Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
We siunajua kukemia mbona humkemei huyo muasisi wa udini...mtei nae umemsahau muasisi wenu wa chama kweli naanza kuami wewe unachuki na jk..ukizungumzia mambo ya ufisadi awamu zote yalikuepo toka kwa Nyerere alichokua anafanya yeye ni kuwaamisha mashirika waendelee kula pole we kwakujifanya kipofu na kiziwi

Nyerere siyo mwasisi wa udini!mzee wa watu kwanza alihakikisha kuna watawala wa tofauti kila mara.(yani mkristo then musilam nk(Na alifanya hivyo kwasababu pengine kuna watu waliokuwa na mawazo kama hayo ya kina JK ya kutaka uongozi si kwasababu ya merits)

Mimi sikumbuki siasa za mwalimu bali nazisoma.Lakini nakuhakikishia kwamba tuliishi kwa udugu kama watanzania.Sasa kama kuna issues,mwalimu alishakufa kitambo.Jk kwa bifu lake alipompiga chini kwenye uteuzi(ambapo kama na yeye angetumia akili alijuwa baada ya Mwinyi kwa utaratibu wa ccm,ni mkristu),aliona kwamba ni udini
,na sasa ndo anataka kulipiza kisasi?

Kama ni mtu alipenda usawa na hakuwa mnafiki,basi angejuwa ni zamu ya mwenzake.Imefika sasa kachaguliwa kwa tiketi ya ccm.Na sasa udini umepamba moto!kweli mwalimu aliona mbali licha ya mapungufu yake.
 
nashukuru kwa complements za ukweli kuhusiana na maendeleo kwenye maeneo hayo,tunataka the whole country iwe hivyo.

Kuhusu hilo la Dr Slaa,nafahamu yeye ni muiraq,lakini nilikuwa nikimjibu yule aliyesema kwamba "kama JK ni mdini na fisadi,basi mimi ni mchagga na chadema",aliijibu posti yangu niliyokuwa nikilaani kitendo cha JK kupita misikitini na kuwahadaa ndugu zetu wampigie kura kwa vigezo vya dini na wala si kwamba atalifanyia nini taifa.Siasa za hatari kweli kweli.

Na miye ndo nikamwambia Slaa naye alikuja kuomba kura na kusema mimi mchagga?ama alienda makanisani na kuomba kura akisema mimi mkristu mwenzenu?

Kama Slaa angesema maneno kama hayo,ningemwita mdini vilevile.Hapa JF ni jukwaa huru.
Wekweli mdini tena ni mtu mbaya sana jk aliyasema hayo mskiti gani na lini ?
 
Nyerere siyo mwasisi wa udini!mzee wa watu kwanza alihakikisha kuna watawala wa tofauti kila mara.(yani mkristo then musilam nk(Na alifanya hivyo kwasababu pengine kuna watu waliokuwa na mawazo kama hayo ya kina JK ya kutaka uongozi si kwasababu ya merits)

Mimi sikumbuki siasa za mwalimu bali nazisoma.Lakini nakuhakikishia kwamba tuliishi kwa udugu kama watanzania.Sasa kama kuna issues,mwalimu alishakufa kitambo.Jk kwa bifu lake alipompiga chini kwenye uteuzi(ambapo kama na yeye angetumia akili alijuwa baada ya Mwinyi kwa utaratibu wa ccm,ni mkristu),aliona kwamba ni udini
,na sasa ndo anataka kulipiza kisasi?

Kama ni mtu alipenda usawa na hakuwa mnafiki,basi angejuwa ni zamu ya mwenzake.Imefika sasa kachaguliwa kwa tiketi ya ccm.Na sasa udini umepamba moto!kweli mwalimu aliona mbali licha ya mapungufu yake.
Unalazimisha kumwita mtu mdini vielelezo Huna kwataaifa yako tumekushtuki ....mbona muasisi wenu wa CDM hutaki kumguza yeye alisema wazi bila kubabaisha maneno
 
Wekweli mdini tena ni mtu mbaya sana jk aliyasema hayo mskiti gani na lini ?

