Kwa miaka 20 ya uongozi wa CHADEMA Manispaa ya Moshi imeshindwa kuwa Jiji, Jafo tuangalie kwa jicho la huruma!

Habari yafo mmeku?

Kumbe kwafo ni Usseri vaita?

Lakini usijali, hata wasipotangaza Moshi kuwa jiji, rais ajae ambae hatakuwa m baguzi na mkabila atatangaza tu.

Hivi nyie huwa mnakosa maneno ya kuongea!!! Moshi kweli liwe jiji!!!!

Sioni ajabu chadema kuongea haya maajabu šŸ˜
 
Tengeneza kwanza Manispaa ya Rombo
Waache wenye Moshi yao
Kwahiyo hamtaki tena theluji ya Mlima Kilimanjaro iwepo? Kila sehemu ikiwa Manispaa itakuwa hatari Jamani ndiyo maana hata nyumba imegawanyika vyumba vyote haviwezi kuwa Master lazima kuwe na store sturdy room choo Umeelewa?
 
Mie hizo mavitu zenu sijui huwa zinzsaidia nini Dar imekuwa jiji miaka yote lakini ndo chafu kuliko mikoa yote mvua ya jero Dar ina simama lini ukasikia moshi ina mafuriko.
 
Na kwa taarifa yako Chato inaenda kuwa Jiji kabla ya Moshi

Ila nashauri Moshi iendelee kuhifadhi ukijani kuulinda mlima unafaida zaidi ya hao watu ma majengo mnayotaka ya badilishe jina kuwa Jii
Unadhani nitashangaa ..kwa serikali hii hakuna cha ajabu...kama korona wanasema ni changamoto ya upumuaji au mafua ya kubana kama JPM anavyosema.
 
Kingereza unajua,Kiswahili unajua,nini tatizo sasa?

Kuna tatizo isipokua Jiji?

Watu wakizikiana na kutambika,nini tatizo?

Ni their native land,they can do what their ancestors did for 800years.

Hivi unadhani pahali pakiitwa JIJI ni kitu cha maana sana?

Linda mazingira wewe,acha ushabiki maandazi!

Ili kamji ka moshi kakuwe angalau kuifikia Morogoro ama Shinyanga wakazi wa mule wanapaswa wagawe viwanja kwa wageni na sio kuyang'ang'ania wao kama wao wachagga, end of the day wanashindwa kuviendeleza.
 
Mara nyingi huwa naiangalia Tanga na Mbeya halafu najiuliza kwanini Moshi haijawa Jiji hadi leo?

Najua kwamba Mwanza na Arusha zimeiacha mbali Moshi kimaendeleo na kipopulation lakini siyo Tanga ya Makamba na Mbeya Sugu.

Chadema imekuwa na mbunge na madiwani wengi Moshi kwa miaka 20 mfululizo lakini imefeli zaidi ya kuongoza kwa usafi tu, ngoja tumuone mbunge na madiwani wa CCM 2020/25.

Jaffo mtuangalie na sisi bwashee.

Johnthebaptist
Usseri Rombo

Maendeleo hayana vyama!
Hivi jiji hupewa mkoa?
Au manispaa??

NISAIDIENI

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu

Unafeli mno,wewe na wenzako wa CCM

Bongo zenu by design politicians wanatumia short term thinking framework.

Wanasiasa short term thinking ndio thinking yao by design,ndio shida ya wanasiasa

Moshi unatakiwa uwe mji mdogo by design utumie eneo dogo mno ku-exist.

