Kwa mwendo anaokwenda nao Rais Magufuli, upinzani unakufa kifo kitakatifu.

Wapinzani gani mnaowagawa watanzania kwa kueneza chuki, ukabila ukanda na udini.Mmekuwa mkidanganya watu kuwa eti Moshi na arusha zinabaguliwa eti hakuna viongozi wa juu, huku mkisahau kuwa mbegu ile ingekuja kuwaangamiza. Tuliwaonya kwa kuishambulia kanda ya ziwa na wasukuma mlijua mnajiimalisha. Sasa angalia kanda ya ziwa Ndiyo inaongoza kuikimbia chademaktk kipindi cha wiki mbili. Tulisema tulisema na tutasema kwamba mmechagua wenyewe sehemu kisu kinatakiwa kuchinja.Watanzania hawataki kusikia ubaguzi hawajafika huko. Mnasema miradi mikubwa intends kanda ya ziwa. Nenda Arusha ukaone shughuli inayoendelea ya kuwaletea wananchi mradi mikubwa ya maji kupitia benki ya dunia. Angalia barabara iliyokamilika ya kutoka Tengeru hadi Sakina na bado mkandarasi huyo huyo kapewa mkataba mpya chapu chapu .Barabara inaanzia Maji chai kupitia Njiro hadi .........HAlafu watu wanashinda kwenye keyboard kuponda. Lake zone mmewatesa sana kwa miporojo yenu, Protas Masha Kitilya TOROKENI MJE.Mtachoshwa na wachonganishi wasio itakia mema nchi
Mi nadhani uliowataji wala hawatoroki.
Hao wanarudi nyumbani.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, kufuatia hii hama hama ya wapinzani kuhamia CCM, Jee rais Magufuli Anaimarisha CCM kwa kujenga CCM imara, Au Anaua Upinzani na kulifanya taifa tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?.

Naendelea kutafakari hii hama hama ya wanachama wa upinzani kuhamia CCM, jee hama hama hii ni kwa sababu rais Magufuli anajenga CCM imara, au CCM ni ile ile, kinachofanyika ni Magufuli kuua upinzani, kwa viongozi wa upinzani kumkubali sana Magufuli, hadi kuamua kuachana na vyama vyao na kujiunga na CCM, kumfuata Magufuli, ili wamsaidie kutimiza azma yake kuiletea Tanzania maendeleo?, ama ni kweli kuna fedha zinatembea kuwanunua viongozi wa upinzani wenye njaa, hivyo kulielekeza taifa letu kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja kwa mlango wa nyuma?.

Wasalaam.

Paskali

Mkulu mimi nadhani wengi wetu hatuelewi maana ya kuwa na vyama upinzani vya kisiasa. Unasikia mtu anasema amehama chama kwa sababu kiongozi fulani amefanya vizuri.

Leo nilikuwa nasikia bbc world service wakiwahoji wa zimbwabwe walioko Harare,South AFrica na London.....kuna dada mmoja ameongea vizuri sana alisema tatizo la vijana wengi Africa hawana msimamo na mpaka hapo waafrica tutakapo acha tabia ya kuwakubali viongozi wawe miungu watu hapo ndio tutaweza kujitawala kwa maendeleo
 
tuwachambue hawa wanaoenda ccm wanaenda kujenga au wana agenda zao za vyeo ,na kupunguza makali ya njaa .tukishawachambua mmoja mmoja utaona kama kweli wana enda kuijenga ccm au kubomoa upinzani .tuanze PASKALI
 
I think it's worth mentioning that the most committed members of a political party are the reason for the political party's resilience and ultimate success. Unfortunately, our political parties probably have way too few committed members. As a result, most of these parties cannot survive without subsidy from the government and/or financial support from a handful of its members, most of whom also happen to be the party founders. This acute dependence on highly concentrated financial support causes such political parties to be treated and run like family businesses. ...That's why politicians such as Maalim, Mzee Mapesa, etc. have been at the helm for as long as their political parties have existed. They literally are more important than their parties.

A respectable number of members should care deeply enough to provide whatever support their party needs to achieve its objectives. The sheer breadth and depth of members' investedness should elicit an appropriate level of accountability from all office bearers. ...In the developed world, political parties receive not a single penny from their governments, but they're much better than our political parties!
 
Upinzani ni mawazo/ideology sio watu . Hauwezi kuumaliza mawazo kinzani.. nakuhakikishia hata mbowe akihama leo chadema itaendelea kuwepo na upinzani utazidi kuishi..
 
Hata siku Mbowe akaacha chadema akarudi ccm utasema hivyo hivyo kuwa na yeye mwanzo alikuwa ccm hana impact yoyote.

