wanajililia wenyewe kwamba misaada au faida mbalimbali ambazo wamekua wanazipata kutoka kwa marehemu hawatazipata tena. Mfano, leo kuna taarifa kwamba 'babu' wa Loliondo amepata msiba. Huku kwetu taarifa hizo zilipotoshwa kwamba 'babu' amefariki. Watu wamesikitika na wengine kulia sana. Nimejiuliza; wanamlilia 'babu' au wanaililia dawa yake? ....Unapolia msibani, unamlilia marehemu au unalilia faida utakazozikosa kutokana na kifo chake? Tutafakari waungwana.

Dazu I would genuinly like to know kama umewahi fiwa na mtu wa karibu na mhimu kwako.
 
...halafu unajua bro? ...kuamkia leo nimeota msiba bana. Mw'Mungu apishilie mbali.
Naelekea job mida hii, inabidi kwenye pedestrian crossings niwe extra careful!
Hujanijibu kule kwa 'watarajiwa wa ajabu' kuhusu Royal Wedding Coverage!

Mbu usiwe na wasi juu ya ndoto hiyo. Hiyo ni dalili ya furaha utakayoipata. Ila usipende kuweka ndoto zako hadharani coz hata asiyojua anaweza kujidai kuitafsiri kumbe sivyo na baadae yakakuta kulingana na tafsiri yake.
 
huwezi amini mie nilienda msibani badala ya kumlilia yule merehemu nikawa nakumbuka kifo cha rafiki yangu mpenzi na kubwaga chozi has ,lakini jibu ndo hilo kila mtu analia kwa sababu zake

Ewala we umenena.
 
Dazu,mada yako imenishtua,sina hata wiki mbili babangu mzazi amefariki,simanzi niliyonayo hata kuieleza siwezi,hebu nieleze Dazu ushawahi kufiwa na mtu wako wa karibu sana? i mean mzazi,kaka

,dada,mtoto(kama ushawahi kuwa nae),rafiki,jirani,office mate,school mate.....?
 
Jamani mimi nilikuwa nalia sana misibani, ila tangu nimemjua Mungu sipati machozi kabisa. Sometimes watu wanashangaa kwa nini sipati machozi. Sina mawazo yoyote wala sina tatizo la kunifanya nilie. what i know mwenzetu ametangulia mbele ya haki akaanze maisha mapya mazuri kuliko haya aliyokuwako. Nilichojifunza tu ni kuwaombea wapendwa wetu walale mahali pema peponi.

Ila sisemi watu msilie, kama mtoa mada alivyosema, wengi tunalia hasa kwa sababu ya shida zetu. Kwa wafiwa nasema uchungu wa kufiwa na wapendwa wao.
 
ni njia tu ya ku-control emotions zako mamii. Kuna wengine hata kufurahi tu tunalia.when we feel loved,or cared for even by total strangers machozi yanatoka na najua Mungu anatimiza ahadi yake ya kunitumia malaika.Unalia hata wakati unaagana na mtu anayeondoka say kwa mwaka manake utamisi ukaribu wenu pia
Dazu,kuna rafiki yangu nilipofiwa na mama alinitumia msg akasema haelewi aniambie nn manake hajawahi kufiwa na mtu wa karibu.alipofiwa na babaye 2 yrs later akawa ananiambia kila mara tell me how to cope.Ukweli ni kwamba unaweza kulia msibani kwa ajili ya kukumbuka ya kwako

Back
Top Bottom