SUPERUSER
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 960
- 308
Kwanza unatakiwa kufahamu kitu kimoja hakuna mtaji uliokua mdogo. Kikubwa ni kusoma mazingira.
Angalia mazingira yanayokuzunguka angalia ni biashara gani hapo uliokuwepo hakuna ili uweze kuwafikishia watu kirahisi.
Hata kama ikiwepo soma udhaifu wa huo mfanya biashara na utumie advantage hio kufanikiwa.
Biashara zipo nyingi sana. Unaweza kuuza maji ya jumla na reja reja, mtaji huo unatosha. Hapo hapo ukaweka na vocha, mtjai wa laki moja unapata elfu 5, ni ndogo lkn mzunguko ukiwa mkubwa ni fresh, unaweza kuweka na sigara ukauza pia.
Unawez kufungua mgahawa, ukatafuta mama mmoja akawa anauza kahawa, chai, maandazi, bvitu km hivo. Hata msosi fresh, ina faida na mtaji mdogo.
Unaweza kununua memory card kkoo mfano ya 2gb kwa jumla hua inauzwa 3,500, ukinunua 2piece mia mtaji wake 350,000, nawe unauza hata 3lfu 6 au 5, faida buku jelo lkn ukimaliza zote hzo una laki na nusu. kuna size tofauti na bei tofauti. (Si shauri sana hii maana inataka uzoefu sn na ujanja).
Unaweza fungua kibanda ukaweka mtu awe anatengeneza matundu, plate 500 fresh inalipa sn.
Unaweza kununua mashine ya bisi laki 4 na nusu tu, ukaweka dogo akawa anauza, utapiga bao, hata madenti wako watanunua.
Unaweza kununua mashine ya juice ya mua bei simple tu hlf ukauza glass 500 fresh tu inalipa mzee.
Zipo nyingi, kikubwa ni kusoma mazingira mkuu.
Unaweza ukanunua hata boda boda akakuletea buku 10 kwa siku (tafuta mtu mwaminifu au itakula kwako), hapa miezi 6 tu umerudisha hela yako na una pikipiki yako.
All the Best.
Ukipata mtaji zaidi, rudi hapa tukushauri tena.
Hivi mashine za bisi zinapatikana wap kwa urahis mkuu