Hakuna mpinzani ambaye hajawahi kuwa CCM as of now, so wote ni wale wale. Wapinzani wote ni wanachama wa ccm wa zamani, ifike mahali chadema ikiri kwa sasa hali yao sio nzuri, hawana sera, hawana agenda na wajipange kuliko kuwakashifu kila anayetoka mkisahau kila mtu anao uhuru wa kujiunga na kuhama chama muda wowote anaotaka akiamua bila hata kutoa sababu.

Majuzi tu mlikuwa mnamsifia Masha wakati wa uchaguzi EA, leo mnamtukana. Ndio maana chama hakiwezo kuwa na member wanaojitambua maana wengi ni watukanaji na wakashifu watu tu
Masha kweli ni mjinga tena mchumia tumbo kabisaaaa.
Anapohama kurudi ccm, na kusema "nimeona upinzani hauna nia ya kushika dola" tafsiri yake ni kwamba; alitegemea labda upinzani mwaka 2015 ungeshika dola na kisha wampe/wamrudishie cheo chake. Sasa hari ni tofauti kabisa ambapo hakuna hata cheo chochote alichopewa ndani ya CDM, kwa hiyo solution yake ni kurudi alikotoka ambako anaona Kuna uafadhali wa kupata/kurudishiwa vyeo vyake, simply kwa kuwa CCM kimeshika dola.
Mapambano ya dhati huwa hayahitaji tamaa ya vyeo, fedha n.k......
Lakini vile vile masha kaona biashara zake haziendi vyema akiwa upinzani, so ni kurudi tu CCM.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, kufuatia hii hama hama ya wapinzani kuhamia CCM, Jee rais Magufuli Anaimarisha CCM kwa kujenga CCM imara, Au Anaua Upinzani na kulifanya taifa tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?.

Naendelea kutafakari hii hama hama ya wanachama wa upinzani kuhamia CCM, jee hama hama hii ni kwa sababu rais Magufuli anajenga CCM imara, au CCM ni ile ile, kinachofanyika ni Magufuli kuua upinzani, kwa viongozi wa upinzani kumkubali sana Magufuli, hadi kuamua kuachana na vyama vyao na kujiunga na CCM, kumfuata Magufuli, ili wamsaidie kutimiza azma yake kuiletea Tanzania maendeleo?, ama ni kweli kuna fedha zinatembea kuwanunua viongozi wa upinzani wenye njaa, hivyo kulielekeza taifa letu kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja kwa mlango wa nyuma?.

  1. Jee CCM imara, ina maana gani kwa mustakabali wa upinzani Tanzania?.
  2. Jee kuna uukweli kuwa rais Magufuli hana nia njema na upinzani Tanzania, ndio maana alisema kamwe hatateua wapinzani kwenye serekali yake?.
  3. Uteuzi wa Mama Anna na Prof. Kitila, ni uteuzi wa hongo ili kuisambaratisha ACT, na sasa kazi kuisambaratisha Chadema, ndio imeanza?.
  4. Jee ni kweli Viongozi wa upinzani wanaohamia Chadema, wamenunuliwa?.
  5. Jee katazo la rais Magufuli kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa ya kitaifa, inawezekana halina nia njema na upinzani?.
  6. Jee ni kweli rais Magufuli, anaendelea kutumia rasilimali za taifa kuitangaza CCM katika mikutano ya kiserikali, au ya kichama inayofanyikia kwenye venue za serikali, hivyo kugharimiwa kwa fedha za umma?.
  7. Kama katiba ya nchi, rais Magufuli aliyoapa kuilinda, inaruhusu mikutano ya kisiasa, lile katazo lake kuzuia mikutano hiyo, lina maana gani kwa mustakabali wa upinzani Tanzania.
  8. What does Mhe. rais Magufuli stand to loose kama ataruhusu shughuli za kisiasa nchini kuendeshwa kwa mujibu wa katiba?. Yaani anapata nini kuzuia mikutano?.
  9. Kwa watu wenye uwezo wa kosoma nia njema iliyoko ndani ya moyo wa mtu kupitia facial expressions mtu anapozungumza, jee kuna nia jema kuhusu upinzani nchi Tanzania katika awamu hii?.
  10. Kwa vile upinzani nchini Tanzania, upo kwa mujibu wa katiba, jee mtu yoyote mwenye nia ya kuudhoofisha upinzani nchini Tanzania, ana nia njema kweli na taifa hili?. Inawezekana kwa mtu kuwa na nia njema na maendeleo ya taifa, at the same time, ukafifisha demokrasia kwa kudhoofisha upinzani?.
My Take.
Kazi ya upinzani Zaidi ya kutaka kwenda ikulu, pia kuisimamia serikali kule bungeni kupitia mawaziri mbadala, kusimamia matumizi ya fedha za umma kupitia oversight committee, ili kujihakikishia serikali inasimamiwa ipasavyo, Tanzania tunahitaji kuwa na upinzani imara, kama juhudi za rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, uzembe, ubadhirifu na ufisadi, matokeo yake ni kuua upinzani, kwa wapinzani kukosa hoja za kuendelea kuwa wapinzani, hivyo kuamua kujiunga na CCM kumsaidia Magufuli, jee ni nini mustakabali wa Tanzania yenye upinzani hafifu?.

