OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,247
- 103,953
Katika video hii Gwajima anasema;
Sio kwamba Makonda au Bashite hafai kwenye kila kitu,lakini hajawa matured enough kwenye mambo ya utawala kama mkuu wa mkoa. Kwa hiyo namuomba kwa heshima na taadhima mh. Rais amtafutie mahala pengine. Mambo ya utawala yanaweza kumfanya atuchafue na akuchafue wewe mbele ya macho ya wananchi. Ukiendelea kumuacha iko siku atafanya jambo Bashite huyu utatoka moshi watu mtashindwa kufungua macho
Haya ni maneno ya Gwajima kipindi Makonda anawataja kina Gwajima,Mbowe,Manji kwamba wanajihusisha na madawa ya kulevya
Sasa tunashuhudia Tanzania inavyochafuka kimataifa. Pamoja na wizara ya mambo ya nje kukanusha tamko la Makonda bado mamlaka ya uteuzi haioni ulazima wa kumpangia Makonda majukumu mengine. Wahenga wanasema samaki mkunje angali mbichi