upinzani unajiua wenyewe kwa kudakia mambo yasio ya msingi kipindi cha kikwete sio kweli kuwa upinzani ulifanya vizuri bali perfomance ya serikali ya JK kutokuwa sirias hasa kwenye swala la rushwa .na ndo kilichofsnya ccm ichokwe kila konaWanabodi,
Hili ni bandiko la swali, kufuatia hii hama hama ya wapinzani kuhamia CCM, Jee rais Magufuli Anaimarisha CCM kwa kujenga CCM imara, Au Anaua Upinzani na kulifanya taifa tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?.
Naendelea kutafakari hii hama hama ya wanachama wa upinzani kuhamia CCM, jee hama hama hii ni kwa sababu rais Magufuli anajenga CCM imara, au CCM ni ile ile, kinachofanyika ni Magufuli kuua upinzani, kwa viongozi wa upinzani kumkubali sana Magufuli, hadi kuamua kuachana na vyama vyao na kujiunga na CCM, kumfuata Magufuli, ili wamsaidie kutimiza azma yake kuiletea Tanzania maendeleo?, ama ni kweli kuna fedha zinatembea kuwanunua viongozi wa upinzani wenye njaa, hivyo kulielekeza taifa letu kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja kwa mlango wa nyuma?.
My Take.
- Jee CCM imara, ina maana gani kwa mustakabali wa upinzani Tanzania?.
- Jee kuna uukweli kuwa rais Magufuli hana nia njema na upinzani Tanzania, ndio maana alisema kamwe hatateua wapinzani kwenye serekali yake?.
- Uteuzi wa Mama Anna na Prof. Kitila, ni uteuzi wa hongo ili kuisambaratisha ACT, na sasa kazi kuisambaratisha Chadema, ndio imeanza?.
- Jee ni kweli Viongozi wa upinzani wanaohamia Chadema, wamenunuliwa?.
- Jee katazo la rais Magufuli kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa ya kitaifa, inawezekana halina nia njema na upinzani?.
- Jee ni kweli rais Magufuli, anaendelea kutumia rasilimali za taifa kuitangaza CCM katika mikutano ya kiserikali, au ya kichama inayofanyikia kwenye venue za serikali, hivyo kugharimiwa kwa fedha za umma?.
- Kama katiba ya nchi, rais Magufuli aliyoapa kuilinda, inaruhusu mikutano ya kisiasa, lile katazo lake kuzuia mikutano hiyo, lina maana gani kwa mustakabali wa upinzani Tanzania.
- What does Mhe. rais Magufuli stand to loose kama ataruhusu shughuli za kisiasa nchini kuendeshwa kwa mujibu wa katiba?. Yaani anapata nini kuzuia mikutano?.
- Kwa watu wenye uwezo wa kosoma nia njema iliyoko ndani ya moyo wa mtu kupitia facial expressions mtu anapozungumza, jee kuna nia jema kuhusu upinzani nchi Tanzania katika awamu hii?.
- Kwa vile upinzani nchini Tanzania, upo kwa mujibu wa katiba, jee mtu yoyote mwenye nia ya kuudhoofisha upinzani nchini Tanzania, ana nia njema kweli na taifa hili?. Inawezekana kwa mtu kuwa na nia njema na maendeleo ya taifa, at the same time, ukafifisha demokrasia kwa kudhoofisha upinzani?.
Kazi ya upinzani Zaidi ya kutaka kwenda ikulu, pia kuisimamia serikali kule bungeni kupitia mawaziri mbadala, kusimamia matumizi ya fedha za umma kupitia oversight committee, ili kujihakikishia serikali inasimamiwa ipasavyo, Tanzania tunahitaji kuwa na upinzani imara, kama juhudi za rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, uzembe, ubadhirifu na ufisadi, matokeo yake ni kuua upinzani, kwa wapinzani kukosa hoja za kuendelea kuwa wapinzani, hivyo kuamua kujiunga na CCM kumsaidia Magufuli, jee ni nini mustakabali wa Tanzania yenye upinzani hafifu?.
