Kwa Mkeo ni hospitali, kwa hawara ni 'love nest'....

Ngoja nitetee kwa hawara.......
Kwa hawara kazi ni moja tu ambayo haitajalisha ni muda gani umeenda
Kwa hawara kuna 'privacy' kama umeamua kwenda kupumzika, hakuna cha shangazi, shemeji, au vilio vya watoto, na hata simu unazima au wakikupigia unawaambia uko busy
Kwa hawara its all budhism, living for that particular moment, hawara hawezi kukusumbua sana kwa mijadala mikubwa ya kihistoria au mbele (future). Akiomba pesa kama unazo unampa, kama huna anakutoa baruti kishney
Kwa hawara kila kitu ni customized kwa ajili yako, na yako tu

Nimeipenda hii tathmini...japo imepinda lol
 
Nyumba ndogo atakupikiaje supu wakati na yeye ana-mme wake?

Kwa hiyo mnachangia na huyo mume akijua?
Humo ndani mipangilio ikoje
kiasi utakapoumwa inabidi ujikokote
kurudi kuugulia kwa mkeo?Au nyumba ndogo mumewe naye anakua
kahamia nyumba ndogo? Ama kweli dunia duara!
Fafanua pls
 
Hawara wapo kutoa changamoto kwa nyumba kubwa ambayo mara nyingi huwa dorooo

ET,
Ishu siyo kwanini mtu una nyumba ndogo.
Ishu ni je, kama nyumba kubwa iko dorooo kwanini usimalizie haja zako zote huko?
 
Kwanza namwomba mungu aniepushie na mwanume wa hivi,
Km mwanaume atanifanyia hivi hakika atakuwa keshanichoka nitakachofanya nikumwomba aondoke mazima na asirudi tena,
Iwe shida au raha akakae huko huko tusileteane magonjwa ndani,akigoma nitaondoka mm na wanangu piriodi.
 
yaani, hii tabia ipo na imekithiri pia na si kwa wanaume wa sasa tu hata wa enzi. Vibabu ambavyo havitaki hata kupewa shikamoo... vimeng'ang'ana tu na vibinti. Yani hapa Jirani kuna mdingi wa hivyo yeye aliacha kabisa mke wake kijiji miaka kapanga chumba kimoja Dar, anapiga kazi (ni mtumishi wa umma) na very soon atastaafu. Sasa ni mgonjwa sana, mkewe ndo anahangaika na mzigo wake huo. Si msemei vibaya.. (Mungu anisamehe), ila inauma sana jamani. Yani wakati wa shibe si wa mke/familia ila wakati wa mateso ndo hadhi ya mke inaonekana.

Ushauri wangu kwa wale Wanaume wa mipango ya kando: Muwe mnawajali wake zenu jamani ili hata mambo yanavyokuwa mabaya muwe mna pakushika.
 
Kama kuna mwanamke aliyewahi onja adha hii, au kuona mwenzie yamemkuta, hebu mwageni mikakati ya kupambana na hawa madume-.Mi najipanga ili nikimpata wa ivo, nimfunze somo ambalo hatakaa alisoma kwenye kitabu chochote duniani!
 
Hizi hadithi mbona zinafurahisha na kuchekesha!
Basi mwaya, kuna mwingine yeye alistaafu tena cheo kikubwa sana.Alikuwa na wake wawili tayari.
Bi mdogo yeye alikuwa anaishi naye kwenye jumba alilopangiwa na shirika.Bi mkubwa yeye akasema atakaa uswazi kwenye nyumba ya NHC. Baba yule alipostaafu akaenda kupanga nyumba kubwa tu mkewe na watoto na yeye wakahamia.Kama haikutosha, ile pensheni sijui aiiona kubwa sana, akaenda kumpangisha hawara.Punde akahama kwa mke wa pili na kwenda kuishi na hawara.Wakazaa na kuzaa!! Saa ngapi pesa hajakata! Alipoona maisha yamempiga changa, karudi kwa bi mdogo! ......
Hivi huwa wanashikwaga na nini hawa?


wanashikwa na wanawake
 
kumbe kuwa na nyumba ndogo sio issue aisee i can't believe this coming from a woman if at all your Avar represents who u r
 
kumbe kuwa na nyumba ndogo sio issue aisee i can't believe this coming from a woman if at all your Avar represents who u r

Sijui kama umesoma mada aisee!!
Hapa hatujadili the right and wrong ya kuwa nyumba ndogo.Ishu ni nyingi ambayo ni:-
Mmeshatenda ovu kwa kuwa na nyumba ndogo.Kama hizo nyumba ni kiviiile, kwanini likikupata la kukupata unarudi nyumba kubwa?Ushanfahamu sasa?
Kweli ualimu kazi.!

 
Hizi hadithi mbona zinafurahisha na kuchekesha!
Basi mwaya, kuna mwingine yeye alistaafu tena cheo kikubwa sana.Alikuwa na wake wawili tayari.
Bi mdogo yeye alikuwa anaishi naye kwenye jumba alilopangiwa na shirika.Bi mkubwa yeye akasema atakaa uswazi kwenye nyumba ya NHC. Baba yule alipostaafu akaenda kupanga nyumba kubwa tu mkewe na watoto na yeye wakahamia.Kama haikutosha, ile pensheni sijui aiiona kubwa sana, akaenda kumpangisha hawara.Punde akahama kwa mke wa pili na kwenda kuishi na hawara.Wakazaa na kuzaa!! Saa ngapi pesa hajakata! Alipoona maisha yamempiga changa, karudi kwa bi mdogo! ......
Hivi huwa wanashikwaga na nini hawa?

na wenzako waliokuzidi maujanja...
 
kwa hawara kazi ni moja starehe...

matatizo , shida, maradhi na mazagazaga mengine kwa mke.

kwanza unafikiri akiumwa huko nyumba ndogo ataruhusiwa kulala? atatolewa spidi vibaya mno

ila wanaume wenyewe hawakomi wala hawaachi, sijui nani kawashikia akili:shock:
 
Ninge mkaribisha home na kumwambia zam yake kukaa nyumbani nami nimepata kijipesa naenda tumia sehem nikiishiwa ntarudi.
Na wabeba wanangu huyooo! Maana hapo kuna mengi na kaugonjwa anaweza kuletea[/QUOTE

Kama mna kajumba mlikojenga ukiondoka atauza hicho kijumba na kurudi kwa hawara. Afadhali uvumilie kwa ajili ya watoto
 
Kwani ni mtoto mdogo asokua na akili, alipokuja kwangu na kukubali kufungiwa hakujua kama ana mke wa ndoa tena ya church.....
Atajijuuuu... akija kama ana michuzi, ni kumchuna ikibidi ngozi, akichacha timuaaaa..!!!! hapendwi mtu...

mmh! wanawake tunamoyo,unamfungia mume wa mwenzio miezi as if ndondocha,unamchunaa ww! akibaki sifuri unamtimua arudi kwa mkewe akiwa mweupeeee!! muogopeni mungu na malaika wake wajameni!
 
nyumbani ni nyumbani tu.....hata niwe na wanawake mia mwisho wa siku lazima niirudi nyumbani
 
Back
Top Bottom