Sijui ni msikiti gani,ni wakati wa kampeni.

Hivi baada ta Mwinyi,JK alitaka kutawala bila ya kujali ule uwiano uliokuwepo wa culture ya ccm kuteua mkristu then musilam.

Halafu mashabiki wake wadini humu eti wanakuja na mfano mbona mwalimu alitawala miaka 25 na yeye ni mkristu.

Hapa kwa utaratibu wa JK hatuwezi kuwa na umoja wa kitaifa.Ina mana alitaka baada ya Mwinyi iwe yeye ili miaka aliyotawala mkristu iwiane na atakayotawala muislam.

Haya ndo mawazo ya JK na haya ndo matokeo yake.Si mtu wa suluhu hata kidogo.Ni mtu wa visa,tatizo visa vyake hivi sasa ni vya kidini.Na karata hiyohiyo anaitumia ili asiulizwe kuhusu utumbo anaoufanyia nchi hii!
 
Wakuu

Mimi mpaka sasa kuna kitu nashindwa kukielewa. Honestly speaking demages anazofanya Kikwete kiuchumi, kijamii na kisiasa ni kubwa kupindukia na zitakuwa na long term effects lakini inaoneka hakuna mtu hata mmoja (zaidi ya Mnyika na Ulimwengu) mwenye nguvu ya kumsema, kumkemea, au kumzuia.

Japokuwa kila mtu anaongelea suala la udini kiushabiki (kama simba na yanga) lakini hili suala ni suala nyeti mno na inashangaza jinsi ndugu Kikwete anavyozidi kulilea na kulikuza. unfortunately watu wengi hawaelewi unyeti wa jambo hili na wanaendeleza ushabiki.

kiuchumi na kisiasa ndi sijua hata niseme nini. I am speechless on the damages that this man has caused to our young Nation.

Hakika huyu mzee ni janga kuu la kisiasa nchini Tanzania. Aligombea urais kwaa ajili ya personal reasons na ametawala for personal gains only. Watanzania na mambo yao ya msingi is at the bottom of his concerns.

sasa ndio tumeelewa lkn kwa njia ngumu,kwamba tunapochagua kiongozi ni kwa manufaa yetu.na tunaposhawishiwa kwa fedha.NI KWA HASARA YETU
 
wewe Ritz acha ujinga na thread yako ya kijinga. Ninyi ndiyo mnaleta udini hapa nchini mkidhani ni jambo la kujivunia. Jaribu kutumia akili ndogo uliyonayo kutafakari ushauri wangu.

Ulimwambia mtei nae atumie akili alipotaka uwiano wadini
 
Familia yetu ni ya wakristo na waislamu na tupo imara pamoja kama zamani. Kijiji chetu kina waumini wa dini zote mbili na bado tunazikana kama zamani. Sijui umeandika haya baada ya kufanya utafiti wa kiasi gani?
Mkuu tutajie hilo gazeti lenye kusambaza sumu hizo.

Unaishi kijiji gani?
 
Mwalimu aliona huyu jamaa hajakomaa akili kwasababu alijuwa kuwa baada ya Mwinyi,ni lazima kiongozi atakayefuatia(kwa mujibu wa taratibu za unofficial za ccm)kuwa sasa ni zamu ya mkristu.

JK akawa mbishi kunga'ng'ania,na baadaye kuwaaminisha waislam wenzake kuwa mwalimu alikuwa mdini.

Na ndo anatoa siri za serikal eti kuwaonyesha kuwa ni kweli kuna udini na mfumo kristo.

Sasa unafanya nini huko ccm?halafu tena huo mfumo kristo wanalalamikiwa chadema ambao hata madaraka hawajawahi kushika?
 
Mwl. Nyerere alipochukua nchi mwaka 1961, alirithi jeshi lililokuwa lina mtii Bibi wa Kiingereze (Malkia wa Uingereza). Kwa maneno mengine jeshi hilo lilikuwa lina nidhamu ya kimalkia malkia.

