Kwa nini Magufuli alikataa ushauri huu wa Gwajima kuhusu Makonda?!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,064
103,271


Katika video hii Gwajima anasema;

Sio kwamba Makonda au Bashite hafai kwenye kila kitu,lakini hajawa matured enough kwenye mambo ya utawala kama mkuu wa mkoa. Kwa hiyo namuomba kwa heshima na taadhima mh. Rais amtafutie mahala pengine. Mambo ya utawala yanaweza kumfanya atuchafue na akuchafue wewe mbele ya macho ya wananchi. Ukiendelea kumuacha iko siku atafanya jambo Bashite huyu utatoka moshi watu mtashindwa kufungua macho

Haya ni maneno ya Gwajima kipindi Makonda anawataja kina Gwajima,Mbowe,Manji kwamba wanajihusisha na madawa ya kulevya

Sasa tunashuhudia Tanzania inavyochafuka kimataifa. Pamoja na wizara ya mambo ya nje kukanusha tamko la Makonda bado mamlaka ya uteuzi haioni ulazima wa kumpangia Makonda majukumu mengine. Wahenga wanasema samaki mkunje angali mbichi
 
Ina maana unaamini Makonda ndiye kachafua Tanzania? Mbona kila mtu ana tope mikononi!
 
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda huko nchini kwa sasa, mtakuja kusikia wanaume wote wa Dar mnatakiwa kwenda Lugalo kubangua Korosho.

Hahahahaha ila JF tunaonaga mbali kwa kweli. Ni kam mmja alisema ukitaka kumpiga picha mke wako inabidi uende TCRA ukaombe kibali.

Juzi juzi walikuwa wanawakamata watu waliovaa vibaya. Kama unavaa vibaya basi polisi wanakukamata kisha wanakupandisha kwenye defender. Ila Bashite ameligharimu nchi, bunge, mahakama ameinajisi alifaa akatwe kichwa kabisa
 
Ni kwa sababu tu ya mahusiano yasiyo ya kawaida. Angeshapigwa chini. Kashfa kama ya makontaina, uvamizi wa chombo cha habari, kuikejeli bunge nk visingemwacha salama.
 
Back
Top Bottom