Kwa mtaji huu nitafanya biashara? Msaada

MENISON

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
726
Reaction score
623
Tatizo la ajira limekua gumu sana, nimemaliza shahada yangu mwaka jana ila wakati nasubiria nipate ajira nilianza kufundisha tuition na nina balance ya tsh 1.5 mil net ambayo ni nje ya matumizi yangu ya kila siku sasa swali langu ni je naweza kufanya biashara gani yoyote halali?

Hope kutakua na wazoefu humu nahitaji msaada wa mawazo
 
Endelea kufundisha tution tuu mkuuu,pata kaz ndo uache kaz
 
huu ushauri wa kufuga kuku na kulima nimechoka kuusikia, hivi hakunaga ideas zingine? mtoa mada angalia mazingira unayoishi unaweza pata wazo.
Hata mimi nimechoka kusikia hii idea ya kufuga kuku mtu asiombe ushauri utasikia fuga kuku utafikir tuna vichwa vya kuku hatuwaz outside the box . mtoa mada nakushauri mamb mawil 1 tafuta site au mwamvuli umwek mtu akufanyie tigopesa au mpesa inalipa kam uko sehem yenye watu
2 Nunua bodaboda umtafute mtu mwaminifu akuletee pesa kila siku mpk mwak unaisha utapata faida
 
asante kwa mawazo yako mkuuu
 
Mbona umekuja na idea zilezile za kila siku na wewe...waza 'outside the box' basi kuonesha mfano
 
huu ushauri wa kufuga kuku na kulima nimechoka kuusikia, hivi hakunaga ideas zingine? mtoa mada angalia mazingira unayoishi unaweza pata wazo.

Nimecheka mimi usiku huu hadi mwanangu ananishangaa! Mkuu Hus umechoka watu kila mara ni aidha wakalime au wakafuge! Hahahahahaha sasa si ndio level zetu mkuu! The options is our country are very limited kwa kweli na hasa kwa mitaji midogo kama ya ndugu yetu hapa.
 
Fanya recycling business ya makopo ya plastic ama takataka ama matairi,or kama unafundisha basi jitangaze zaidi na wapatie barua wanafunzi wako wawapelekee wazazi ukutane nao uwaambie nia ya kuanzisha shule ya awali etc etc etc
 
Hata mimi nimechoka kusikia hii idea ya kufuga kuku mtu asiombe ushauri utasikia fuga kuku utafikir tuna vichwa vya kuku hatuwaz outside the box . mtoa mada nakushauri mamb mawil 1 tafuta site au mwamvuli umwek mtu akufanyie tigopesa au mpesa inalipa kam uko sehem yenye watu
2 Nunua bodaboda umtafute mtu mwaminifu akuletee pesa kila siku mpk mwak unaisha utapata faida

Kabisa inalipa ni siyo mwaka miezi sita tu
 
Nenda Mkata kule Tanga kanunue vitanda kwa jumla wanauza kati ya Tsh 80,000 mpaka 100,000/:
peleka Arusha kitanda kimoja kinauzwa rejareja 180,000 hadi laki 2.
Au lete Dar
Itakulipa vitanda haviozi wala kuhitaji chakula kama vifaranga.
 
Tatizo la ajira limekua gumu sana ,nimemaliza shahada yangu mwaka jana ila wakati nasubiria nipate ajira nilianza kufundisha tuition na nina balance ya tsh 1.5 mil net ambayo ni nje ya matumizi yangu ya kila siku sasa swali langu ni je naweza kufanya biashara gani yoyote halali? hope kutakua na wazoefu humu nahitaji msaada wa mawazo

mambo vipi mkuu?

naomba nikushauri kwanza ufanye market research accordingly with your level of initial capital.

jaribu kuangalia fursa ambazo ziko katika eneo uliloko currently... usiache kazi yako uliyonayo, earn twice man!!

angalia usije ukaingia kwenye biashara kichwa kichwa kwa kufuata upepo, you are educated, utaanguka ukose pa kushika nakwambia..

machache tu ya kusema, financial books should be kept and recorde regularly. USIOGOPE MKUU!
 
