Kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo tu

Samahan wakuu ..napenda kujua zaidi kilimo cha matango.kama kina msimu,magonjwa,bei sokon,aina ya tango, aina ya udongo kinapo kubali sana.
Asanteni
 
Samahan wakuu ..napenda kujua zaidi kilimo cha matango.kama kina msimu,magonjwa,bei sokon,aina ya tango, aina ya udongo kinapo kubali sana.
Asanteni
Kilimo chochote msimu wake haswa huwa sababu ya maji kama unamaji ya uhakika ya kumwagilia muda wowote unayalima, magonjwa si sana ila haswa hushambuliwa na mdudu nzi wa matunda (fruit fly) ni vyema ukafahamu njia za kumcontrol kabla hata ya kuanza kulima,bei sokoni inategemea na soko-msimu-mahali kwa Arusha hufika mpaka roba la tpc tsh 150,000/= na huweza shuka mpaka elfu 20,000/=, Aina hutegemea na soko ila Arusha hupenda membamba marefu haswa hapo utapata mydas (hybrid) na ashley (o.p) , aina ya udongo halihitaji udongo wa kutuamisha maji muda mrefu kama mfinyanzi hivyo ukiwa na udongo wenyechanganyiko mzuri wa kichanga,mfinyanzi na tifutifu (loam soil) ni bora sana maana hautopoteza maji kwa haraka na pia hautosimamisha maji kwa muda mrefu,
Ahsante na karibu sana
 
kwa maswali na majibu kwa masuala ya kilimo cha mboga,matunda,maua,viungo na dawa.Wataalam na wakulima tukutane hapa
Naomba kupata mawasiliano ya moja kwa moja na ile taasisi inayojihusisha na kilimo cha maparachichi kwa mkoa Kilimanjaro, wanaitwa AFRICADO, nikiwatafuta kwa google siwapati vizuri. Ni inbox tafadhari, nina shida nao sana
 
Samahan wakuu ..napenda kujua zaidi kilimo cha matango.kama kina msimu,magonjwa,bei sokon,aina ya tango, aina ya udongo kinapo kubali sana.
Asanteni

Mkuu da'ritoh , vipi ulifanya hiki kilimo cha matango? tupe mrejesho kaka. namimi nafikiria kufanya hii kitu
 
Jamani mi mgeni.ndio kwanza leo natokea kwa jukwaa.lengo jamani ni ushauri nataka kulima pilipili mbuzi.nataka kujua soko lake likoje na mda gani hiyo pilipili mbuzi ina soko kuliko kipindi kingine?
 
@hortculturalist nimepanga kulima Tangawizi lakini changamoto kubwa ni mtaji hususani bei ya mbegu na niliwahi kutana na mtu akanambia kua kunauwezekano Wa kupanda mbegu kidogo halafu zikichipua I mean kuota, hutoa machipukizi mengi then unaweza kata hicho chipkizi na mzizi wake na kupandikiza sehemu nyingine na mmea ukakua? msaada tafadhari
 
Ukiamua kulima basi usifanye majaribu invest mahitaj stahiki upate mavuno bora na mengi pita shortcut upate mavuno machache ,remember shortcut si njema kama tatizo mtaji basi lima eneo dogo ambalo unauwezo nalo
 
kitu kingine naomba kujua ni aina ya udongo Tangawizi kwa kiasi kikubwa hulimwa kwenye udongo mwekundu je kwenye udongo mwingine haiwezekani?

kwa ujuzi wako ni magonjwa gani hasa hukumba zao hili?
 
kitu kingine naomba kujua ni aina ya udongo Tangawizi kwa kiasi kikubwa hulimwa kwenye udongo mwekundu je kwenye udongo mwingine haiwezekani?

kwa ujuzi wako ni magonjwa gani hasa hukumba zao hili?
Uzuri wa mazao ya viungo huwa na magonjwa machache sana sababu ya asili yake hivyo usiwe na shaka ,kuhusu udongo zao lolote linalozalia kwenye mizizi linahitaji udongo ambao ni loose ili liweze kutanuka ,mfinyanzi hua sio mzuri kwa mazao ya mizizi
 
Naomba kujua gharama za kilimo biashara cha mahinda ya kuchoma kwa ekari moja niko mlandizi maji yapo na pamp ninayo
 
Naomba kujua gharama za kilimo biashara cha mahinda ya kuchoma kwa ekari moja niko mlandizi maji yapo na pamp ninayo
Mahindi very simple sijui kwa uliko ila kwa Arusha eka moja inahitaji from laki nne mpaka tano kutegemea mbolea utaweka mara mbili au tatu na return kwa eka ni from laki saba mpaka milioni moja kutegemea na soko limekaaje
 
Haswa nini ulitaka kufahamu ndugu kwenye pilipili mbuzi !?
Ningepata kufahamu ulimaji wa pilipili mbuzi kwa kuzingatia aina za mbegu ...inahitaji udongo aina gani ...inakaa muda gani shamban mpaka kuvuna pia soko lake na unaweza kupata kwa makadirio kiasi gani kwa ekari moja....pia cost ake ya kulima mkuu

Nashukuru kwa mchango wako!
 
Mtaalam
nakusalim sana..kuna mdau mmoja nnlikua napitia comments kauliza kua mbegu ya kitunguu anzia siku ile ya kusia,,inatakiwa ikae siku ngapi kwenye kitalu ??

Pia naomba kufahamishwa kua hivi kitunguu huwa kinapigwagwa buster??
 
Back
Top Bottom