Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,704
- 9,060
Kwa sasa siyo siri tena kwamba kuna Vita kali na ya chinichini inaendelea kati ya RC Makonda akisaidiwa na Rais Magufuli zidi ya Mawaziri wa Serikali ya CCM na Bunge la JMT.Hii vita ilianza kama vita ya mzaha mzaha kati ya Daudi Bashite a.k.a Paulo C. Makonda na Gwajima lakini sasa imepamba moto na mwisho wake ni mlipuko ambao kuna watu wataumia sana.
Kitendo cha RC Makonda kukingiwa kifua na Mkuu wa nchi kwa makosa aliyo nayo na anayoendelea kuyafanya mbele yz macho ya Watanzania inazidi kujenga chuki kubwa sana kati ya Magufuli na Baraza lake la Mawaziri. Rais anafanya makosa makubwa sana ya kiufundi na kiutawala kumfanya RC Daudi Bashite Paulo Makonda aonekana kuwa yeye yuko juu ya Mawaziri na hata zaidi ya Waziri Mkuu mwenyewe. Kwamba RC Bashite anakingiwa kifua na Rais asitumbuliwe hata baada ya ushahidi wa kuwa ameingia kwenye ajira kwa kutumia vyeti fake.
Lakini pia kama hilo halitoshi kuna hili la juzi kwa RC Bashite kuvamia kituo cha CLOUDS TV akilazimisha SHILAWADU warushe hewani kipindi kilichoandaliwa kwa ufadhili wake ili kumchafua Askofu Gwajima. Waziri mwenye dhamana, Habari Utamaduni na Michezo Mhe. Nnape Nauye kaamua kuchukua hatua kuhusu swala hilo lakini kabla hata hajaanza mchakato Rais anahutubia kwa kumsifia RC Makonda aendelee kuchapa kazi. Maana yake ni kwamba aendelee kuvamia vituo vya TV, Radio na Magazeti kwa vile ana baraka zote za Mkuu wa nchi!
Rais amekwenda mbali zaidi hata kusema kuwa RC Makonda ana uhuru wa kufanya chochote na yeye ataendelea kum-support. Haya matukio ya kwenye mitandao, kuwa sijui ana vyeti fake, kavamia CLOUDS TV ni mambo ya UDAKU tu hivo aendelee kuchapa Kazi. Hapa Kazi tu!!! Kwa hali ya kawaida Waziri mwenye dhamana hata kubaliana na msimamo wa Rais kuhusu Makonda. Waziri ni mtu aliyepewa dhamana ya kushughulikia maswala ya Habari, Michezo na Utamaduni kwa nchi nzima na lazima asimamie hilo. Inapotokea Mkuu wa Mkoa anayeangalia Mkoa peke yake anaanza kupingana na Mawaziri ujue kuna Vita kali na matokeo yake ni mlipuko ambao matokeo ni Serikali kujeruhiwa au kufa kabisa. Tayari Kamati ya Waziri Nnape imemaliza Uchunguzi wake kuhusu sakata la CLOUDS TV lakini imezuiwa na Rais Magufuli kuweka taarifa yake hadharani. This is what we call it Management by Crisis!! Huu ni uongozi ulioparaganyika. Katika nchi za wenzetu Waziri Nnape angelikuwa ameshatangaza kujiuzulu mara moja kwa kuingiliwa katika mamlaka aliyo nayo Kikatiba.
Daudi Bashite a.k.a Paulo Makonda ana kesi ya kujibu mbele ya Bunge baada ya kulidhalilisha Bunge kwa kuwatukana Wabunge. Bashite leo kavamia Kituo cha TV na Waziri anaunda Kamati ya Uchunguzi kulingana na sheria na kanuni lakini anafungwa mikono. Juzi Waziri wa Sheria na Katiba Daktari Mwakyembe kapingana na Rais wake kuhusu agizo la kufunga ndoa kwamba lazima kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Sina hakika Mwakyembe huko aliko anajisikiaje lakini ni wazi kuwa atakuwa amedhalilishwa na majibu ya Rais wake Magufuli. Kwa Rais mwungwana alipaswa kumwita Waziri wake na kumwambia alirekebishe hilo kwa lugha ya kidiplomasia. Lakini hilo hailkufanyika na hii inaonyesha picha kuwa hii Serikali haifanyi kazi kama TIMU MOJA kila mtu na lwake. Kwa namna fulani Rais polepole anaanza kujikuta akiwa amebakia yeye na Makonda wake huku Mawaziri wakikaa pembeni ili waone jinsi nchi ianvyoendeshwa na Watu 2 tu yaani Rais John Joseph Pombe Magufuli na RC Daudi Albert Bashite Paulo Makonda.
Nimalize kwa kutoa Ushauri kwa BARAZA LA MAWAZIRI wote wa SERIKALI YA CCM kwamba hapa ilipofikia lazima waseme Hapa Kazi Tu imetosha. Mawaziri wote waungane pamoja na Wabunge wa Upinzani ili kumshikisha ADABU Rais Magufuli na kijana wake mpendwa Daudi Bashite. Wajipange kuing'oa serikali ya Magufuli kwa KUPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU. Hili linawezekana kulinga na Katiba na Kanuni za Bunge. Hilo likishakamilika na kupita ina maana Serikali ya Magufuli itavunjwa na Uchaguzi Mkuu utaitishwa tena. Hapa mdipo mahali pa kumwonyesha Magufuli kuwa HAKUINGIA IKULU KWA AKILI ZAKE, KWA NGUVU ZAKE WALA KWA UBABE WAKE. Hapa ndipo atakapojua nini maana ya KURA ZA WATANZANIA WALIOMPIGIA KURA MWAKA 2015 ILI AINGIE IKULU LAKINI LEO ANAWATUKANA WATANZANIA KUWA HAKUNA ALIYEMWAMBIA ACHUKUE FOMU!!!
Naomba kuwasilisha.