Nimecheka mimi usiku huu hadi mwanangu ananishangaa! Mkuu Hus umechoka watu kila mara ni aidha wakalime au wakafuge! Hahahahahaha sasa si ndio level zetu mkuu! The options is our country are very limited kwa kweli na hasa kwa mitaji midogo kama ya ndugu yetu hapa.

hahahaha!! vimezidi kwakweli. nafikiri tuna uvivu wa kufikiri ndio maana ushauri tunaotoa haraka haraka ni kufuga kuku na kulima. opportunities zipo nyingi tu basi watu hawataki kuzitafuta.
 
Na hicho ndicho anachoulizia mwenzetu,kama unajua hizo opportunities zitaje hapa ili huyu mh. asipewe hayo maushauri ya kufuga na kulima. Kuna kipindi nami nilichukua ushauri wa ndg mmoja kwenye jukwaa la uchumi juu ya kilimo na mtaji wangu mdogo nikafanyia kazi utadhani nilikuwa nashauriwa mimi nikaenda ruvu kwenye mashamba ya serikali nikakodi na kulima mpunga na imenilipa na sasa naendelea tena.
Kwahiyo badala kuonesha kuchukia ushauri toa suluhisho mbadala dada yangu

Kwanza unatakiwa kufahamu kitu kimoja hakuna mtaji uliokua mdogo. Kikubwa ni kusoma mazingira.

Angalia mazingira yanayokuzunguka angalia ni biashara gani hapo uliokuwepo hakuna ili uweze kuwafikishia watu kirahisi.

Hata kama ikiwepo soma udhaifu wa huo mfanya biashara na utumie advantage hio kufanikiwa.

Biashara zipo nyingi sana. Unaweza kuuza maji ya jumla na reja reja, mtaji huo unatosha. Hapo hapo ukaweka na vocha, mtjai wa laki moja unapata elfu 5, ni ndogo lkn mzunguko ukiwa mkubwa ni fresh, unaweza kuweka na sigara ukauza pia.

Unawez kufungua mgahawa, ukatafuta mama mmoja akawa anauza kahawa, chai, maandazi, bvitu km hivo. Hata msosi fresh, ina faida na mtaji mdogo.

Unaweza kununua memory card kkoo mfano ya 2gb kwa jumla hua inauzwa 3,500, ukinunua 2piece mia mtaji wake 350,000, nawe unauza hata 3lfu 6 au 5, faida buku jelo lkn ukimaliza zote hzo una laki na nusu. kuna size tofauti na bei tofauti. (Si shauri sana hii maana inataka uzoefu sn na ujanja).

Unaweza fungua kibanda ukaweka mtu awe anatengeneza matundu, plate 500 fresh inalipa sn.

Unaweza kununua mashine ya bisi laki 4 na nusu tu, ukaweka dogo akawa anauza, utapiga bao, hata madenti wako watanunua.

Unaweza kununua mashine ya juice ya mua bei simple tu hlf ukauza glass 500 fresh tu inalipa mzee.

Zipo nyingi, kikubwa ni kusoma mazingira mkuu.

Unaweza ukanunua hata boda boda akakuletea buku 10 kwa siku (tafuta mtu mwaminifu au itakula kwako), hapa miezi 6 tu umerudisha hela yako na una pikipiki yako.

All the Best.

Ukipata mtaji zaidi, rudi hapa tukushauri tena.
 
Na hicho ndicho anachoulizia mwenzetu,kama unajua hizo opportunities zitaje hapa ili huyu mh. asipewe hayo maushauri ya kufuga na kulima. Kuna kipindi nami nilichukua ushauri wa ndg mmoja kwenye jukwaa la uchumi juu ya kilimo na mtaji wangu mdogo nikafanyia kazi utadhani nilikuwa nashauriwa mimi nikaenda ruvu kwenye mashamba ya serikali nikakodi na kulima mpunga na imenilipa na sasa naendelea tena.
Kwahiyo badala kuonesha kuchukia ushauri toa suluhisho mbadala dada yangu

kweli kama umeshindwa kutambua suluhisho nililotoa kwenye comment yangu ya kwanza utaweza kutambua fursa kweli wewe? hebu rudi uisome tena usipoona suluhisho uliza.
 
Back
Top Bottom