Kwa Mkeo ni hospitali, kwa hawara ni 'love nest'....

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
Mwanaume kuhamia kwa hawara wakati wa kutumbua maraha, ukiugua unajikongoja nyumbani kwa mkeo kuuguzwa.Kwani huyo hawara yako hajui kuchemsha supu?
Mwanaume kuja home kubadili mavazi na kuacha nguo chafu - kwani kwa mkeo ni kwa dobi/dry cleaner?
Yapo sana kwanini lakini?
 
wanaume wa zizazi cha .com!!

Unadhani ni dot.com tu shosti?
Miye hapa rafiki yake babu yangu alikumbwa na mkasa huu wa kubwagwa na hawara nje ya geti lake.
Kala pesa ya pensheni na hawara.Ilipoisha kauguaaa...hawara hana taimu kumuuguza!
 
Unadhani ni dot.com tu shosti?
Miye hapa rafiki yake babu yangu alikumbwa na mkasa huu wa kubwagwa na hawara nje ya eti lake.
Kala pesa ya pensheni na hawara.Ilipoisha kauguaaa...hawara hana taimu kumuuguza!

Patam hapo, na hawakomi wala kujifunza hawa watu...
Mtu ana mke na watoto anaenda malizia mshiko kwa awala, halafu anarudi kwa mkewe akiwa empty!
 
Unadhani ni dot.com tu shosti?Miye hapa rafiki yake babu yangu alikumbwa na mkasa huu wa kubwagwa na hawara nje ya eti lake.Kala pesa ya pensheni na hawara.Ilipoisha kauguaaa...hawara hana taimu kumuuguza!
mmh! wanawake tunamoyo,unamfungia mume wa mwenzio miezi as if ndondocha,unamchunaa ww! akibaki sifuri unamtimua arudi kwa mkewe akiwa mweupeeee!! muogopeni mungu na malaika wake wajameni!
 
mmh! wanawake tunamoyo,unamfungia mume wa mwenzio miezi as if ndondocha,unamchunaa ww! akibaki sifuri unamtimua arudi kwa mkewe akiwa mweupeeee!! muogopeni mungu na malaika wake wajameni!

Lakini kani hao wanaume hadi wafanywe ndondocha, ina maana hawana akili au?
 
Ngoja nitetee kwa hawara.......
Kwa hawara kazi ni moja tu ambayo haitajalisha ni muda gani umeenda
Kwa hawara kuna 'privacy' kama umeamua kwenda kupumzika, hakuna cha shangazi, shemeji, au vilio vya watoto, na hata simu unazima au wakikupigia unawaambia uko busy
Kwa hawara its all budhism, living for that particular moment, hawara hawezi kukusumbua sana kwa mijadala mikubwa ya kihistoria au mbele (future). Akiomba pesa kama unazo unampa, kama huna anakutoa baruti kishney
Kwa hawara kila kitu ni customized kwa ajili yako, na yako tu
 
Unadhani ni dot.com tu shosti?
Miye hapa rafiki yake babu yangu alikumbwa na mkasa huu wa kubwagwa na hawara nje ya geti lake.
Kala pesa ya pensheni na hawara.Ilipoisha kauguaaa...hawara hana taimu kumuuguza!

Tehe tehe tehe, unanikumbiusha jirani yetu aliepata pension akachukua tax kutoka Dar hadi TAnga (enzi hizo) akiwa na hawara yake.
Alikufa fukara wa kutupwa
 
mmh! wanawake tunamoyo,unamfungia mume wa mwenzio miezi as if ndondocha,unamchunaa ww! akibaki sifuri unamtimua arudi kwa mkewe akiwa mweupeeee!! muogopeni mungu na malaika wake wajameni!

Ka kweli sisi wanawake ni majasiri sana. Kitendo cha mume wa mwenzio kuhamia kwako kabisa, mnapika na kupakuwa na mtaa mzima unajua.

Kwa wanaume hilo jibu lake liko wazi kabisa, ukihamisha mke wa mtu basi wewe umeshajinunulia jeneza, no matter what!!!
 
Tehe tehe tehe, unanikumbiusha jirani yetu aliepata pension akachukua tax kutoka Dar hadi TAnga (enzi hizo) akiwa na hawara yake.
Alikufa fukara wa kutupwa

Hizi hadithi mbona zinafurahisha na kuchekesha!
Basi mwaya, kuna mwingine yeye alistaafu tena cheo kikubwa sana.Alikuwa na wake wawili tayari.
Bi mdogo yeye alikuwa anaishi naye kwenye jumba alilopangiwa na shirika.Bi mkubwa yeye akasema atakaa uswazi kwenye nyumba ya NHC. Baba yule alipostaafu akaenda kupanga nyumba kubwa tu mkewe na watoto na yeye wakahamia.Kama haikutosha, ile pensheni sijui aiiona kubwa sana, akaenda kumpangisha hawara.Punde akahama kwa mke wa pili na kwenda kuishi na hawara.Wakazaa na kuzaa!! Saa ngapi pesa hajakata! Alipoona maisha yamempiga changa, karudi kwa bi mdogo! ......
Hivi huwa wanashikwaga na nini hawa?
 
Nyumba kubwa m-boreshe huduma ili tusiende kwenye nyumba ndogo :A S embarassed: ...
Samahani sana ....
 
Back
Top Bottom