Kwa African standards unazotumia wewe,mji kua jiji unatakiwa uwe ume-cover bigger land area na ujinga mwingine mwingi na idadi kubwa ya watu na upumbavu mwingine mwingi sana

Moshi upo chini ya mlima,unatakiwa usikue zaidi ya hapo ili kuokoa huo mlima

Moshi inatakiwa iwe na idadi ndogo ya watu,itumie eneo dogo sana isiwe na systems nyingi za kuharibu mazingira

Ukijaza watu Moshi,wataharibu ardhi wapate makazi,wata-cover eneo kubwa zaidi,watapanda milimani kukata miti wapate makazi mji upanuke

Ni most definitely watapanda milimani zaidi kuliko bondeni kufata hali ya hewa...eneo litakua packed mno na ule mlima ndani ya miaka 20-30 utakufa kabisa

By design na makusudi makubwa,Moshi watu wazuiwe wasijae,watu waende miji mingine,Moshi kua JIJI kwa African standards ni kuua Mlima ambao ni world's heritage

Pamoja na kampeni mbali mbali za kuotesha miti na awareness mbalimbali tangu nikiwa mdogo mpaka leo mid 2000's Moshi ilikua kwenye brink ya kua jangwa na snow cap was the lowest ni its history

Leonidas Gama aliokoa that time kwamba ukitaka kukata tawi la mti shambani kwako ni lazima ukachukue kibali ofisi ya kata na ukikata makusudi unafungwa....Walao leo kuna vimiti somehow

Ukiwa rais wewe takataka utaharibu nchi nzima kwa euphoria ya stupid cities which do no make any sense in a long run.
Mkuu,

Huwezi kuilinganisha Moshi na Mbeya kwa sababu zifuatazo

Moshi
1. Kijana wa Kilimanjaro akiondoka kwenda kutafuta maisha mikoani akifanikiwa huwekeza huko na mwisho wa mwaka anaenda Moshi kupumzika na kufanya matumizi ya kile alichokipata
2. Uwekezaji wa wenyeji wa Kilimanjaro ni wilaya za pembezoni kama Hai, Siha, Kibosho, Machame na Marangu ila mjini Moshi, Moshi vijijini na Rombo hakuna chochote cha maana;
3.Moshi mjini wamewekeza wahamiaji wa kutoka mikoa mingine
4.Machinga (biashara ndogo ndogo) Moshi mjini zinafanywa na akina mama
5. Wenyeji wakiwa Moshi mjini hawajivunii kuwa wako kwao

Mbeya
1. Mbeya imegawanyika maeneo matatu ambayo ni Uhindini, Mwanjelwa na Mbalizi
2. Wenyeji wa Mbeya wakienda mikoani na kufanikiwa hurejesha uwekezaji maeneo ya Mwanjelwa na Mbalizi
3.Wenyeji wakiwa Mbeya wanaona fahari kuwa hapo
4. Wenyeji wanaendesha shughuli za kiuchumi katika maeneo yaliyoanishwa hapo juu

TANBIHI: IDADI ya watu wenye asili ya Mbeya ni wengi hapo mjini lakini kwa Moshi mjini ni wachache na kwa kawaida hata kama anaendesha shughuli hapo mjini ikifika jioni anarudi milimani hivyo hapo mjini wanaoishi ni watu kutoka maeneo ya nje ya mkoa. Hata hivyo kwa namna moja ama nyingine wanafanana katika tabia ya kujibagua
i. Moshi wanatambuana huyu katoka Machame, Kibosho, Marangu, Uru, Old Moshi, Rombo nk
ii. Mbeya wanatambuana huyu katoka Kyela (goigoi kwa kazi za kujituma na wanajivuna), Tukuyu, Mwakaleli (Busokelo), Ileje, Mbozi, Chunya nk
iii. Idadi ya watu walioko Mbeya mjini ni kubwa ukilinganisha na Moshi mjini hivyo huduma nyingi kuhitajika

USHAURI
Ili Moshi mjini pawe na sifa za kuwa Jiji wanashauri kuishawishi serikali izungumze na mwekezaji wa kiwanda cha sukari TPC waachie maeneo ya mashamba ya miwa yaliyoko Fonga, Kikavu, Chekeleni kisha ifidiwe maeneo ya Mikocheni (Mijongweni), Kahe na kiasi fulani Msitu wa Tembo ili mji upanuliwe na wenyeji pamoja na watu wengine wenye mtaji kuwekeza shughuli za uzalishaji mali na huduma kukidhi vigezo
 
Likewise miaka 50 ya uongozi wa CCM; taifa limeshindwa kumaliza tatizo la vyumba vya madarasa na madawati shule ya msingi.
 
Unasahau kuwa chama cha mapinduzi, kimejaa ubaguzi, majungu, na fitna Chadema hata wangefanya mazuri gani lkn Meko hawezi appreciate, kama alifikia anakwenda sehemu anaponda alafu baadae akiambiwa mbunge wa hapa wa CCM anasema basi kafanya kazi nzuri.
Umenikumbusha Charles Njonjo aliyepata kuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Katiba nchini Kenya miaka hiyo.
Huyu bwana alipenda sana wazungu na uzungu kupindukia,kiasi akawa anawaponda nakuwadharau waAfrika.
Inasemekana siku moja alipanda ndege,kama kawaida majina ya rubani yalitajwa,na yote yalikuwa ya kizungu.
Baada ya ndege kutua Njonjo akawa anasifia jinsi rubani wa kizungu alivyotua kwa umahiri wa hali ya juu,lakini baada ya kuambiwa kuwa huyo rubani pamoja na kuwa na majina ya kizungu lakini ni Mkenya mweusi ghafla akabadili kauli eti kumbe ndiyo maana nimesikia mshtuko usiokuwa wa kawaida wakati tunatua!!!!!!.
 
Mara nyingi huwa naiangalia Tanga na Mbeya halafu najiuliza kwanini Moshi haijawa Jiji hadi leo?

Najua kwamba Mwanza na Arusha zimeiacha mbali Moshi kimaendeleo na kipopulation lakini siyo Tanga ya Makamba na Mbeya Sugu.

Chadema imekuwa na mbunge na madiwani wengi Moshi kwa miaka 20 mfululizo lakini imefeli zaidi ya kuongoza kwa usafi tu, ngoja tumuone mbunge na madiwani wa CCM 2020/25.

Jaffo mtuangalie na sisi bwashee.

Johnthebaptist
Usseri Rombo

Maendeleo hayana vyama!
Mji wa Moshi ulioko mkoa wa Kilimakyaro uwe jiji? Kwa hiyo kila kiongozi anayetokea eneo fulani apewe fadhila ya jiji hizo ni akili zenye tija?

Fufueni kiwanda cha vipuri na 'Kilimanjaro Machine Tools Manufacturers Ltd' haraka acheni longolongo.
Fufueni kiwanda cha ngozi 'Moshi Leather Industries Ltd)' & '(Himo Tanneries Ltd)'.
Fufueni kiwanda cha madawa ya kilimo 'Twiga Chemicals Ltd'. Fufueni kwanda cha mazao ya mbao ' Kiliwood Products Ltd)'.
Fufueni kiwanda cha voberiti ' Kibo Match Ltd'.
Fufueni kiwanda cha karatasi 'Kibo Paper Ltd'.
Fufueni kiwanda cha magunia 'Tanzania Packaging Manufacturers'.
Fufueni kiwanda cha kukoboa mpunga Kilimanjaro Paddy Hulling Co. Ltd''.
Fufueni kiwanda cha matunda Bella view Fresh Fruits Company Limited'.'
Acheni kupora eneo la mashamba ya kiwanda cha sukari kisha kujenga makazi yenye jina la nchi ya Marekani [New Land]
Acheni kubadili kijiji cha wafugaji cha Mserekia kwa kuvamia na kuanzisha makazi hatarishi kwa ustawi wa upanuzi wa mashamba ya miwa ya kiwanda cha TPC kwenda Kahe.

Badilisheni tabia za wakaazi wa maeneo ya PASUA, KIBORORONI, FONGA, CHEKELENI na MAJENGO ziwe za kiungwana na maadili mema.

