Kwa nini Shela ya Harusi haina thamani tena??

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
Hili ni swali... kwa ninavyojua mimi shela (vazi jeupe lenye kifuniko..) ya harusi huvaliwa na mwanamke "bikira" wakati wa kufunga ndoa.. ila siku hizi hata wenye mimba za miezi tisa wanavaa na wanaingia makanisani na ndoa inafungwa..

Angalia kituko huko Tanga..........

Bibi harusi ashikwa uchungu, ajifungua kanisani Muheza
Thursday, 11 August 2011 21:16


Mwandishi Wetu, Muheza
BIBI harusi aliyefahamika kwa jina la Mariam Shabani, ameshikwa na uchungu wa kujifungua kanisani wakati akifungishwa ndoa na mchumba wake, aliyefahamika kwa jina la Deo Massawe.Tukio hilo lilitokea juzi Kanisa Katoliki lililopo maeneo ya Majengo Shimoni, wilayani Muheza, huku umati wa watu ukiwa umejaa ndani ya kanisa hilo ukiisubiri kufungwa kwa ndoa hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa hilo, wakati Padri Martin Kihiyo, akiendelea na misa ya kufungisha ndoa hiyo, ghafla bibi harusi akiwa amevaa vazi rasmi la harusi, alianza kupiga kelele akidai anasikia uchungu wa kujifungua.

Hata hivyo, baada ya bibi harusi huyo kupiga kelele, Padri Kihiyo alisitisha misa hiyo na Mariamu kuchukuliwa haraka na kuwekwa kwenye gari huku akiwa hajiwezi hadi Hospitali Teule Muheza.Pia, Mariamu anafahamika kwa jina la Sada Shabani, baada ya kufikishwa hospitali alipelekwa chumba cha kujifungulia huku akiwa na vazi lake la harusi.

Baada ya kuhudumiwa Mariamu, alijifungua mtoto wa kike na kulazwa wodi ya Azimio wanakolazwa wazazi.
Mmoja wa muuguzi hospitalini hapo aliyeomba asitajwe, alisema bibi harusi huyo alijifungua njiti akiwa na miezi saba.Kwa upande mwingine, kwenye ukumbi ambao ulikuwa umeandaliwa kwa sherehe ya harusi hiyo, watu walikuwa wamekaa ndani wakisubiri maharusi bila kufahamu kilichokuwa kikiendelea.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo bwana harusi alilazimika kufunga ndoa na msichana mwingine wa pembeni kwa niaba ya bibi harusi, ili kuhalalisha sherehe hiyo huku bibi harusi mwenyewe akiwa hospitali analea.

Inasemekana Mariamu alianza kusikia uchungu akiwa saluni na aliwaeleza baadhi ya watu, lakini walimjibu kuwa huo ni woga wa harusi.Katika hatua nyingine, mbuzi wa ndafu aliyekuwa ameandaliwa alianguka chini kwenye mchanga.

Baadhi ya Wakristo walisikitishwa na tabia ya viongozi wa dini kuendelea kuwafungisha ndoa watu ambao wake zao wana mimba kwamba, ni aibu.




Swali la kujiuliza: (i) hapa ni viongozi wa dini kukosa mwelekeo na kubaki kuangalia sadaka tu??
(ii) maadili ya yameporomoka??
(iii)watu hawana tena hofu ya Mungu??
 
Point no 1 ina nafasi kubwa sana,viongozi wetu wa kanisa ndio wamelea hii tabia,nadhani makanisa ya kilokole hii tabia haijashika kasi,watumishi wa Mungu wanapaswa kusimama ktk kweli.
 
Point no 1 ina nafasi kubwa sana,viongozi wetu wa kanisa ndio wamelea hii tabia,nadhani makanisa ya kilokole hii tabia haijashika kasi,watumishi wa Mungu wanapaswa kusimama ktk kweli.
<br />
<br />

Wana bahati sana hao, wamepunguza gharama za birthday ya mwanao na anniversary ya harusi yao parties maana vitaenda pamoja, a lucky couple!!
 
Point no 1 ina nafasi kubwa sana,viongozi wetu wa kanisa ndio wamelea hii tabia,nadhani makanisa ya kilokole hii tabia haijashika kasi,watumishi wa Mungu wanapaswa kusimama ktk kweli.

nimependa jibu lako..tena ukizingatia location lako ni kanisani... wewe ni Parish worker nini!!
 
Bibi_harusi.jpg

Umuhimu wa shela umekwisha kwa wote kanisani na kwa waolewaji.
 
(iii) hofu ya mungu hakuna) Zamani msichana aliyekuwa anaruhusiwa kuvaa shela nyeupe ni yule ambaye hajawahi kuishi na mwanaume wala kuzaa. Tofauti na hivyo achague rangi nyingine sio nyeupe. Lakn sasa hivi ni mchanganyo kwenda mbele. Ndio mambo kama haya yanatokea. Ee Mungu uturehemu.
 
Wasichana wengi siku izi wanatoa mimba, ni vizuri kujihakikishia unacho-oa ni ridhiki.
 
Kwa sababu hata wamama wenye watoto wanavaa na wengine wameshafunga ndoa zaidi ya mara moja na wao pia wanang'ang'ania kuvaa....mweee
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom