Kwa mara nyingine tena CCM waliiweka rehani Zanzibar Oktoba, 2020. Mara hii ilikuwa too much

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Ilikuwa ni Zanzibar tena kwenye hesabu kali za kuvurugwa na kuvurugika. Mara hii hesabu zilikuwa kali kuhakikisha kinatumika kivuli cha uchaguzi ili kuivuruga Zanzibar na mwelekeo wao wa kudai haki kwenye Muungano na usawa.

Kazi ya CCM kwenye hili haijawahi kuwa na makosa tokea kuundwa kwake mwaka 1977. Mara hii rungu lilipata mpigaji kwa maana hakuna aliweza kusema kwi kutokana na mazingira ya kisiasa yaliyokuwepo kuelekea uchaguzi wa 2020. Nadhani wote tunajuwa mazingira yalivyokuwa.

"Theory" ni ile ile ya kutumia "tool" ya chama ili kufikia malengo ya kuipoteza Zanzibar kimkakati.

Mbinu za kuwapoteza watetezi, kuwafukuza kwenye chama watetezi, kutumika mbnu ya kuwagawa na kuwatawala wazanzibari, mbinu za kuwatesa na kuwafunga watetezi bado zinaonekana zinachelewesha Agenda.

Hesabu ilikuwa zaidi ya Hesabu za kale za kuwapeleka wajinga waliopitiliza kwenye vyombo vya maamuzi ili mambo yanayohusu Zanzibar yapite kiulaini lakini uchaguzi wa 2020 ulikuwa "TOO MUCH"

Inashangaza eti CCM Zanzibar walishindwa kungamua janja ya kitoto ya kupewa pipi ile ile na kusahau. Eti kwa kisingizio cha Kuibeba CCM kutawala hawakuona HATARI YA KUKUBALI KUPELEKA WABUNGE WASIO NA UWEZO KULE DODOMA kiasi kile?

Kwamba hawajafahamu hadi leo mbinu za kuimaliza Zanzibar kimkakati.

ISHU ILIKUWA HIVI

Mfumo wote wa uchaguzi Zanzibar ulidhibitiwa na "System" kutoka Vyombo vya Muungano. Walichoamini CCM Zanzibar ni kiu yao ya kudhibitiwa Upinzani ambao kwao wao ndio kitisho kikuu cha Maslahi yao kumbe hawakujua kulikuwa na hesabu kali nyuma yake.

Mfumo uliokuwepo na nguvu za Mwenyekiti hazikuwaamini wazanzibari katika zoezi la Uchaguzi. Wasimamizi wote wa Uchaguzi wakiwemo wale wa majimbo walikuwa watu wa" System" wanaopokea maagizo ya moja kwa moja katika mfumo wa kiaskari kwa mkubwa wake hata kama anaviunja sheria.

Lengo ni kusimamia maagizo ya kutekeleza walichoelekezwa na hatimae kwa mara ya kwanza eti ngome ya Upinzani kule Pemba ikawa ngome ya CCM.

Kilichoshangaza hao waliwekewa hawana uwezo wowote zaidi ya ukereketwa. Hii dhambi ilikuwa na hesabu ya kuwaburuza mbeleni na kufikia hesabu za watawala kirahisi.

Leo hii hakuna Mbunge wa CCM mwenye uwezo wa kuhoji chochote chenye maslahi na Zanzibar zaidi ya kupiga makofi.

Ukweli huo umeonekana wazi na ilikuwa ni suala la muda tu. Si tu kwamba hesabu ya kwanza ni kuhusu ajenda ya kuongeza muda wa Uraisi Mwenyekiti aliepita, lakini kuna theory ya kudumu ya Zanzibar ilikuwa nyuma yake.

Nani atabisha kwamba mkakati ule ulikwa na madhara kwa Zanzibar kwa ujumla wake ingawa ulifichwa kwenye kivuli cha CCM kushinda Zanzibar?

Bado CCM kuna Tatizo kwa maslahi Mapana ya Zanzibar na mbinu zao za kuwatumia mapandikizi na wahafidhina ambao kwao wao hawajui kutofautisha nchi, utaifa na CCM.

Kwa nini janja hii hawakuiona? hivi hawana uwezo wa akili? jee ni maslahi yao na familia zao au kulikuwa na nini?

Yaani unatafuta wabunge wa kuisadia Zanzibar unadodosa kwenye bunge, kuna mtu gani pale wa kuweza kuibua mambo makubwa na kuyajengea hoja?

Acha ninyamaze kwanza.

Kishada.
 
Back
Top Bottom