CCM Mara Hapatoshi

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Dawa ni CCM kutema wote hawa ili ianze na watu wapya kabisaaa... ili kuiponya Mara na kutunza heshima ya Muasisi wa taifa na chama ambaye alitoka mkoa wa Mara.

Haiwezekani kundi dogo la watu wachache likamiliki siasa, chama na ukwasi kwa maslahi yao. CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi siyo cha mabepari.

Makongoro mtoto wa Mwl. Nyerere alipodhaniwa Mara haiwezi kwenda naye walimvua uenyekiti mkoa kabla ya muda wa uchaguzi wa chama kuwadia.

Sasa hawa ni akina nani hadi Ma-RC, Ma-DED na Ma-DC wauogope mkoa wa Mara kwa sababu yao?

Kusema kweli uchaguzi mkuu ni mgumu ndani ya CCM (uchaguzi wa ndani wa teuzi za nafasi za kushika dhamana za dola) kuliko nje ya CCM.

CCM break political emirate of these Bolsheviks and Mensheviks to set Mara on a Perestroika trajectory.

Mara has had enough of them!
 
CCM mmeanza kuwachukia wanaccm waliokatwa mikia
Hivi sasa mifugo ikiibiwa Rorya Mbunge (wanayemuita ahsante Magufuli) hawezi kufuatilia na kufanikiwa kurejesha mifugo hata akishirikisha 100% vyombo vya ulinzi na usalama. Hii sasa ni karata ya kumuondoa jimboni.

Lakini kundi hili lina mbinu za kurejesha mifugo ya wizi hata iliyoishavuka mipaka ya jamhuri hata bila msaada wa vyombo vya dola.

Hapo unagundua nini?

Vita ya madaraka imefikia hatua ya baadhi ya viongozi wa CCM walio vitani hata kujiuzulu na kukibeba CHADEMA hadi kupata ushindi kwa lengo tu la kumkomoa fulani na CCM huku yeye kivuruge akiendelea kubaki mwanaCCM.
 
Back
Top Bottom