Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo tu

the horticulturist ahsante, ila kuna jamaa yangu yupo tengeru training institute aliniambia variety ni chanzo kikubwa akanishauri nitumie hybrid seeds

Kama nilivyokueleza aina nyekundu(red varieties) zinatatizo hilo kutatua kua na calenda ya umwagiliaji na mbolea pia panda kwa nafasi stahiki kati ya kitunguu na kitunguu(5 to 8sm) na mstar hadi mstar (15sm) na tuta mpaka tuta (30 sm)

Nami ni zao la horti tengeru nimeitimu mwaka huu
 
Last edited by a moderator:
kaka naomba unielekeze upandaji wa viazi mviringo ? je wakati wa kupanda natakiwa niweke mbolea? naomba procedures please

Viaz mviringo huwa tunatumia viaz vilivyoanza kuota ,andaa shamba piga matuta umbali wa sm 75 mpaka 100 tuta hadi tuta,viazi upande umbali wa sm 30 mpaka 40 kati ya kiaz na kiaz vile vile ukubwa wa shimo uwe sm5 mpaka 15 ili shina la mche lije kua imara.

Kuhusu mbole kiazi uhitaji virutubisho vya aina nyingi kwa pamoja hivyo ni vyema utumie mbolea ya wanyama au mimea iliyooza vizur uiweke shambani kwako unaweza weka hata wakati wa kulima ukailimia shambani.
 
Habari mkuu,naomba unipe somo na uzoefu, unapo lima shamba kubwa la vitunguu (1-5acre) kwa kua vitunguu tuna-transplant haitakua kazi sana kulimaliza shamba hilo? pili, kuna njia nyingine tofaute na kutransplant? kama ipo nielekeze hatua zake
asante.(eneo langu linaudongo wa mbuga, mweusi unaonata)
 
Ni vizur ukuze kwenye kitalu ili uweze kuweka spacing uitakayo shambani,kuhusu ugumu wa activity ni kutokana na eneo kwanini usilime kwenye eneo dogo tu hata la 1acre uwe na uhakika wa management na soko?
 
mkuu horticulturst nasikia pia pilipili ( mbuzi na type nyingine but sio hoho) yaweza kupandwa pembezoni ikafunction kama live barrier je ikoje hii ni sahihi?
 
swali lingine je? nawwza kupanda aina mbili tofauti za nyanya kwennye ekar moja kama vile shanti na anna f1?
 
The horticulturist naomba unielimishe spacing za pilipili mbuzi, mbolea ya kupandia, mbolea ya kukuzia pia na chochote cha ziada kuhusu kilimo cha pilipili mbuzi.
 
mkuu horticulturst nasikia pia pilipili ( mbuzi na type nyingine but sio hoho) yaweza kupandwa pembezoni ikafunction kama live barrier je ikoje hii ni sahihi?

Hapana haifai sababu hazina uwezo wa kufungamana ikazuia wadudu,magonjwa na upepo maana ndio kazi kuu ya live barrier
 
The horticulturist naomba unielimishe spacing za pilipili mbuzi, mbolea ya kupandia, mbolea ya kukuzia pia na chochote cha ziada kuhusu kilimo cha pilipili mbuzi.

Spacing tumia 45 kwa 45sm kwa 150 sm,pandia map/dap,kuzia urea/npk ila kipindi cha maua na matunda piga mbolea zenye calcium na potassium uzuie kudondoka maua na matunda
 
Mkuu Samahani Naomba Msaada Wa Maelezo Juu Ya Mbegu Ya Nyanya Iitwayo Kipato F1 Sifa Yake Na Utunzaji Na Namna Ya Upandaji
 
Me nilikuwa nahitaji kujua kuhusu kilimo cha tikiti in general kuanzia uoatikanaji wa mbegu na favourable climate kwa zao hili ikiwezekana kwa hapa tanzania huwa yanalimwa sana mikoa gani?? Na vitu vinahitajika kwa ajili ya kilimo hiki
 
Back
Top Bottom