Gwajima anaendelea kumshikia bango Makonda, adai amekimbia nchi kama Magufuli alivyotabiri

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,156
2,000

Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.

Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.

“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema

Gwajima alisema kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki ni kifungo cha miaka mitatu.

Kosa jingine alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.

======

MUNGU KATIKA NCHI”
Bishop Dr Josephat Gwajima
Jumapili ya Tarehe 12.03.2017
Ufufuo na Uzima Tanzania

Yesu alipokuwa na wanafunzi wake walimwambia Mwalimu tufundishe kuomba kama ambavyo Yohana alivyo wafundisha wanafunzi wake. Yesu akawaambia mkitaka kuomba ombeni hivi:-

Baba yetu uliye Mbinguni Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje.
Hii ilikuwa kuwaonyesha kuwa hapa duniani kuna Ufalme mwingine ambao ni Ufalme wa Mungu na pia upo Ufalme wa shetani wa kuzimu. Aliwafundisha waombe kwa kujua Baba yao yupo mbinguni na jina lake ni kuu si dogo, ufalme wake uje hapa duniani (maana yake mila ya mbinguni ihamie duniani.
NATAKA UTEMBEE KWENYE NGAZI NYINGINE YA MAARIFA,

Kwenye ulimwengu wa Roho kuna majini, mashetani, n.k hawa sasa tunapopigana vita vya rohoni na kuwashinda lazima tujue kwamba shetani baba yao alishahamia kwenye ulimwengu wa roho na amevaa mwili anaonekana kama mwanadamu analindwa na sharia za wanadamu kumbe ni shetani amekuja kuharibu kazi ya Mungu duniani.

Sisi tunapokuwa na nia ya Mungu ndani ya Yesu kile tunachokigusa ni Mungu amekigusa, kile tunachokisema ni Mungu amekisema. Kile tunachokipiga ni Mungu amekipiga, kile tunachokikemea ni Mung anakua amekikemea.
Na wachawi nao wamevaa nia ya ibilisi wakitenda ibilisi ametenda, hivyo ukisema kuwa unamuachia Mungu unakuwa unakosea maana ndani yako tari una nia ya Mungu, ubebe hiyo nia ndani yako.

Mataifa yote tumepewa, (nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu.
Kwanini manabii wa zamani walikuwa wanatabiri na mambo yanatokea, kwa sababu waliibeba ile nia ya Mungu ndani yao. Kile walichokua wakikisema ni Mungu anakua amesma na sisi ndivyohivyo sababu hutakaa umuone Mungu anakuja kutenda kwaniaba yako sababu tayari ameshatuoatia mamlaka ya kutawala hapa duniani na chochote tunachokisema kinatokea vilevile.
Lazima tufahamu kuwa sisi tumeumbwa kwa suna na mfano wa Mungu, kwa sababu hiyo tuna sura ya Mungu, tuna asili ya Mungu, tuna kinywa cha Mungu na tuna mamlaka kwa sababu tumezaliwa na Mungu.

Sisi ndio wana wa Mungu na sisi ndio tunawakilisha Ufalme wa Mungu duniani. Kama sisis ndio wana wa Mungu ndio tunatenda kazi duniani, ukisema namwachia Mungu unakosea kwa kuwa Mungu alishatupa mamlaka. Ndani yetu kuna Yesu tukigusa Mungu amegusa, tukitembea Mungu ametembea Duniani.

KILA MTU ANA AKILI YAKE
- Mwingine ana akili ya kumtosha yeye peke yake.
- Kuna mwingine ana akili ya kumtosha yeye na mke wake.
- Mwingine akili yake inamtosha yeye mke wake na watoto wake
- Kuna mwingine ana akili ya kumtosha yeye na familia yake na majirani. (Huyu anaweza akawa kiongozi)
- Kuna mwingine akili yake hata yeye mwenyewe haimtoshi, yaani haziwezi kumsaidia kujua kipi kizuri au kipi kibaya.