Jee Tumeanza safari ya kuelekea nchi ya chama kimoja cha siasa?, na uchaguzi wa rais 2020, utakuwa ni uchaguzi wa rais kweli au litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini rais wa Tanzania hadi 2025, ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli?. If this is case for 2020, kwa umasikini wetu nchini Tanzania, do we real need to spend so much kufanya igizo hili?. Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

Wasalaam.

Paskali
JPM hajawahi kuchukia ufisadi wakati yeye in sehemu ya ufisadi. Anachukia kuona watu wanafaidika kama alivyosema mwenyewe kuwa anapenda kuona tukiishi kama mashetani

Kifupi ni mtu mwenye roho mbaya sana, mbinafsi na mpenda sifa kupindukia.

jiulize angekuwa anachukia rushwa vipi anatumia pesa ya uma kununua wapinzani. kuhonga wabunge wapitishe hoja zake na kutumia pesa za uma kinyume na taratibu zilizowekwa kikatiba?
 
kuzuia matamanio ya binadamu binadamu ni ngumu sana,kwa mawazo yake ataona kama anaua upinzani kumbe ndio unazidi na kuimarika na wapinzani sio mpaka watoke nje ya chama wengine anao humo hmo ndani ya chama chake.hitaji la watu kwa sasa ni ccm kutoka madarakani sio kingine na wale msioamini subirini 2o2o hali ya uchaguzi itakua ngumu sana kwa ccm kuliko hata wanavyodhani,
 
Huu si wakati wa kumjadili magufuli wala ccm,ingependa kama ungejadiliwa upinzani,lakini kwa mahaba yalivyowazidi mnawajadili ccm kana kwamba ccm wanajali upinzani ukifa
CCM ndiye baba, bahati mbaya wamekuwa wabinafsi, wasiopenda wenzao washiriki siasa kama wao wanavuoshiriki. Ingawa kwa sasa wanajiona wanafaidika na hali hiyo lkn wanaweka rehani mustakabali wa nchi yetu kwa kuwabana wenzao wakati wao wanafanya siasa kama kawaida.

Kama unadhani kuna mambo mema wanafanya (mimi naamini yapo) lkn hili la kuzuia sauti za wapinzani wao ambao kmsingi, kimaadili na kisheria wanapaswa kuwa huru kufanya siasa (kama wafanyavyo CCM ) wenye hekima hawawezi kulinyamazia. Kuminya uhuru wa watu wenye mawazo kinzani ni hatari sana, Gaddafi aliwafanyia mema watu wake lkn kwa kudhibiti uhuru wa watu wake ilikukuwa alikuwa anawafungulia mango adui zake, kuwakamata, kuwatesa, kuwatisha na kuwatia kizuizini wapinzani wake kulitosha kugeuza mazuri yake yote kuwa ubatili.

Vv
 
Hata siku Mbowe akaacha chadema akarudi ccm utasema hivyo hivyo kuwa na yeye mwanzo alikuwa ccm hana impact yoyote.

Hakuna mpinzani ambaye hajawahi kuwa CCM as of now, so wote ni wale wale. Wapinzani wote ni wanachama wa ccm wa zamani, ifike mahali chadema ikiri kwa sasa hali yao sio nzuri, hawana sera, hawana agenda na wajipange kuliko kuwakashifu kila anayetoka mkisahau kila mtu anao uhuru wa kujiunga na kuhama chama muda wowote anaotaka akiamua bila hata kutoa sababu.

Majuzi tu mlikuwa mnamsifia Masha wakati wa uchaguzi EA, leo mnamtukana. Ndio maana chama hakiwezo kuwa na member wanaojitambua maana wengi ni watukanaji na wakashifu watu tu
Sawa CCM
 
upinzani unapotea. na upinzan unajikaanga wenyew kw yule samaki waliyemuweka kweny tenga Edo, Si unajua Samaki m1 akioza. CCM walipoona Samaki yule kaoza wakamtupa, wapinzan wakamuokota hapi ndio matatzo yakaongezeka CHADEMA.
 
Hiyo ndio kazi tuliyomtuma ikulu? , tulimtuma kazi nyingine yeye anafanya kazi nyingine
 
Back
Top Bottom