Kwa Nini Baadhi ya Wasichana Wanapata Waume Wa Kuwaoa Haraka Lakini...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Nini Baadhi ya Wasichana Wanapata Waume Wa Kuwaoa Haraka Lakini...?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Buchanan, Jan 16, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jan 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kuna baadhi ya wasichana wanakimbiliwa na wanaume kuolewa, lakini wengine hata wakijirahisha namna gani wanaume wanawachezea kimapenzi na kuwaacha! Tatizo lao wanaoachwa ni nini hasa? Naomba tuchangie ili tuwasaidie hawa dada zetu jamani! Mimi kwa kuanza: 1. Naona baadhi ya Wasichana wako "too selective!" Wanatafuta wenye nazo (vijisenti) zaidi ambao kwa bahati mbaya "huwa wanaoa asubuhi na kuacha jioni!"
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jan 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naona bado hakuna wachangiaji!
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkono mtupu haulambwi.
  Unajua wadada wametofautiana sana na wanaume nao wametofautiana sasa kwendana kitabia ndipo inapo kuwa ngumu kumpata mtu ambae mnaweza mkamechi ndo maana wengi wanaishia kumegwa na kuachwa. Na mwanamke wa kuolewa anajulikana.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..ngoja FL1, Pretty,MwanajamiOne,Nyamayao, binti Maringo waje najua wanaweza kuwa makungwi wazuri wale. Lakini kwa mtazamo wangu baadhi ya hawa wadada ambao ni wazuri lakini bado wanakosa kuolewa ni kutokana na vitabia vya kuwa na ndoto za may be kupata mume wa class ya juu ambaye huenda kwenye mazungumzo na marafiki zake huwa wanasimuliana. Kwa mfano nakumbuka jamaa yangu mmoja ana mdogo wake wa kike binti kwa muonekano wa nje ni mzuri sana, ana shule nzuri na mwaka jana tu amepata kazi yenye malipo mazuri na trip za nje nyingi. Tukiwa kwenye mazungumzo kwa kuwa tumezoeana akaniuliza kama utani kuwa nimtafutie mchumba naye anahitaji kuolewa, nikamuuliza yule jamaa yako wa tuliyekuwa tukikuona naye vipi? akadai jamaa alishaoa two years ago. Nilishangaa kidogo, lakini binti akaniambia kuwa kwa kuwa umri wake anaona umeenda kidogo na haoni dalili ya kuolewa anafikiria kutafuta at least mtu wa kuzaa nae tu hata kama ni mume wa mtu. Lakini nilichogundua kwa huyo binti ni katabia alikokuwa nako huko nyuma kuwa atapenda apate mume mwenye angalau nyumba mikocheni, awe na gari nzuri, kwa maelezo yake angalau akaunti yenye salio la 5ml na ingekuwa vizuri zaidi kama atakuwa Dr wa tiba, Lawyer au dereva wa ndege (pilot). Mawazo yao si mabaya lakini nadhani uhakika wa kupata watu wanaolingana mitazamo yao ni majaliwa zaidi. na hata wale waliobahatika kuwapata hao hizo ndoa zao hazikufika mbali maana mtu akiyumba kidogo kiuchumi binti anatafuta mbadala. So uchaguzi wao ndio hupelekea kuishia kumegwa tu na hakuna kuolewa.
   
 5. P

  Pangan Member

  #5
  Jan 16, 2010
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna sababu nyingi, lakini nitazitaja chache kwa kuanzia:
  1. Kutojua kum handle mwanaume wa aina ile

  2. Sura nzuri mara nyingi huleta kiburi katika ndoa

  3.Wengine wavivu kitandani

  4. Wengine hawatosheki, hivyo hulazimika kwenda nje ya ndoa

  5. Vitu laini muhimu unapopumzika , unaweza kuona sura safi lakini maini hayafai

  6.Kupika, na maandalizi mengine muhimu kwa mume wengine hawajui
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  wengi wanaangalia yalipo majani mabichi, halafu mfumo wao wengi wa maisha ni kuwa wanataka bwana awe na mali tayari na sio mtafute wote. wengi wao sio wakweli, wanataka maisha ya juu sana tofauti na walivyo.lakini pia wanaume wengi wanaangalia mwanamke mwenye mawazo chanya, wengi wao hawana.
  ndio maana wengi wanaishia kuwa mikwasu kwasu,vinyanambo,mademu, wasimbe, ngege nk nk nk. hawaolewi na wanaishia kuwa manung'a yembe!!!
   
