Kwa maswali haya sensa imefeli kabla haijafanyika!

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,801
12,247
Kwanza maswali ni mengi bila sababu ya msingi halafu mengi ni ya kijinga na kipuuzi. Ingewezekana kabisa kuwa na dodoso lenye maswali machache na ya msingi. Baadhi ya maswali wangeachiwa watendaji wa mitaa/vijiji wakisaidiwa na wenyeviti wao kwani ni ya kifamilia zaidi na yanahitaji utulivu.

Kwa ufupi hii itakuwa sensa ya hovyo kabisa kufanyika nchini na itachukuwa muda mrefu bila sababu yo yote. Wananchi wengi watayakwepa au kuyapuuza baadhi ya maswali kwa kusema uongo!

PIA, SOMA:
- Maswali 100 ya sensa ya watu na makazi ya mwaka
 

Attachments

  • Orodha ya Maswali ya Sensa. Sambaza 22.08.2022.pdf
    178.7 KB · Views: 6
Tunafanya sensa mara moja tu kila baada ya miaka 10....na bado watu wanaona maswali mengi! Issue hapa ni maswali ya msingi, yatasaidia kutambua ukubwa wa mahitaji ya msingi, by the way...huhitaji haya certificate ya darasa la 7 kuyajibu!
 
Hayo maswali yako wapi? Acha kuandika vitu nusu nusu
Kwani wewe hawakutumii kwenye simu yako?
Ilitakiwa liwepo swali linalohusu katiba mpya. Kujua kama wananchi wanafahamu katiba iliyopo na endapo wangehitaji katiba mpya.

Pia swali la uchumi liwepo. Je, mwananchi anaonaje hali ya kiuchumi katika eneo lake? Nzuri, inaridhisha, mbaya au haieleweki! Ili sasa wazee wa tozo wajue kama waendelee na tozo au wasitishe kwanza!
Screenshot_20220822-154438.jpg
 
Unaandika kama unakimbizwa na malaya vile! We vp? Lete hayo maswali hii ni thread mbovu kuwahi kutokea humu jamii forum! Au shemeji yko amekunyima chakula?
Acha uzembe na uvivu wa kusoma na kutafuta! Hata ungewekewa hapa hayo maswali ungetaka tukusomee!
 
Back
Top Bottom