Kwa nini hivi karibuni mechi za Simba na Yanga zinafanana?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,131
7,901
Kuna jambo ambalo nilianza kulinotice msimu uliopita.

Nakumbuka kuna kipindi ambacho Simba akishinda 4, Yanga anashinda 4, Yanga wakifunga goli kama la Mudathir Yahya dhidi ya TP Mazembe, Simba wanakuja kufunga goli hilo hilo.

Kwa wale waliobahatika kuangalia mechi za kwanza za Simba vs Power Dynamos na ile ya Yanga vs El Mereikh zilizochezwa kwa wakati mmoja, kuna jambo la kushangaza ambalo nililishuhudia. Siyo tu matukio mengi yalikuwa yanatokea kwa wakati mmoja, lakini hata magoli yalikuwa yanafungwa ndani ya dakika 3 katika mechi zote mbili.

Kiasi fulani hii hali imejirudia mechi za wiki hii za Simba vs Al Ahly na Yanga vs Azam. Baada ya mechi ya Yanga vs Azam, nilijiambia Simba hawezi kufunga zaidi ya goli moja kule Misri na imekuwa hivyo. Hata lile la magoli kufungwa ndani ya dakika 2-3 katika mechi hizo nalo limejirudia.

Inafikirisha.
 
Hiyo kitaalamu huitwa "coincidence" ni bahati tu na hakuna utaratibu maalumu wa hayo matukio.

Ukiangalia pia mechi za ulaya kwa wakati mmoja utagundua, matukio kama free kick, magoli yanafungwa kwa nyakati za kufanana ( japo siyo mara zote)
 
Back
Top Bottom