 7. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ilo suala nimultidisciplinary mkuu,

  siku hizi sababu kubwa a ndoa za haraka ni mimba zinazopelekea shinikizo la mwanmke na ikiwa mwanume anataka watoto kwa wakti huo. hivyo utaona, kazi ubwa ya kushinikiza ni ya mwanmke, vunginevyo mimba inatolewa.

  kwa iyo kama unataka mtoto, unaoa ndipo kinaeleweka. kwa wananwake wajanja ni rahisi kumsoma mwanaume na kujua kumtegea mtego wa mimba ili kufanikisha malengo yake hasa kama ana pesa au msomi mzuri au anatoka mara mojamoja ng'ambo au anaishi hukohuko.

  nk.

  hii ni mojawap tu, sababu mni nyingi
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Buchanan hii mada ina mashiko sana ila wakishazungumza wao nafikiri na sisi ndio tutapata cha kuongea.
  Karibu Mlimba Mkuu upate japo mpunga
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  uko mlimba mkuu, gunia moja la mpunga tsh ngapi?
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ni bahati kupata Mke/Mume anayefaa.
  Kwa kifupi na kwa maelezo rahisi naweza kusema kwamba wanaume wana advantage ya kuchagua wa kumuoa, mwanamke anasubiri kufuatwa na mwanaume ambaye anaona anamfaa kumuoa.Subira hiyo inaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu.Wasichana wengine ni kweli wanachagua sana hadi umri unapitiliza na kufanya ushindani kuwa mkali zaidi katika " soko la wachumba".Wengine wanafikiria kujipanga vema kabla ya kuolewa - elimu au kiuchumi na wakati mwingine malengo haya huja kuwa kikwazo katika kupata mchumba mzuri!
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Jan 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ni kweli wakitoa mawazo wahusika italeta changamoto nzuri badala ya kuwasemea. Mimi nimechokoza tu, na nawasikitikia sana wasichana wenye sura nzuri kwa kuwa wao ndio victims namba moja! Huko Mlimba nilishawahi kufika miaka ya 2005/2006, sijui nitafika lini tena! Nashukuru hata hivyo kwa mwaliko wako, ubarikiwe!
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Jan 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nashukuru WOS kwa mawazo yako mazuri. Unawashauri nini akina dada, maana msichana akishapita umri wa miaka 30 kuolewa linaanza kuwa jaribu?
   
