Kwa mwendo anaokwenda nao Rais Magufuli, upinzani unakufa kifo kitakatifu.

Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
10,277
18,363
Wakuu kama mnaangalia namna game inavyochezwa mtagundua mbinu anayotumia mhe. Rais ni ile tunaita mchawi mpe mwanao amlee.

Rais alianza na Prof. Kitila, baada ya muda Zitto (mb) akasema rais ameamua kufanya kazi na watu wote, tukumbuke huyu Prof. Kitila alikua mkosoaji wa serikali kabla ya kupata nafasi ya kuingia kwenye system, sasa kaingia kimyaaa.

Leo rais amemteua Mama Anna Mghwira kua RC Kilimanjaro.

Amini usiamini Zitto atapongeza na kimsingi rais kawafanya wapinzani wakose hoja aisee.

Rais kama atasoma huu uzi naomba amteue mhe. Lissu ili tujue rangi yake halisi maana analawama na vitisho sana.
Mhe. Rais nakuomba umteue Lissu ndo tutajua kama ni akili ya njaa au ni mzalendo.

Naishia hapa kwa leo ila upinzani unakufa bila kelele.
Rais Magufuli ni genius amini msiamini.

Naona wadau wananikejeli mnadhani mimi ni mchumia tumbo, mimi sio CCM wala Chadema hivyo vyama mnavyo nyinyi, mimi nimetoa maoni kama mtanzania tu.
Mnisamehe ila ndo ninachoona mimi
 
lisu anakunyima usingizi
pambana na maisha acha kupambana na lisu.

jk kikwete
kulipo lisu aingie bungeni bora dr slaa awe raisi.

lisu ni mfupa ulioshindikana na fisi wewe panya utauweza??????
 
Wakuu kama mnaangalia namna game inavyochezwa mtagundua mbinu anayotumia mhe. Rais ni ile tunaita mchawi mpe mwanao amlee.

Rais alianza na Prof. Kitila, baada ya muda Zitto (mb) akasema rais ameamua kufanya kazi na watu wote, tukumbuke huyu Prof. Kitila alikua mkosoaji wa serikali kabla ya kupata nafasi ya kuingia kwenye system, sasa kaingia kimyaaa.

Leo rais amemteua Mama Anna Mgwira kua RC Kilimanjaro.

Amini usiamini Zitto atapongeza na kimsingi rais kawafanya wapinzani wakose hoja aisee.

Rais kama atasoma huu uzi naomba amteue mhe. Lissu ili tujue rangi yake halisi maana analawama na vitisho sana.
Mhe. Rais nakuomba umteue Lissu ndo tutajua kama ni akili ya njaa au ni mzalendo.

Naishia hapa kwa leo ila upinzani unakufa bila kelele.
Rais Magufuli ni genius amini msiamini
Unapomtaja Mkumbo na Mgwila naomba uangalie uwezo wao kwa mapana si kama Tundu; sisi tunaomjua hatuwezi kupendekeza hilo mkuu.
Bora kumpa mchawi kuliko hili TUNDU Mkuu; kwani unadhani yeye JPM hana akili kiasi hicho?
Kumbe hujui kama TUNDU ni mpiga deal sawa sawa na Chenge alah...!
 
lisu anakunyima usingizi
pambana na maisha acha kupambana na lisu.

jk kikwete
kulipo lisu aingie bungeni bora dr slaa awe raisi.

lisu ni mfupa ulioshindikana na fisi wewe panya utauweza??????
Huu ni mtazamo sipambani na mwanasiasa yeyote, haya ni mawazo yangu tu.
Usichefukwe roho mkuu
 
Wakuu kama mnaangalia namna game inavyochezwa mtagundua mbinu anayotumia mhe. Rais ni ile tunaita mchawi mpe mwanao amlee.

Rais alianza na Prof. Kitila, baada ya muda Zitto (mb) akasema rais ameamua kufanya kazi na watu wote, tukumbuke huyu Prof. Kitila alikua mkosoaji wa serikali kabla ya kupata nafasi ya kuingia kwenye system, sasa kaingia kimyaaa.

Leo rais amemteua Mama Anna Mgwira kua RC Kilimanjaro.

Amini usiamini Zitto atapongeza na kimsingi rais kawafanya wapinzani wakose hoja aisee.

Rais kama atasoma huu uzi naomba amteue mhe. Lissu ili tujue rangi yake halisi maana analawama na vitisho sana.
Mhe. Rais nakuomba umteue Lissu ndo tutajua kama ni akili ya njaa au ni mzalendo.

Naishia hapa kwa leo ila upinzani unakufa bila kelele.
Rais Magufuli ni genius amini msiamini
Kwa akili yako ACT nao ni wapinzani wa CCM? AU akili yako ndiyo kama ya Lusinde?
 
Wakuu kama mnaangalia namna game inavyochezwa mtagundua mbinu anayotumia mhe. Rais ni ile tunaita mchawi mpe mwanao amlee.

Rais alianza na Prof. Kitila, baada ya muda Zitto (mb) akasema rais ameamua kufanya kazi na watu wote, tukumbuke huyu Prof. Kitila alikua mkosoaji wa serikali kabla ya kupata nafasi ya kuingia kwenye system, sasa kaingia kimyaaa.