Jee Tumeanza safari ya kuelekea nchi ya chama kimoja cha siasa?, na uchaguzi wa rais 2020, utakuwa ni uchaguzi wa rais kweli au litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini rais wa Tanzania hadi 2025, ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli?. If this is case for 2020, kwa umasikini wetu nchini Tanzania, do we real need to spend so much kufanya igizo hili?. Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...
Wasalaam.
Paskali
pascal ndugu yangu ccm watatawala muda mrefu sana , hakuna chama chenye nguvu kuwatoa ccm
wapinzani awana msimamo wanaingia na kutoka kama wanaingia chooni
Risasi zipi mkuu?Kama hayo yote uliyosema ni kweli risasi za nin?
Ninakubaliana na wewe! Huwezi kuimarisha chama kwa kununua watu kwa pesa na ahadi za vyeo. Watu wakununua hawawezi kujenga chama imara wala nchi. Na hii ni aina mbaya kabisa ya rushwa! Wanaonunua wapinzani na wale wanaonunuliwa hawana maadili yoyote....both are crooked....hawawezi kujenga mifumo...wanajijenga wenyewe...kwa masilahi yao..siyo ya nchi!Haimarishi CCM na wala haui upinzani. Kifupi. Asilimia kubwa kama si wote wanaoenda CCM, ama wanashawishiwa kwa ahadi ya au pesa ama vyeo, na pengine kutaka kuhurumiwa katika shughuli afanyazo mtu. Sasa CCM haiwezi kujengwa kwa kuwapa asante wanaohamia huku kuna wanachama wengi ambao kwa muda mrefu wametumika chamani kwa bidii na uaminifu na bila kudai au kupewa malipo. Kuhusu upinzani hauwezi kuuawa kwa kuwarubuni wanachama ambao kwa kweli si kuwa wanarubunika kwa sera za CCM, bali kwa aina fulani ya rushwa, ambayo kwa maoni yao inawasaidia kutatua shida zao za kimaisha, ikiwamo njaa. Kwa wale wanaohamia upinzani, huwa hakuna ahadi ya kupewa chochote. Na hata kama ahadi itakuwepo, ni ile ya kupiga kazi bila malipo, ambayo kwa kweli ni wale tu wenye msimamo na maamuzi binafsi ndiyo wanao weza kuhamia upinzani. Kwa maoni yangu mimi, CCM lazima tu itakufa, kwa sababu zifatazo. Kwanza CCM haina sera. Ndiyo maana kila mwana CCM hawezi ongea kitu bila kumtaja Magufuli. Kwa hiyo CCM haina sera kwa sasa. Sera ni Magufuli. Pili Magufuli alishasema CCM kuna majizi hivyo hategamei CCM. Ndiyo maana hata wakati wa kampeni alijinadi kama Magufuli, na ndiyo maana hakuwa anatumia nembo ya chama, alikuwa na nembo yake "M" yenye mwenge katikati. Pia siku hizi ni nadra sana kusikia serikali ya CCM, si kwenye chama wa serikalini, wote wanasema serikali John Pombe Magufuli. Hivyo kwa maoni yangu, tofauti ya CCM na CHADEMA ni kuwa CCM ni Magufuli na CHDEMA ni Taasisi yenye sera ambayo ni wale tu wenye imani na sera ndiyo wanajiunga. Na kwa kuwa CHADEMA ni Taasisi, haiwezi kufa kamwe, japo kweli inaweza kuyumba, lakini ikaimarika zaidi.
kwani wanaoibia taifa ni upinzani?viongozi ndio wezi, china hakuna kulindana kama hapa kiongozi mwizi,lzm hatua zichukuliwe ndiyo maana wanaenda ingawa wezi wapo lkn wanashughurikiwa, ingekuwa china huyo nani visenti na wenzie wangeshakula kamba siku nyingi tu.Bora chama ki moja on China anavyoipeleka Mbio dunia kiuchumi, lakini watu kila siku wanailaumu haifuati utawala bora wa kuwatetea wezi wa Mali za umma.