 13. L

  Lori Member

  #13
  Jan 16, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si vizuri kwa mwanamke kukubali kirahisi kuolewa, ni muhimu sana kumjua anaoa ni nani.. Sasa basi, kile kipindi cha kutaka kujua nani anaeoa, ndio mwanamme hukumbia.. Mara nyingi wanawake waliokimbilia kuolewa haraka wamepatwa na matatizo tofauti, unakuta mwanamme anaekuoa kumbe alishaoa mara 2 au 3 nyuma, au ni jambazi la kutumia silaha nk. Lkn si wote wanaokutwa na matatizo hayo. wengine huwa ni kiburi tu! KUTINGISHA kibiriti kama kweli unapendwa na ndio unakuwa mwanzo wa kuachwa.
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Jan 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kuwahi bila kuchambua masuala muhimu si vizuri na vipi habari ya kuchelewa, esp ukipita miaka 30? Si kuna akina dada wanafika mahali wanadai "wanataka kuolewa ili angalau kutoa nuksi?" They become desperate kiasi kwamba "they're ready for anything!" Isn't that also bad? And what's the best solution?
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa WOS kumpata mke kwa sisi vijana limekuwa jaribu kubwa kuliko majaribu mengine. Unaweza pata pesa ya kutosha lakini ukakosa mke anayefaa.
  Mfano baadhi ya vijana wengi wanataka wanawake wenye elimu ya chini ili waweze kuheshuimiwa lakini ikumbukwe kuwa wanafanya hivi kwasaabu wameona baadhi ya dugu au rafiki zao walivyofanyiwa na wake zao wenye elimu ya kutosha.
  Ila kutafuta mke mwenye elimu ndogo kwa mtazamo waangu bado halijawa suluhisho la kudumu kwani wake hao hao wamekuwa wa kwanza kutoka nje ya ndoa zao, kutokuwaheshimu waume zao na mambo yanayofanana na hayo. Imefikia hata wakati wanaume baadhi wanasema kuwa wanawake wazuri sana ni headache na ndio hapo ninaporudi kwenye point ya msingi ya mtoa mada (Buchanan).
  The way forward
  Ni kubadlisha kwanza tabia kwa wanawake na wanaume
  Pili Mitizamo ya wanaume dhidi ya wanawake
  Tatu ni kuheshimiana na kutathimiana kwa wapenzi wake na waume
   
 16. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #16
  Jan 16, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Narudia tena kusema mada yako ni nzuri sana na inaweza kuwa msaada kwa wanawake na wanaume ambao hawajao wala kuolewa
  Pili Mlimba sasa hivi ni mjini wacha kabisa. Wakati unatoka Ifakara kwenda uko kupita maeneo ya Mbingu, Lukolongo, Mngeta, Udagaji, huwezi amini kuwa unaenda sehemu ambayo iko populated mazingira mazuri kwa kilimo na biashara na pia wanapata umeme wa kutoka Kihansi. Its a nice place kwakweli. Karibuni nyote
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Jan 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nimefurahia sana usemaji wako Buchanan!

  Msichana yeyote amekamata mwenyewe funguo za kuolewa na kutoolewa.

  Hawa wanaojirahisi sana mitaani wana'face wakati mgumu maana wanaume wakishawalamba wanatangaziana kwamba fulani ni dada poa, wanaenda mbali zaidi kwa kusema hata jiografia ya mwili wake, na perfomance yake wakati wa kunanihino, na hata uzuri/ubaya wa mashine yake(japo siamini sana katika ubaya/uzuri wa hiyo inayoitwa mashine).

  Msichana akiwa na heshima na habebwibebwi hovyo, uwezekano wa kuolewa ni mkubwa, maana sifa zake pia zinavuma.

  Ningekuwa msichana mie nabania ile mambo kishenzi...huh!
   
 18. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #18
  Jan 16, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huyu Mkuu ametulia sana kwenye maandiko yake!!! Is among the people ninaowakubali kwakweli. For instance hii mada yake ni mada ambayo kwa undani ni muhimu sana ila ikichukuliwa light itapoteza lengo!!!
  Big up Buchanan and PJ too!! You are always in my heart Men
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Jan 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nashukuru kwa comment ndugu Sipo. Ningependa sana kusikia toka kwa akina dada tuangalie namna ya kuwasaidia! I am sure they can get something useful and they will surely enjoy their marriages, whenever they get into in!
   
 20. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #20
  Jan 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni kweli wanawake wanapenda sana wanaume ambao ni tayari wana Pesa na maendeleo ,na hilo ndo linawakwamisha sana kuolewa.
  Ukiangali wanawake ni wengi kuliko wanaume na wanaume ndo hao MAKONDA,WASUKUMA MIKOKOTENI,WAVUBUA VYOO,WAKATA MANYASI .....sasa imekuwa ngumu kwa wao kupata hao wanaume wa kuwaoa.
   
Loading...