Imani ni nini
Imani ni kuchukua neno la Mungu unalifikiria alafu unalishika unaliweka ndani ya moyo wako na ukisema sitakufa unatumia ile Imani haufi kizembe sababu Mungu anaongea ndani yako kupitia neno lake kwa Imani yako.

Kinyume cha Imani ni woga, ukianza kuogopa Imani inapungua ndani yako, kiwango cha Imani alichonacho mtu ndio ujasiri alionao mtu. Ukiwa mtu wa kusikiliza maneno ya kukuvunja moyo na viticho utakua na uoga bila kujijua sababu umesikiliza ukaamini huwezi na ukabaki mnyonge.
Nia ya Mungu ndio Imani yako, unapobeba neno la Mungu ndani yako kile unachokifikiria kinakuwa sawa sawa na vile unavyofikiria maana umebeba nia ya Mungu ndani yako.

Kicholeta shida ni kwasababu umetenda dhambi. Ukimkosea Mungu omba msamaha mara moja hata kwa siku mara 100 ili utembee na nia ya Mungu uwe na mamlaka juu ya mambo yote yanayoinuka mbele yako.

Ukibeba nia ya Mungu ndani yako ukikemea Mungu amekemea, ukionya Mungu ameonya, ukigusa Mungu amegusa. Usiseme tumuachie Bwana maaana Bwana alishakuachia wewe.

UKIWA NA NIA YA MUNGU NDANI YAKO WEWE NI MTU HATARI
Yesu anasema “ninyi mpo ndani yangu, na yeye yupo ndani ya Baba” kwa maneno haya sisi tupo ndani ya YESU.
Sisi ni Roho na tumetoka Mbinguni mwili ulitoka kwa baba na mama Mungu akaweka Roho Ndani yake. Asili yetu ni Mbinguni. Tunatakiwa kusema maana tukisema inakuwa, tunatakiwa tuseme maneno, ni wakati wa kutenda kazi duniani. Sisi sio mwili huu, bali ni wanadamu ni Roho zinazokaa ndani ya mwili, tunafanana na Mungu na tukisema jambo linakua vilevile.

Sisi tuna mamlaka, tukisema tumesema na kila kiumbe duniani kina masikio, Yesu aliuambia mtu kuanzia leo ukauke na ikafika kesho asubuhi ukakutwa umekauka sababu mti una masikio lakini unasikia maneno ya mtu wa mbinguni.

Kila kiumbe kina masikio ya kusikia sauti ya mtu wa Mungu ukisema nacho kinasikia na kinatii lile ulilosema, mtu wa Mungu unauwezo wa kutengeneza mambo kwa kuzungumza kwa kinywa chako, unaweza kuzungumza na laana ya familia ikuacha ufanikiwe kwa jina la Yesu.

Unaweza kuzungumza na wachawi waliotawala ukoo wako, unaweza kuzungumza na mizimu ya familia ikuachie ukafanikiwe vaa nia ya Mungu kwenye moyo wako,vaa mawazo ya Mungu, tenda kama Mungu maana wewe ni Mungu katika nchi ukikaa kimya ukamwachia Mungu utabaki mwombaji bila mafanikio lakini ukisimama ukaumba kesho yako kwa mamlaka uliyonayo kwa jina la Yesu na kushughulikia wanaosimama mbele yako kukuzuia utafanikiwa na Mungu atatenda sawasawa na neno lako, ukisema nawapiga wanapigwa, ukisema nawafunga wanafungwa kwa jina la Yesu, ukisema hapana Mungu anasema hapana, unatakiwa useme kwa mamlaka ya jina la Yesu, usiseme namwachia Mungu maana hawajui watendalo, wale wanaokuonea wanajua watendalo sio jambo zuri lakini wanakutendea sabu wanajua utawasamehe, lakini leo badilika kaa sehemu tumia mamlaka yako kwa jina la Yesu shughulikia wale wanaokusumbua kwa jina la Yesu na watakoma kukuonea maana wewe ni Mungu katika nchi

