Naombeni kujibiwa maswali haya na kupewa ufafanuzi zaidi kwa yeyote anayejua

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Najiulizaga Mimi juu ya maombi haya ambayo watu wanaombaga kanisani na misikitini.

Je, ni kweli hivi ndivyo wanavyo muombaga Mungu au watu ambao walikuja kutupa dini walituficha system ya kumuomba Mungu na anasikia hapo hapo na kutowa msaada

Nina brother yangu fulani ambaye ni mchungaji huyo brother yangu alikuwa anaumwa kwa madai yake yeye alikuwa anasema kuwa kuna kitu Kilikuwa kinabana koo lake lakini kila akienda hospital madocta walikuwa hawaona tatizo lolote katika vipimo vyao kwa hiyo ikawa vigumu kumtibia.

Hali yake ilikuwa mbaya saana watu kila siku kumuombea lakini wapi kila kukicha kubadirisha wachungaji wanapiga maombi lakini Hali ya mtu ilikuwa mbaya saana.

Familia ikaona huyu tunaweza kumpoteza kizembe hivi hivi wakaenda kwa Waganga wadunia jamaa yule alipiga dunia zake pale mtu akapona kabisa.

Na sio tu tukio ilo kuna matukio mengi ambayo yanashindikana kwa makanisa yanaenda kupona kwa waganga wa dunia hii.

Maswali yangu mimi najiulizaga inawezekana Vipi mganga ambaye sisi tunaambiwa wanamuomba shetani aweze kuponya mtu kwa matatizo yake
Lakini Mungu tunaambiwa ana nguvu kuliko kitu chochote Ana shindwa kufanya ivo ivo

Je, hivi tunavyoomba ndivyo anavyoombwa Mungu au sisi tunakosea maana mimi na amini labda watu hawajui kumuomba Mungu maana na amini kila kitu kinataratibu zake sio kufika tu na kuanza kupayuka maneno
 
Kupona ni imani, mwenye imani yoyote ile duniani anaweza kupona bila hata kuomba Kwa mungu wa waislamu na wakristo.
 
Kwani kila uchoomba unapewa?
Pia Unaweza ukaomba akakupa kwa wakati wake autakae yeye.
Alafu si kila tatizo linatibiwa kwa maombi tuu mwambie aache huo ujinga
 
Back
Top Bottom