Kwa mara nyingine tena nimeumizwa

Badili mbinu za kutokea,ukipenda awamu hii hakikisha unafanya kila ufanyalo ugegede kwanza,ikiwezekana uweke mpira nyavuni aka umdunge mimba mengine yatajiweka sawa yenyewe,tatizo ulilonalo hujui zama zimebadilika bado unawinda kwa rungu wakati kuna Ak47
Yani seriously umdunge mtu mimba kisa tu asikuache? I thought ni wanawake wasiojiamini tu ndo wanategeshea mimba, hadi nyie wanaume? Acheni ubinafsi, mtakuja kutesa watoto bure, kama mtu hakupendi ni hakupendi tu period.
 
Pole sana Mkuu... Upo msemo mmoja usemao LIKUEPUKALO LINA HERI NDANI YAKE, unajua kuna Jambo moja tunajisahau, Leo Mungu hazungumzi na watu ana kwa ana, nachofanya ni kuonyesha ishara, kwa hiyo binafsi kitendo tu Kuwa na mawasialiano yanayosua sua ningeshajua hapa ni Mungu ananionyesha ishara Kuwa huyu sio mkewangu, wala nisingesubiri mpaka aniambie Kua Tupo wawili katika mizani yake.

Mpotezee, inauma sana Ila jikaze, Huo ndio uanaume, wala usiwachukie wanawake, kuna wengine wanajielewa sana, kuna wengine macho juu juu.. Kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa yote tu. Huenda kuna Jambo anakufundisha Ili aje akupe mwanamke wa maisha yako. Kwajinsi niwajuavyo wadada kuna siku atarudi tu kukuomba msamaha. Usiangalie nyuma, Daima Mbele Kama Yanga, Nyuma Mwiko. Mpotezee tu, Tafuta pesa Mkuu,
Kweli kabisa mkuu. Akizingatia maneno yako atajiponya maumivu yake.
 
At times huwa nafikiria kwamba there is always a price to pay just for being a decent/ good person.

Siku zote, usitegemee watu wote kukutreat vizuri simply because wewe unawatreat vizuri. Wengine hata hawaoni thamani ya hicho unachokifanya kwao, maybe wataiona thamani yako baadaye sana. Hufanyi investment kutenda mema, unafanya kile ambacho moyo wako unakitaka na ndicho kinachokupa wewe furaha. Just do it anyway. Ipo siku utakutana na atakayejua thamani yako, machozi yote utayasahau.

Kingine, siku zote usije ukaziignore "red flags". Mawasiliano yanapungua tu ghafla au mtu anakwambia kabisa eti "mpo wawili nawachuja, ila wewe nafasi yako ndo kubwa zaidi", jamani jamani tupende ndiyo ila na akili zetu ziwe active. Basi Mshukuru tu Mungu, ulimwomba mke mwema wako na yeye kakupruvia kuwa huyo aliyeondoka siye mke mwema wako.

Ugulia tu kwa muda, futa machozi na usichoke kumuomba Mungu hadi pale atakapokupa mkeo mwema. Usilaumu sana, usikufuru ila shukuru tu kwa kuwa katika kila break up unajifunza kitu kipya, cha kukufanya uwe mtu bora zaidi huko mbeleni. Na uwe na uvumilivu pia coz vitu vizuri havijagi kirahisi rahisi wakati mwingine. "Never give up on love, people hurt you; not love". "Don't let the actions of other people turn you cold on the inside"
Ah! Maneno kuntuntuna hayo.
 
Mkuu unaweza kumfanyia mwanamke yooote hayo lakini bado asiridhike akawa kichwa maji tu. Yaani treatment na handling kwa baadhi ya wanawake sio kitu na hawaithamini,na ndio maana finally mkiachana wao ndio wanajutia sana na kulia everytime.
Unatakiwa uwe mgumu ndio heshima itakuwepo. Mwanamke anatakiwa akuone unajithamini sana kuliko unavyomthamini yeye, hapo atajua kwamba hata kumpiga kibuti ni jambo dogo sana, akijua una misimamo mikali hawezi kuthubutu kutingisha kiberiti kwa sababu anajua hutambembeleza. Asikwambie mtu, hakuna kitu wanachokiogopa wanawake kwenye mahusiano kama kupigwa kibuti.
 