Mwalimu aliliona hilo ni tatizo. Nadhani mtakumbuka tatizo hilo lilivyokuja kuwa kubwa kiasi cha kutafuta wanaigeria kuja kutuliza "umalkia malkia" wa jeshi mwanzoni mwa miaka hiyo ya 60.

Mwalimu hakuliacha tatizo hilo liendelee, alichukua hatua. Akalibadirisha Jeshi, jeshi likaondokana na "umalkia malkia" kupitia mpango wa siasa jeshini. Mpango huo ukafanikwa kwa kiasi kikubwa tukapa jeshi letu yaani Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambalo kwa sasa linajulikana kama Jeshi la Waafrika kwa heshima kutokana na mchango wake kwa bara la Afrika.

Nimeyaeleza haya yote kuonyesha kuwa linapokuwepo tatizo linatakiwa litatuliwe, na litatuliwe kwa umakini ili suluhisho hilo la tatizo liwe la manufaa ya kudumu.

Tusingoje tatizo liwe kubwa kiasi cha kuagiza "wanageria" kuja kutuliza mambo. Maana kwa wakati huu wanageria hawapo na hata wangekuwepo hawataweza kutuliza balaa la ugomvi wa kiimani.

Ni kweli tatizo la kiimani limeota mizizi na linazidi kushamiri kwa kasi ya ajabu. Watanzania wote kwa imani zetu tunalo jukumu la kuondoa tatizo hili. Kwa kuwa tatizo hili linahudumiwa (ndiyo maana linaoota mizizi), watanzania tunayo kazi moja na muhimu ambayo tunatakiwa tuifanye kuepusha janga hili la kiimani.

Kazi hiyo ni muhimu kuifanya, na ilitufanikiwe tunatakiwa tuchague njia sahihi za kulikomesha tatizo. Njia ninazoziona ni muhimu kwa na zilizopo ni kukata mizizi ya tatizo, kumdhibiti anayepanda mbegu za tatizo, na kudhibiti anaye hudumia tatizo.

Njia ya haraka kufuata kabla ya kulimaliza kabisa tatizo ni KUMDHIBITI ANAYEPANDA TATIZO. Watanzania tunamjua/wajua wanaye/wanaopanda mbegu za tatizo hili la kiimani, tushirikiane kuwadhibiti.

Kelele zangu hizo.

after all nimefuatilia huu mjadala kuanzia mwanzo mpaka mwisho,nilichokiona hapa kuna baadhi wana-acknowledge kuwa tatizo lipo and still pointing fingers to some politicians,wengine wanakataa kuwa tatizo halipo ila sisi tunaolizungumzia sana kwenye hizi social networks ndio tunalikuza na ndio wadini haswa,kundi la mwisho linakubali kuwa tatizo lipo nakusort out way foward,mimi nipo pamoja na hili kundi la mwisho...tulipofika hatuhitaji kumnyooshea kidole yeyote yule,kwa knowledge ndogo tu ya conflict resolution niliyonayo,naamin ili kutatua tatizo fulani baina ya certain conflicting parties ni kuwa both parties must realize that a certain situation that sorrounds them is a problem,kwa hiyo hatua ya kwanza kabisa kwa sisi watanzania ni kuikubali hii hali kama tatizo,from there tuchukue hatua madhubuti kama taifa kukabiliana na hili tatizo kwani zitakapolipuka vurumai hazitachagua kama wewe ulikua unashabikia udini au la,naamin bado tuna mda kidogo umesalia kuondokana na hili tatizo kabla halijaleta madhara zaidi.
 
Wekweli mdini tena ni mtu mbaya sana jk aliyasema hayo mskiti gani na lini ?

SIERA,
Huyu jamaa mdini sana halafu mnafiki mzandiki, anadhani msikitini kama Kanisani mtu yeyote anaweza kusimama na kusema lini JK alisimama Msikitini na kusema kwanza JK ni nadra sana kwenda msikiti tofauti na Maamur Upanga.