Leo rais amemteua Mama Anna Mgwira kua RC Kilimanjaro.

Amini usiamini Zitto atapongeza na kimsingi rais kawafanya wapinzani wakose hoja aisee.

Rais kama atasoma huu uzi naomba amteue mhe. Lissu ili tujue rangi yake halisi maana analawama na vitisho sana.
Mhe. Rais nakuomba umteue Lissu ndo tutajua kama ni akili ya njaa au ni mzalendo.

Naishia hapa kwa leo ila upinzani unakufa bila kelele.
Rais Magufuli ni genius amini msiamini

Nadhani wewe ndio utakayekufa!
Kadri ulimwengu uishivyo ideas pinzani hazitakaa ziishe!
 
Teh teh teh! Umenena vyema mkuu. Mkulu ampe wadhifa Lissu tumuone rangi yake halisi.
Hawezii kuumwa huo ugonjwa hata dakika moja amteue hawezi ninnina uhakika pombe anacheki wanyonge japo wanakuwa na majina ya upinzani

Sharif hamad
Tundu
Mdee
Mbilinyi
Hawezi kabisa
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, kufuatia hii hama hama ya wapinzani kuhamia CCM, Jee rais Magufuli Anaimarisha CCM kwa kujenga CCM imara, Au Anaua Upinzani na kulifanya taifa tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?.

Naendelea kutafakari hii hama hama ya wanachama wa upinzani kuhamia CCM, jee hama hama hii ni kwa sababu rais Magufuli anajenga CCM imara, au CCM ni ile ile, kinachofanyika ni Magufuli kuua upinzani, kwa viongozi wa upinzani kumkubali sana Magufuli, hadi kuamua kuachana na vyama vyao na kujiunga na CCM, kumfuata Magufuli, ili wamsaidie kutimiza azma yake kuiletea Tanzania maendeleo?, ama ni kweli kuna fedha zinatembea kuwanunua viongozi wa upinzani wenye njaa, hivyo kulielekeza taifa letu kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja kwa mlango wa nyuma?.

  1. Jee CCM imara, ina maana gani kwa mustakabali wa upinzani Tanzania?.
  2. Jee kuna uukweli kuwa rais Magufuli hana nia njema na upinzani Tanzania, ndio maana alisema kamwe hatateua wapinzani kwenye serekali yake?.
  3. Uteuzi wa Mama Anna na Prof. Kitila, ni uteuzi wa hongo ili kuisambaratisha ACT, na sasa kazi kuisambaratisha Chadema, ndio imeanza?.
  4. Jee ni kweli Viongozi wa upinzani wanaohamia Chadema, wamenunuliwa?.
  5. Jee katazo la rais Magufuli kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa ya kitaifa, inawezekana halina nia njema na upinzani?.
  6. Jee ni kweli rais Magufuli, anaendelea kutumia rasilimali za taifa kuitangaza CCM katika mikutano ya kiserikali, au ya kichama inayofanyikia kwenye venue za serikali, hivyo kugharimiwa kwa fedha za umma?.
  7. Kama katiba ya nchi, rais Magufuli aliyoapa kuilinda, inaruhusu mikutano ya kisiasa, lile katazo lake kuzuia mikutano hiyo, lina maana gani kwa mustakabali wa upinzani Tanzania.
  8. What does Mhe. rais Magufuli stand to loose kama ataruhusu shughuli za kisiasa nchini kuendeshwa kwa mujibu wa katiba?. Yaani anapata nini kuzuia mikutano?.
  9. Kwa watu wenye uwezo wa kosoma nia njema iliyoko ndani ya moyo wa mtu kupitia facial expressions mtu anapozungumza, jee kuna nia jema kuhusu upinzani nchi Tanzania katika awamu hii?.
  10. Kwa vile upinzani nchini Tanzania, upo kwa mujibu wa katiba, jee mtu yoyote mwenye nia ya kuudhoofisha upinzani nchini Tanzania, ana nia njema kweli na taifa hili?. Inawezekana kwa mtu kuwa na nia njema na maendeleo ya taifa, at the same time, ukafifisha demokrasia kwa kudhoofisha upinzani?.
My Take.
Kazi ya upinzani Zaidi ya kutaka kwenda ikulu, pia kuisimamia serikali kule bungeni kupitia mawaziri mbadala, kusimamia matumizi ya fedha za umma kupitia oversight committee, ili kujihakikishia serikali inasimamiwa ipasavyo, Tanzania tunahitaji kuwa na upinzani imara, kama juhudi za rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, uzembe, ubadhirifu na ufisadi, matokeo yake ni kuua upinzani, kwa wapinzani kukosa hoja za kuendelea kuwa wapinzani, hivyo kuamua kujiunga na CCM kumsaidia Magufuli, jee ni nini mustakabali wa Tanzania yenye upinzani hafifu?.

Jee Tumeanza safari ya kuelekea nchi ya chama kimoja cha siasa?, na uchaguzi wa rais 2020, utakuwa ni uchaguzi wa rais kweli au litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini rais wa Tanzania hadi 2025, ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli?. If this is case for 2020, kwa umasikini wetu nchini Tanzania, do we real need to spend so much kufanya igizo hili?. Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

Wasalaam.

Paskali
 
Back
Top Bottom