Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,236
Sore ni mistake.nisharekebisha.we ZD mbona unatuchanganya hapo? una maana wanaume waliookoka ndio wengi au? mbona sijakuelewa? fafanua plz
Sore ni mistake.nisharekebisha.we ZD mbona unatuchanganya hapo? una maana wanaume waliookoka ndio wengi au? mbona sijakuelewa? fafanua plz
Ok! Kwa hiyo unategemea kulea "watoto haramu?" (ie watoto wa nje ya ndoa? Au kama wanavyodai kitanda hakizai haramu?)
Na vipi kuhusu fact kwamba kuzaa nje ya ndoa ni dhambi kwa Mungu? Au unafikiri maisha yataishia hapa duniani tu?
Ni dhana ya kikatili kabisa kudhania kuwa mtoto anaweza kuwa haramu. Binadamu atakuwaje haramu? Ni watu wasio na moyo ndio wanaweza hata kujaribu kufikiria hivyo. Hakuna binadamu aliye haramu. Halafu kwanza ni nani anayempa mtu mwingine mamlaka ya kuamua nani haramu na nani asiye haramu? Ujinga mtupu.
Ukishaanza kum invoke mungu kunakuwa hakuna mambo ya "fact" tena. Mambo ya dhambi ni mambo ya mtazamo tu. Iweje kuzaa mtoto iwe dhambi? Labda ungeniambia kuzaa na kutelekeza mtoto ni dhambi basi hapo tungekubaliana. Lakini kuzaa mtoto iwe nje au ndani ya ndoa ni baraka kwa mtazamo wangu ili mradi unatimiza wajibu wako kama mzazi.
Kuolewa ni Mpango wa Mungu,kwa ninavojua mimi.
Mimi nina experience na akina dada wa aina 2.
1. Wanaoishi maisha ya wokovu( waliookoka)
Kule kanisani kwa uchunguzi wangu mdogo ni kuwa Wanawake ni wengi kuliko wanaume.Na kuna mafundisho kule kuwa ni lazima uolewe na aliyeokoka,kama hajaokoka sio mpango wa Mungu.Na no matter what ni lazima usubiri mpaka muujiza utokee.Ukienda nje ya kanisa kwa maana ya siyeokoka basi ni dhambi na unaweza hata kutengwa.Vilevile wadada hawa waliookoka wakati mwingine wanaweza kukutana na wasiookoka na wakapenda na wakaamua kukubaliana lakini inakuja tatizo kuwa wanaume wasiookoka wanataka mpaka "watest" kabla ya ndoa,jambo ambalo ni dhambi kubwa kwa wadada hawa na wanajikuta wakishindwana.
2.Wanaoishi maisha ya kawaida( i mean church wanaenda lakini hawafuatilii sana mambo hayo)
Mara nyingi wana uhuru mkubwa wa kujichagulia wanayemtaka.Na hii imepelekea kuweka material things mbele na wakijikuta wakichagua sana wakati muda unaenda.
Lakini pia sababu nyingine ukweli bado upo palepale kutokana na takwimu,kuwa wanaume ni wachache kuliko wanawake.Hivyo wanawake wengi ni lazima wabaki bila kuolewa.No way out kwa vile sheria za kanisa zinataka mme 1 na mke 1.
Ni hayo tu kwa leo na ni mtizamo wangu tu.
Asanteni.
jamani yaani hii mada imegonga penyewe kabisa..mie mwenyewe mwenzenu nilikoma kwa kuchagua kwanza nilianza na mwanaume aweje ,sifa nikawa nazo kwa hiyo kila aliyekuwa akija kwangu namcheki kwanza kama yuko vile ninavyotaka kama akiwa sivyo ndo basi tena miaka ikaenda weeeeeeeeeee miaka ikarudi..
harafu sometimez wadada huwa tunadanganyana sijui kama tunakuwa tumeingia katika true love eti ooh namtaka mwanamme ambaye hata nikumuonyesha kwa mashostito wangu anakubalika ..hata nikitembea naye popote sijutiii wakati mwingine unakuwa usichana unatudanganya
lakini ikifika wakati na mwenyezi mungu kama ameweka yes wakwako yupo anatokea na anaweza kuwa hana sifa hata moja unayoitaka na huyo ndio anakuwa mmeo
Umesema mengi lakini hujamalizia stori... kwani bado hujapata... nina mdogo wangu ambaye atakufaa kama bado.... soulbrother2 anasubiria kuwa na firstlady1 wa kwake
Ni kweli kabisa WOS kumpata mke kwa sisi vijana limekuwa jaribu kubwa kuliko majaribu mengine. Unaweza pata pesa ya kutosha lakini ukakosa mke anayefaa.