Halafu anakuambia Nyerere alikuwa sio mdini wakati Vatican wanajiandaa kumuita mtakatifu kwa kazi nzuri ya Kanisa.
 
Last edited by a moderator:
Sijui ni msikiti gani,ni wakati wa kampeni.

Hivi baada ta Mwinyi,JK alitaka kutawala bila ya kujali ule uwiano uliokuwepo wa culture ya ccm kuteua mkristu then musilam.

Halafu mashabiki wake wadini humu eti wanakuja na mfano mbona mwalimu alitawala miaka 25 na yeye ni mkristu.

Hapa kwa utaratibu wa JK hatuwezi kuwa na umoja wa kitaifa.Ina mana alitaka baada ya Mwinyi iwe yeye ili miaka aliyotawala mkristu iwiane na atakayotawala muislam.

Haya ndo mawazo ya JK na haya ndo matokeo yake.Si mtu wa suluhu hata kidogo.Ni mtu wa visa,tatizo visa vyake hivi sasa ni vya kidini.Na karata hiyohiyo anaitumia ili asiulizwe kuhusu utumbo anaoufanyia nchi hii!
Lakwanza Huna uwakika nalo ushafeli ......uwiano upi unaozungumza kwaiyo Nyerere alimchagua mwinyi ili pawe na uwiano!!? Another point less unahisi vitu usivyokua na uhakika navyo....najua kwenye nafsi yako inakusuta kuongea uwongo.... Haya na nyinyi chadema mnampango gani wa kumsimamisha muislam this time hau zamu ya muislam haijafika
 
Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
1) www.wikipedia.com/tanzania
2) www.arc.com/tanzania

web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????

Ndugu yangu RC ni wasomi wanajua namna ya kufanya sensa ya watu wao. Kwa taarifa yako wanajua kila muumini na kuna jumuhia nchi nzima na mtoto anapozaliwa na kubatizwa taarifa zake utunzwa sambamba na kumbukumbu zinazopatikana ofisi za vizazi na vifo. Acha sisi waislamu tuendelee kushangaa kwa ujinga wetu eti tunashindwa hata kujihesabu!!!!!!!!! Hivi tunapokutana miskitini uwa tunafanya nini????
 
SIERA,
Huyu jamaa mdini sana halafu mnafiki mzandiki, anadhani msikitini kama Kanisani mtu yeyote anaweza kusimama na kusema lini JK alisimama Msikitini na kusema kwanza JK ni nadra sana kwenda msikiti tofauti na Maamur Upanga.

Halafu anakuambia Nyerere alikuwa sio mdini wakati Vatican wanajiandaa kumuita mtakatifu kwa kazi nzuri ya Kanisa.
Soma huo ujinga wake mwingine alonijibu hapo chini sijui Kama Yuko sawa kwenye kichwa chake
 
Last edited by a moderator:
Mwalimu aliona huyu jamaa hajakomaa akili kwasababu alijuwa kuwa baada ya Mwinyi,ni lazima kiongozi atakayefuatia(kwa mujibu wa taratibu za unofficial za ccm)kuwa sasa ni zamu ya mkristu.

JK akawa mbishi kunga'ng'ania,na baadaye kuwaaminisha waislam wenzake kuwa mwalimu alikuwa mdini.

Na ndo anatoa siri za serikal eti kuwaonyesha kuwa ni kweli kuna udini na mfumo kristo.