mbona sijawahi kumfanyia mtu yoyote kitu kama hiki? mbona sikuwahi kudhamiria ubaya wowote na nalipwa yasionistahili. kama mwanadamu nimeumia sana kwa kweli
nikisimulia na mimi yaliyonipata utaanza kulia kwa ajili yangu.mwache aende tunamuomba mungu akitujibu tunapinga tena hatujielewi.mwache huyo ibilisi aende omba dua mke atakuja na utafurahi.onyo akirudi kwa vyovyote usimsikilize wala kumkaribia.na lazima atarudi tu hata kama miaka itapita.atarudi kivingine piga moyo konde.HII NI MUHIMU HATA AKIRUDI KESHO USIMPOKEE
 
kumtongoza mwanamke mpaka kumuweka kwenye himaya yako si kazi ndogo... na hasa ambae unataka kusafiri nae kwenye safari ya mahaba. Unaweza ukawa na mkakati mzuri lakini hukujua ni wapi pa kuutumia....unapomuomba Mungu akupe nke....mke bora..usitegemee utampata kanisani pekee, elewa mazingira yote ya dunia binadamu wanaishi. Nakushauri endelea Kumuomba Mungu but usimpangie wapi pa kumpata....jichanganye yuko anaekusubiri mahali.....ila suala lako la kusema tutasubiri mpaka cku ya ndoano litakukost braza.....keep going....pole sana..
 
Wakati mwingine tunapo kataliwa na wale tunaohisi kuwa tunawapenda hatupaswi kuvunjika mioyo isipokuwa tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa kutuepushia mabalaa mapema na kuendelea na maisha.......hizi sio nyakati za kubembelezana kwenye mapenzi bali ni nyakati za kuambiana ukweli kwenye mapenzi ili kuepuka kupotezeana muda....

Mkuu sio kwamba una bahati mbaya kwenye ulimwengu wa mahaba bali unaangukia katika mikono isiyo salama na ndio chanzo cha maumivu yako lakini haimaanishi kuwa ndio mwisho safari yako ya kimahaba...bali ni changamoto zinazokujenga kuwa baba imara wa familia yako na utakuwa na uwezo wa kufanya chaguo kwani moyo wako utakuwa na ganzi na hutakuwa na hofu na maumivu.....
 
Ya Mungu muachie Mungu,na ya wanawake waachie wanawake ndugu yangu Pendael24

Hawa viumbe ukiwawaza sana utakufa tu bure kwa BP!Nenda hapo gengeni chukua kiroba chako anza kukipiga taratibu utamsahau tu
 
nikisimulia na mimi yaliyonipata utaanza kulia kwa ajili yangu.mwache aende tunamuomba mungu akitujibu tunapinga tena hatujielewi.mwache huyo ibilisi aende omba dua mke atakuja na utafurahi.onyo akirudi kwa vyovyote usimsikilize wala kumkaribia.na lazima atarudi tu hata kama miaka itapita.atarudi kivingine piga moyo konde.HII NI MUHIMU HATA AKIRUDI KESHO USIMPOKEE
Kusema ukweli huyu binti tunasali kanisa moja, na kwa macho ya kawaida anaonekana ni mcha Mungu na pengine ndio hivyo alivyo. Kilichoniumiza ni kwanini kunidanganya na kunipotezea muda? najua hela si ishu sana lakini kunikubalia na kunihakikishia mwishowe eti hawezi kumwacha alie nae! si angesema napema tuu jamani.
 
kumtongoza mwanamke mpaka kumuweka kwenye himaya yako si kazi ndogo... na hasa ambae unataka kusafiri nae kwenye safari ya mahaba. Unaweza ukawa na mkakati mzuri lakini hukujua ni wapi pa kuutumia....unapomuomba Mungu akupe nke....mke bora..usitegemee utampata kanisani pekee, elewa mazingira yote ya dunia binadamu wanaishi. Nakushauri endelea Kumuomba Mungu but usimpangie wapi pa kumpata....jichanganye yuko anaekusubiri mahali.....ila suala lako la kusema tutasubiri mpaka cku ya ndoano litakukost braza.....keep going....pole sana..
Kwa kiasi fulani nimevunjika moyo ndugu yangu, kama mtu anaeonekana anamcha Mungu lakini ndani yake anaudanganyifu da hao wengine itakuwaje? Lakini nikubali tuu ushauri wako maana njia za Mungu si kama zetu si tunona pafupi mno.
 
Whaaaaaaàt?? House girl anakutema?????
Ndio hivyo ndugu yangu, na alikua analalamia kuonewa nampa moyo na mwombe lakini ndio hivyo,sikamchukia ila angeniambia tuu ukweli kwakua ndani yangu nilikua namaanisha ukweli.
 
Back
Top Bottom