Mungu hataki useme baba Mungu ponya, Mungu anataka utamke wewe na inakuwa maana Mungu anatenda kazi kupitia wewe.
Kwenye mabo ya Rohoni Mtu, anaweza kuokoka leo na akakushinda unabaki vile vile, mpaka utakapochukua hatua na uanze kusema, kama ni jambo ambalo hulitaki kwenye maisha yako sema jambo hili silitaki kwangu, litaondoka lakini usiposema litabaki vile vile a kukusumbua.
Wagalatia 2:20

KWENYE MAMLAKA HAPA DUNIANI.
Kuna Mungu
Kuna malaika watakatifu
Kuna sisi tuliokoka
Kuna wachawi na waganga
Kuna mashetani na majini

Sisi tuna mamlaka juu ya wakala wa giza wote waliotoka kuzimu na nia mbaya juu ya kanisa, tukiwashughulikia wale wanapotea kabisa lakini tukiwaacha itafika wakati watatufuta kabisa kwenye nchi.

Yohana 1:12
Mtoto wa Mungu ni Mungu katika dunia, ukiwa mtaani ni Mungu, ukitenda ni Mungu ametenda. Kuna falme mbili hapa duniani, Ufalme wa Mungu na Ufalme wa giza, ufalme wa giza kazi yake ni kuiba, kuchinja na kuharibu na ukizubaa unachinjwa mbele ya watu na kupotea.
Kuna watu wanapanga mipango ya uovu juu yako hujawahi tu kusikia jinsi wanavyokupangia, washambulie kabla hawajaja kukukabili kwa jina la Yesu. Unaweza kuwa una uvimbe mahali, unatakiwa uambie uvimbe ng’oka kwa jina la Yesu mimi ndio Mungu naishi Mwili huu nao utapotea kabisa.
Nataka uelewe jambo moja kuwa wewe ni Mungu katika uso wa nchi, ukisema inakua, ukiamuru inakuwa,
Iwe ni kansa au magonjwa ya moyo yang’oe

“kwa jina la Yesu, ukisema hivyo inakua, masikini wa familia ninautafuna, mimi ni Mungu katika familia yetu, ninang’oa kwa jina la Yesu. Kila wachawi wa ukoo wachawi wa familia ninawang’oa katika jina la Yesu, popote mlipoandaa mpango mbaya juu yangu ninawafuata maana mimi ni silaha ya Bwana iliyokubalika kwa wakati huu ninawafyeka kwa jina la Yesu Amen.
Watu wengi hawajui kuwa unakuwaje na Mungu

Zaburi 82:6 "Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia. Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu."
kule kutenda dhabi kule ndio kufa kama mwanadamu lakini ukiomba msamaha hapohapo unabakia mungu hapa duniani ukiwakilisha Ufalme wa Mbinguni, kukosea kwako hakukuondelei uhalali wa kuwa mtawala hapa duniani kwa niaba ya Mungu, ukitubu na kuacha dhambi mamlaka yako inabaki vilevile.
Wewe umezaliwa na Mungu, tena Mungu yuko ndani yako na wewe ndani yake, ongea na hali uliyonayo utaona mabadiliko lakini sipoonge hakibadiliki kitu. Huu ni wakati wa kutenda kwa mamlaka.

Mtu anaweza akajiuliza, Je na mimi nina uweza?
Unapofanya maamuzi tu ya kumpokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mokozi wa maisha yako tayari ndani yako una uweza wa kusema lolote kwa jina la Yesu likawa.

Kwa jina la Yesu, ninaumba Amani, ninaumba mafanikio kwenye maisha yangu, kwa jina la Yesu ninatafuna kila alienifunga, kwa jina la Yesu ninafungua akili yangu, ninafungua mikono yangu, kwa sababu mimi ni Muumbaji pamoja na Mungu. Ninafungua macho na moyo wangu kwa jina la Yesu Amen.

Zaburi 82:6
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
11,849
2,000
Mange kaua
 

Attachments

  • IMG-20170312-WA0010.jpg
    File size
    55.9 KB
    Views
    73

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom