Kwa mheshimiwa rais kikwete tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mheshimiwa rais kikwete tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Nov 14, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Habari za kazi mheshimiwa Rais, pole sana na majukumu pamoja na visafari vya hapa na pale. Sielewi nikusalimie kwa salamu ipi, lakini bila shaka shikamoo itafaa zaidi. Mimi ninaye kuandikia barua hii ni raia wa kawaida sana. Ni mtu wa mtaani tu kama walivyo watanzania wengine.

  Nimekuandikia kupitia hapa kwa sababu sina namna nyingine kufikisha ujumbe wangu kwako. Naamini kwa njia hii, maneno yangu yatakufikia huko uliko.

  Mheshimwa, sidhani kama unatambua kuwa, hivi sasa watanzania tuna matatizo makubwa sana. Maisha yamekuwa magumu, ajira hakuna, thamani ya shilingi imeporomoka, maandamano kila kukicha, watu wasio na hatia wanaumizwa bila ya sababu, mfumuko wa bei kila baada ya masaa sita.

  Imekuwa afadhali ya Zimbabwe na Somalia. Hata mishahara ya sisi walimu sasa imekuwa kama bahati nasibu. Hayo ni machache tu, lakini kuna mengi zaidi ambayo hayaandikiki. Pamoja na yote hayo, umekuwa kimya sana. Kimya kama kifaranga kilicho ndani ya yai.

  Waswali wanasema; kukaa kimya ni namna moja nzuri ya kumpuuza anayekupigia kelele. Lakini kumbuka kuwa, kimya kingi, kina mshindo mkuu.

  Moja ya mfano wa mshindo huo, ni kile kilichotokea Mbeya. Hata ukiwa kimya, ni imani yangu kuwa ujumbe na maneno ya watanzani unayasikia kwani hata mabango barabarani hayaongei, lakini watu wakisoma wanaelewa.

  Wakati unaingia madarakani, mimi ni mmoja wa watu waliokupigia kura japo itikadi zetu kisiasa ni tofauti. Lakini mpaka sasa sijafaidika na chochote katika utawala wako. Labda cha maana nilichofaidika nacho ni kuacha pombe.

  Nimeacha kwa sababu hali imekuwa ngumu na kulazimika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Unajua kuwa umaarufu wako uliotuka sasa unabalika? Watu wanaona kuwa unawatesa sasa, wengi wanaona kuwa umewageuka.

  Vijiweni jina lako limekuwa ndiyo agenda kuu kwa sasa. Naomba ujitokeze utupe japo maneno ya kutufariji tu ili mioyo yetu iburudike na kurejewa na matumaini.

  Mengi yametokea, lakini binafsi napenda sana wanyama wa porini. Hivi ni nani aliyeswaga wale twiga kutoka porini na kuwapakia katika ile ndege?

  Mpaka sasa waliohusika wamechukuliwa hatu gani? Halafu walikuwa twiga ndama au? Manaake nadhani kumswaga twiga mzee ni kazi kubwa sana.

  Mwisho naomba ujue kuwa, wananchi hali zetu ni mbaya sana kwa sasa. Tunahitaji msaada. Nashukuru sana kwa ukarimu wako..Ni mimi raia mwema.

  Naishi Mbezi hapa Dar es salaam.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  msg sent!
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Sikubaliani, kama ni msaada nenda kwa Cameroun anatoa lakini kuna masharti
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  atasoma lakini hawezi kuelewa'uwezo wa kuelewa hautokani na degree mkuu'
   
 5. O

  Omr JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hayo malalmiko yako yote yana wizara zake. Peleka huko, usituletee unafiki hapa.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Uh,anaweza akataka kujua mbez bichi au ile ya m0ro rod?
   
 7. W

  Wababa Senior Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukome kabisa, me kura yangu ckumpa huyo ndugu yake na cameroon, me nilizisoma alama za nyakati toka kipindi kile anagombea ukuu wa kaya, hahahahahahaha kumbe ka elimu kangu ka standard 7 kananisaidiaga kuona mbali? Thanx God.
   
 8. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mmmmh huyu jamaa hata tv sidhani kama anaangalia, je hii barua atasoma??
   
 9. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kwa Jk ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa ukitegemea ataelewa afurahi na kuanza kucheza!
   
 10. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  yupo active sana kwenye facebook labda umpelekee huko. JF anaiogopa
   
 11. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hahahah TV anaangalia espn (NBA)
   
 12. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  napita njia.
   
 13. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha haaaa pole sana ndgu yangu... kwamba faida uliyopata sana sana ni kuacha pombe kutokana na ugumu wa maisha
   
 14. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Omr unapotoa ushauri, inabidi umfahamishe maana hafahamu, kwa mfano ugumu wa maisha wa wananchi apeleke malalamiko wizara gani?

  Unakumbuka kwamba Kikwete aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania? Kwanini hiyo kauli asiiachie Wizara husika? Omr Tanzania tupo katika wakati mgumu sana kutokana na kuwa na ombwe la uongozi hata kama wewe Omr binafsi unafaidika na hili Tatizo la uongozi usipende kujitokeza mbele kiasi hicho.

  Kaa kimya kula bata kimya kimya kama Wahindi wanavyokula bata kariakoo kimya kimya kutokana na udhaifu wa ukusanyaji kodi hapa nchini.

  Ni ushauri tuu.
   
 15. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,315
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Mkuu msg yako imetulia sana, nakushauri uipost kwenye baadhi ya magazeti ili watu wengi waione. Hlf nipe ruhusa niipeleke kwenye wall facebook yake maana ni friend of mine.
  ASANTENI JAMANI NGOJA NIRUDI DARASANI NAONA TICHA ANAINGIA.
   
 16. O

  Obinna Senior Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu Huyu jamaa huwa na wasiwasi kuwa yeye na Africa Magic Movies tu.
   
 17. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hv wewe unaona mbali kweli au ili mradi umeandika tu?
   
 18. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,026
  Likes Received: 7,419
  Trophy Points: 280
  Kwani nyie mliojibu ndiyo Vikwete?
   
 19. msani

  msani JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  msg nzuri sana ila ni ngumu sana kuielewa kwa mtu jk,ufahamu wake sidhani km ataambulia kitu hapa,utaona km atakujibu!!!
  mi nadhani ili kumvutia ungeongeza yafuatayo
  -mialiko mingapi inatoka kwa cameroon
  -obama anamuhitaji lini
  -km kuna bembea mpya zimetengenezwa
  -km babu seya ametoka jela
  -uhusiano wa liyumba na vick-shika umeisha
  -migodi mingapi inahitaji kukabidhiwa kwa marekani kwa ubia na yeye

  tofauti na hapo sidhani km atakuelewa
   
 20. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nyie wote wanafiki tu, mnasogeza muda siku iishe.
   
Loading...