Mfano baadhi ya vijana wengi wanataka wanawake wenye elimu ya chini ili waweze kuheshuimiwa lakini ikumbukwe kuwa wanafanya hivi kwasaabu wameona baadhi ya dugu au rafiki zao walivyofanyiwa na wake zao wenye elimu ya kutosha.
Ila kutafuta mke mwenye elimu ndogo kwa mtazamo waangu bado halijawa suluhisho la kudumu kwani wake hao hao wamekuwa wa kwanza kutoka nje ya ndoa zao, kutokuwaheshimu waume zao na mambo yanayofanana na hayo. Imefikia hata wakati wanaume baadhi wanasema kuwa wanawake wazuri sana ni headache na ndio hapo ninaporudi kwenye point ya msingi ya mtoa mada (Buchanan).
The way forward
Ni kubadlisha kwanza tabia kwa wanawake na wanaume
Pili Mitizamo ya wanaume dhidi ya wanawake
Tatu ni kuheshimiana na kutathimiana kwa wapenzi wake na waume
Kuolewa ni Mpango wa Mungu,kwa ninavojua mimi.
Mimi nina experience na akina dada wa aina 2.
1. Wanaoishi maisha ya wokovu( waliookoka)
Kule kanisani kwa uchunguzi wangu mdogo ni kuwa Wanawake ni wengi kuliko wanaume.Na kuna mafundisho kule kuwa ni lazima uolewe na aliyeokoka,kama hajaokoka sio mpango wa Mungu.Na no matter what ni lazima usubiri mpaka muujiza utokee.Ukienda nje ya kanisa kwa maana ya siyeokoka basi ni dhambi na unaweza hata kutengwa.Vilevile wadada hawa waliookoka wakati mwingine wanaweza kukutana na wasiookoka na wakapenda na wakaamua kukubaliana lakini inakuja tatizo kuwa wanaume wasiookoka wanataka mpaka "watest" kabla ya ndoa,jambo ambalo ni dhambi kubwa kwa wadada hawa na wanajikuta wakishindwana.
lakini ikifika wakati na mwenyezi mungu kama ameweka yes wakwako yupo anatokea na anaweza kuwa hana sifa hata moja unayoitaka na huyo ndio anakuwa mmeo
What if kama msichana akifanikiwa kumshawishi mchumba wake naye aokoke je watapokelewa kanisani na ndoa itafungwa?
Wokovu unaopatikana kupitia mchumba ni mbaya sana, hata kama ndoa itafungwa! Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, hayo yote (wachumba, etc) mtazidishiwa! Msigeuze maneno na kusomeka: Tafuteni kwanza wake/waume na hayo yote (ufalme wa Mungu) mtazidishiwa!
Mada ni nzuri.Asante kwa wote mliochangia na alioanzisha hii mada.
Mtazamo wangu mimi ni kwa wote wanawake kwa wanaume ni kwamba huwezi kumpata mtu ambaye atakuwa na sifa zote unazozitaka. Hilo haliwezekani kamwe labda umuumbe wako!
Kwahiyo katika maisha yako kama umekutana na mtu ambaye ana walau sifa 2 au tatu kati ya 5 unazozitaka na umri na vigezo vingine vinakuruhusu basi huyo ndiye wako.Mapungufu mengine mnaweza kurekebishana au kuvumiliana wakati maisha yanaendelea.
Just my 2 cents!
Kuna baadhi ya wasichana wanakimbiliwa na wanaume kuolewa, lakini wengine hata wakijirahisha namna gani wanaume wanawachezea kimapenzi na kuwaacha! Tatizo lao wanaoachwa ni nini hasa? Naomba tuchangie ili tuwasaidie hawa dada zetu jamani! Mimi kwa kuanza: 1. Naona baadhi ya Wasichana wako "too selective!" Wanatafuta wenye nazo (vijisenti) zaidi ambao kwa bahati mbaya "huwa wanaoa asubuhi na kuacha jioni!"
Bora mara mia Msichana akubali kuolewa na mwanaume akiwa hajaokoka ,na akae akijua wazi yupo na mtu wa aina gani,kuliko kutumia ushawishi wa aina yoyote "kumuokoa" au yeye mwanaume "ajilazimishe" kuokoka,it will be a disaster.What if kama msichana akifanikiwa kumshawishi mchumba wake naye aokoke je watapokelewa kanisani na ndoa itafungwa?
bora mara mia msichana akubali kuolewa na mwanaume akiwa hajaokoka ,na akae akijua wazi yupo na mtu wa aina gani,kuliko kutumia ushawishi wa aina yoyote "kumuokoa" au yeye mwanaume "ajilazimishe" kuokoka,it will be a disaster.
Nb; kuhusu swali lako,inategemea na dhehebu,mengine hawakupokei ng'oo,wengine watakuchunguza,na wengine utapokelewa chapchap hasa kama una vijisenti.