Sasa unafanya nini huko ccm?halafu tena huo mfumo kristo wanalalamikiwa chadema ambao hata madaraka hawajawahi kushika?

ndugu yangu nakuheshimu sana na mimi ni mfuatiliaji mzuri wa posts na comments zako,kilichofanya huu mjadala ukawa mrefu kiasi hichi ni hii tendence ya kunyoosheana vidole na kumtafuta mchawi,sasa akiwa pointed mwanasiasa ambaye member fulani humu ana maslahi nae inasabisha emotions zinatawala badala ya hoja,anashambuliwa mtoa hoja badala ya hoja.well tumeshaacknowledge tatizo,what is the way foward?jk na kizazi chake watapita but what about Tz?tujenge nchi hii kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho
 
Nchi ilipofikia,credits huwa anapewa rais na serikali yake,kwahili la udini,hakuna ubishi umeshaota mizizi.Na sijawahi kusikia kauli ama vitendo kutoka kwa JK vya kukemea haya mambo ya udini.

Kinachonifanya niamini ni JK,ni kwasababu hao wanaopinga kasi ya upinzani,wanapoijibia serikali ya ccm,basi wanaoonyesha chuki za wazi kabisa za kidini.Ule udugu tuliokuwa nao wakitanzania haupo tena,na sijui utarudi kwa njia gani.

Kuna habari kuwa hata mtu na mke wake wanataka kutoana roho kwasbabu hizo hizo.Sheick Ponda alipotoa kauli kinyume na yakwake kuhusu sensa,kaliachia na gazeti lenye kusambaza sumu hizo huku akilifungia lenye kusema ukweli(mwanahalisi)

Ninamini kabisa kuwa tulipofikia,uwezekano wa kuingia kwenye vurugu na mapigano ya kidini ni mkubwa kuliko wakati wowote ule kwenye historia ya Tz toka tupate uhuru.

Kama JK ni mdini,tufanyeje?Ni wazi anapenda haya yaendelee kuwepo kwasababu ni kama anauwa ndege wawili kwa jiwe moja,yani kwasababu yeye ni fisadi na mdini,basi issue za ufisadi wake anazifukia kwa kupenyeza sentiments za kidini kwasababu anajuwa the issue is extremely sensitive.

Je kama taifa tutapona dhidi ya udini huu wa JK?je kukitokea mapigano,nani atakuwa responsible?Je nini kifanyike kukomesha udin8I hu?ama tumeridhika?!....

Mimi pia nina hasira sna na Mambo haya. Mwaka Fulani Mrema alipotikisa nchi kwenye uchaguzi walimchafua kwa kusema ni mchaga, mpaka leo lugha hiyo inazunguka miongoni mwa wa TZ. Cuf walipokuja juu walisemwa wanaendekeza Uisilamu, mpaka leo dhambi hiyo inatutafuna huko visiwani. Chadema wamekuja wanaambiwa wakatoliki, mpaka sasa matokeo ya dhambi hii yanazidi kuwa makubwa na mabaya. Yote haya ni CCM na siasa zao. Uchaguzi ujao tusikubali ujinga wa aina kama hizi.Tunaacha misingi ya katiba (mtu asisemwe kwa misingi ya rangi, dini, wala kabila lake) Upuuzi mtupu huu
 
Sasa utajuaje uwiano bila kupata data ambayo ingepatikana kutoka kwenye zoezi la 'censer'? Ila itakuwa kazi kweli kweli kila dini kuwakilishwa katika utawala. Kumbukeni dini sio ukristu na uislamu tu kama ambavyo inaelekea baadhi yetu tumejiaminisha. Dini ni imani yo yote ile aliyo nayo mtu kuhusiana na masuala ya kiroho. Hakuna binadamu asiyekuwa na dini!!!!
 
Lakwanza Huna uwakika nalo ushafeli ......uwiano upi unaozungumza kwaiyo Nyerere alimchagua mwinyi ili pawe na uwiano!!? Another point less unahisi vitu usivyokua na uhakika navyo....najua kwenye nafsi yako inakusuta kuongea uwongo.... Haya na nyinyi chadema mnampango gani wa kumsimamisha muislam this time hau zamu ya muislam haijafika

JK angekuwa si mdini,basi akili yake ingeonekana kuwa imekomaa!hilo tu.Na akili yake ingekuwa imekomaa,angejuwa baada ya Mwinyi si yeye.Umeelewa?
 
