'Kwa nini hatukuonana zamani'???

'Kwa nini hatukuonana zamani'???

SnowBall

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Posts
3,052
Reaction score
2,846
Wanabodi natumaini hamjambo.

Jana nilikutana na mtu mmoja hivi na katika mazungumzo yetu mwenzangu akawa kavutiwa na mazungumzo yangu...Tulizungumza sana na actually the talk was nice. Ila mwishoni wakati tunaagana kama mtu aliyekata tamaa akasema 'kwa nini sikukuona tangu mwanzo'???

sasa baadaye niko home ndo najiuliza ....hivi kuna wakati tunaregret kuwa na wale tulionao na kuwish tungekuwa na huyu au yule??...Hivi haijawahi kukutokea ukakutana na huyu na ukajilaumu kwa nini uliwahi kufanya maamuzi??...Na ikitokea ukawaza hivyo inakuwa ni tamaa tu au ndo ile a human is an insatiable creature???

Naomba kuwasilisha
 
hata mimi imeshanitokea na hata jana nimeulizwa swali hilo na mamii kwenye mahakama ya kitanda ila nilijibu ndio ila nilikwepa kukubali kuwa nilijuta kwa kumtamani mwingine. kwahiyo nikamwambia nilijutia kwa kujilaumu mwenyewe....politics u know?
 
hahhahaaaaa leo hii tukipiga kura utaona kila mtu ambaye ana ndoa (both sex) watajibu kuwa walikosea au wangetamani wawe na akina fulani na sio type ya mke/mume alienane!! Mambo ya vituko haya usisikie
 
Kumbe inatokea kwa wengi...
 
hahhahaaaaa leo hii tukipiga kura utaona kila mtu ambaye ana ndoa (both sex) watajibu kuwa walikosea au wangetamani wawe na akina fulani na sio type ya mke/mume alienane!! Mambo ya vituko haya usisikie

Sasa mpwa hii huwa ni kwa nini??
Kuchokana au??
p
 
Kama signature yangu below inavyosomeka, kwamba kila mtu kwa wakati wake hasa awapo katika tafakuri ya nafsi yake, hujiliwa na dhamira mbaya. Sio matakwa yako wala sio shetani but is nature! Ni matamanio tu ya kidunia, huwezi kuzuia ila tunaweza kuyapunguza tu. Mkeo ni mkeo na mumeo ni mumeo. Full stop Jifunze kuweza kumvumlia ulienae na kumrekebisha ikiwezekana na sio kwa nguvu wal akwa kukomoana. Usikubali kila kitu bali pia usipinge kila kitu. Kuwa muwazi wa kuomba msamaha na kumaanisha kuwa yamiesha, sio useme yameisha huku yapo bado moyoni, sio kila kosa au tofauti ndogo tu basi uiwekee kikao na kuanza kusutana, mengine yapotezeee, hajaweka maji bafuni basi isiwe shida, nenda chukua ndoo kachote weka bafuni oga na endelea na ratiba nyinge.

Mumeo kachelewa kurudi basi mpe pole akirudi, muulize kwa ustaarabu achana na jazba na kuhusianisha na mambo mengine yalipopita,
Pia kama ni kosa au ni tofauti ikijitokeza hakikisha huingizi na mambo yaliyopita, deal with the current issue alone. sio useme hio ndio tabia yako hata juzi uliofanya hivi na vile nikakkaaa kimya tu!!! Kwa kufanya hivi utakua wewe ni wa kutamani kila mtu

Mfano ni mimi mwenyewe Elli wa JF; mke wangu kwa taratibu zake za maisha na mihangaiko hulazimika wakati mwengine kufika nyumbani saa tatu hadi tatu na nusu, huwa siulizi alikotoka na hata kama nikiuliza nauliza tu kumkumbusha asichelewe sana kwa ajili ya watoto. Imani yangu ni kwamba hata kama ana michezo yake anaifanya kwa kumzuia awahi kurudi nyumbani haimaniishi nimemzuia asifanye.

Ni ngumu hata kuizoea but kikubwa ni kumuomba MUNGU tu
Sasa mpwa hii huwa ni kwa nini??
Kuchokana au??
p
 
Wanabodi natumaini hamjambo.

Jana nilikutana na mtu mmoja hivi na katika mazungumzo yetu mwenzangu akawa kavutiwa na mazungumzo yangu...Tulizungumza sana na actually the talk was nice. Ila mwishoni wakati tunaagana kama mtu aliyekata tamaa akasema 'kwa nini sikukuona tangu mwanzo'???

sasa baadaye niko home ndo najiuliza ....hivi kuna wakati tunaregret kuwa na wale tulionao na kuwish tungekuwa na huyu au yule??...Hivi haijawahi kukutokea ukakutana na huyu na ukajilaumu kwa nini uliwahi kufanya maamuzi??...Na ikitokea ukawaza hivyo inakuwa ni tamaa tu au ndo ile a human is an insatiable creature???

Naomba kuwasilisha

leo nimekutana na binti kweny daladala,,,seem nice and kind kupitia maongezi yake,(na mrembo ofcoz),tatizo kumwomba namba,majitu yote yanakodoa macho....daah,sasa najuta ni bora ningeenda mpaka anaposhuka....
 
ulikuwa unaimba au ulikuwa unaimbishwa?? nadhani hukufika mbali. Hahaha
 
leo nimekutana na binti kweny daladala,,,seem nice and kind kupitia maongezi yake,(na mrembo ofcoz),tatizo kumwomba namba,majitu yote yanakodoa macho....daah,sasa najuta ni bora ningeenda mpaka anaposhuka....

Unaomba mngekutana juzi....ha ha ha
 
Na wewe unatamani tungeonana zamani...
Kiukweli kuna wakati unatamani mshale wa saa hurudi nyuma....

nilikuwa mahali wiki iliyopita nilikuwa na vijana 5 tulikuwa tunazungumzia mahusiano wote walitamani mshale wa saa ungerudi nyuma nikawauliza sababu nini mmoja akanijibu "hakujua upendo unakuwa kila mara na unavyozidi kukua ndivyo unavyosema laiti ingekuwa....... SnowBall tungeonana zamani lol hapo kaukweli kapo
 
Last edited by a moderator:

Umeonaeeh...
Yaani niliposikia anasema vile nikajiuza maswali mengi..
Lakini kumbe yanawakuta wengi
 
Back
Top Bottom