Punguzeni kushobokea kuoa au kuolewa na wazungu kwa kuwinda mali zao-naishia hapo

Eneo la wilaya ya Same liko sawa na ukijumuisha wilaya za Siha, Hai, Rombo, Marangu, Moshi-Maajabu ya duni halafu wanalilia kuwa jiji wanaposhauriwa namna bora ya kuipata sifa hiyo wanakushobokea-Too pathetic

Kwa hiyo usinifyatukie wakati wala hauijui vizuri Kilimakyaro

Hakikisheni mji unarejeshewa baridi asili kama ilivyokuwa zamani.
 
Uhuru kamili kwanza kwa raia ndio mambo yajiji badaye. Itakusaidia nini ukiwa na jiji halafu unanira ya maksai shingoni.
 
Tangia msukuma aingie madarakani ni kelele tuuu zisizokuwa na maana. Mkuu, Eti hawa ndio wakupewa nchi kweli!!!! Na ndio maana miaka yote since Tanzania ipate uhuru haijawahi kuongozwa na hawa jamaa, tungekomaje!!! Heri ya mzungu ama mwarabu atuongoze lakini sio hawa.
 
Mara nyingi huwa naiangalia Tanga na Mbeya halafu najiuliza kwanini Moshi haijawa Jiji hadi leo?

Najua kwamba Mwanza na Arusha zimeiacha mbali Moshi kimaendeleo na kipopulation lakini siyo Tanga ya Makamba na Mbeya Sugu.

Chadema imekuwa na mbunge na madiwani wengi Moshi kwa miaka 20 mfululizo lakini imefeli zaidi ya kuongoza kwa usafi tu, ngoja tumuone mbunge na madiwani wa CCM 2020/25.

Jaffo mtuangalie na sisi bwashee.

Johnthebaptist
Usseri Rombo

Maendeleo hayana vyama!
Kuitwa jiji ni jina tu jengeni mji wenu
 
Kama maamuzi yenyewe ndio kama hayo yaliyofanywa kwa Ilala/Dar, wacha isiwe jiji tu. Kama Masaki, Mbezi, Beach Morocco, Mwenge ni sio sehemu ya jiji lolote hapa Tz, itakuwa Moshi?

......hayana chama!
 
Aisee una uchungu sana na Wachagga

Hakuna mtu anataka usifie chochote cha Moshi

Wewe una kwenu,mmeendelea,ni JIJI,ya nini unaifatafata Moshi isiyokua na hadhi ya JIJI?

Plus hawataki kua JIJI kulinda mlima wao,wewe unawapa pressure ya kua JIJI kama nani?

Utamaduni wa makabila mbalimbali ni mzuri na mbaya,wachagga ni hivyo hivyo,wana mazuri na mabaya...

Wewe inakuuma nini kabila kua na mabaya yake?

Nadhani unatamani sana ungekua mchagga,too bad umezaliwa pengine,kubali kwenu,wachagga achana nao,huna haja ya kuwatukana ili wewe ujisikie vizuri

Kabila lako ni precious pia,huna haja ya kutukana na kudharau makabila mengine ili ujisikie lako ni bora

I think ungekua na uwezo wa kuchagua wazazi wakuzae,ungechagua wazazi wa kichagga,too bad umezaliwa na wengine,ni hii bitterness unayoonesha hapa ni your own problem binafsi,una majuto of things you cant control.

Relax bwana na toa hoja mujarabu,acha kutukana the whole group of people as if walishakukosea chochote
The right message has nailed the hypocrites inside the din.

I acknowledge all the insults you flamed out to defend your personality which has assisted to expose the true colour as to how you are and how mentallyweak you are angrily pewing the heartbreak after being blatantly told the truth.

I neither have interest from Moshi and Mbeya nor do I expect to degrade you as you speculate to court around mob psychosis attention.

Please read while relaxed you may approriately discern the contents aimed to forge transformation.
 
Back
Top Bottom