Kwa nini hakuna biashara ya silaha za nuclear duniani kati ya nchi?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
63,563
Reaction score
107,457
Kwa nini nchi zinazotengeneza silaha za nyuklia hawauzi hizo silaha kwa nchi nyingine kama wanavyouza silaha nyingine zote?
 
Wanaweza uziana kisiri ila wazi wazi ni ngumu kutokana na mikataba kama SALT, Nuclear Proliferation treaties na kadhalika ambayo sio tu inataka Nuclear itumike kwa nishati na sio kutengeneza mabomu bali pia inataka nchi ipunguze silaha za Nuclear ili kuepusha maangamizi kwa dunia.

However nchi kama China huko nyuma iliwapa teknolojia Pakistan ya kutengeneza bomu na hata Cuba iliwahi taka kupewa Nuclear warheads na urusi kama ikivamiwa na marekani ila ikaleta mgogoro mkubwa but naamini trade ya silaha hizo inafanyika kwa kisiri sana.
 
Hizo jumuiya za kimataifa za nyuklia ni uhuni mtupu, Ni agents WA ukoloni mamboleo, Wakubwa wanazuia wengine wawe nazo, wakati wao wanazo na wanaendelea kua nazo.
 
Nakumbuka umoja wa mataifa walibariki USA, EU na NATO kutuma vikosi kumwangamiza SADAM Kwa kile walichosema amekiuka makubaliano ya kimataifa khs uzalishaji WA silaha za nuclear na nyinginezo za maangamizi ya dunia.

Walidai anazo nuclear warheads zaid ya 200 na nyingine anazidi kutengeneza

Na anaemlalamikia kua SADAM anazo 200, yeye USA alikua nazo Zaid ya 1000.

Ila mpka SADAM ananyongwa kitanzi, Hadi Leo, hizo silaha hazijawai kuoneshwa kokote
 
Hizo jumuiya za kimataifa za nyuklia ni uhuni mtupu, Ni agents WA ukoloni mamboleo, Wakubwa wanazuia wengine wawe nazo, wakati wao wanazo na wanaendelea kua nazo.
Wamejaa unafiki tu wao kumiliki ni halali ila wengine ndio inageuka haramu
 
Hizo jumuiya za kimataifa za nyuklia ni uhuni mtupu, Ni agents WA ukoloni mamboleo, Wakubwa wanazuia wengine wawe nazo, wakati wao wanazo na wanaendelea kua nazo.
Si hilo tu, bali vile vile kutumia umiliki wa silaha hizo ku-blackmail mataifa mengine yanayo onekana hayaungi mkono siasa zao za "divide and rule!!"
 
Taifa kama marekani anajikuta yeye ndiyo headmaster wa dunia anataka mambo yaende kama anavyotaka hofu inakuja apo akiona kuna wapinzani wake wanakuja kwa kasi
 
Back
Top Bottom