ndugu yangu nakuheshimu sana na mimi ni mfuatiliaji mzuri wa posts na comments zako,kilichofanya huu mjadala ukawa mrefu kiasi hichi ni hii tendence ya kunyoosheana vidole na kumtafuta mchawi,sasa akiwa pointed mwanasiasa ambaye member fulani humu ana maslahi nae inasabisha emotions zinatawala badala ya hoja,anashambuliwa mtoa hoja badala ya hoja.well tumeshaacknowledge tatizo,what is the way foward?jk na kizazi chake watapita but what about Tz?tujenge nchi hii kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho
Tatizo ni ccm,lakini tuanze kwa kumwajibisha rais mdini.Hatutaki rais wa wakristo ama waislam,bali rais wa watanzania.Kiongozi wa nchi anayewagawa wananchi wake kwa siasa za udini hafai!we might need a referundum on this.Kukaa kwake kimya huku haya yakiendelea kunaonyesha jinsi asivyo fit kuwaongoza watanzania.
 
Nyerere siyo mwasisi wa udini!mzee wa watu kwanza alihakikisha kuna watawala wa tofauti kila mara.(yani mkristo then musilam nk(Na alifanya hivyo kwasababu pengine kuna watu waliokuwa na mawazo kama hayo ya kina JK ya kutaka uongozi si kwasababu ya merits)

Mimi sikumbuki siasa za mwalimu bali nazisoma.Lakini nakuhakikishia kwamba tuliishi kwa udugu kama watanzania.Sasa kama kuna issues,mwalimu alishakufa kitambo.Jk kwa bifu lake alipompiga chini kwenye uteuzi(ambapo kama na yeye angetumia akili alijuwa baada ya Mwinyi kwa utaratibu wa ccm,ni mkristu),aliona kwamba ni udini
,na sasa ndo anataka kulipiza kisasi?

Kama ni mtu alipenda usawa na hakuwa mnafiki,basi angejuwa ni zamu ya mwenzake.Imefika sasa kachaguliwa kwa tiketi ya ccm.Na sasa udini umepamba moto!kweli mwalimu aliona mbali licha ya mapungufu yake.

Hivi mwaka 1992, huo unaolalamikiwa kuwa na MOU kati ya serikali na kanisa ulikuwa chini ya utawala wa nani ?
Pia, kuna haja gani kumjadili Nyerere mtu ambaye Mungu alishamchukua ( Amlaze mahali pema peponi, na njia yetu ni moja), alituanzishia mchakato, katika moja ya speech zake nilisikia akisema hivi: " ... msipoteze muda mwingi kujadili makosa yetu, ... wakati sisi tunachukua nchi hii kutoka kwa wakoloni, wasomi tulikuwa wachache, hivyo tusingeweza kufanya mambo yote sawa kwa ubora unaotakiwa kwa Tanzania nzima, ... tunaomba mjadili yale mazuri machache tuliyofanya, ... na katika yale mnayoona tulifanya sivyo, kwa wingi wenu, na wasomi wengi mlionao, muyatengenezee mkakati wa kuyarekebisha, ... na lengo lenu liwe ni kuendeleza yale mazuri tuliyofanya, na kurekebisha pale tulipokosea, ili mweze kusonga mbele ...." sitaweza kunukuu kila neno, but atleast nimeweza kunukuu baadhi ya maneno na hasa maana. Alipiga vita udini, alipigania usawa, hata kama hakuweza kwa 100%, naomba tumwenzi kwa yale machache aliyoweza kufanya. Labda niwaambie kitu: WAKATI WA MWINYI HATUJAONA MTU ALIYEMSEMA VIBAYA BABA WA TAIFA, WAKATI WA MKAPA PIA HATUJAONA, LAKINI WAKATI WA JK WATU WAMETUKANA NA KUSEMA SANA OVYO KUHUSU BABA WA TAIFA, Why ? why ? why ? ni CCM na Ukatoliki ? ni CCM na CDM ? ni CDM na ukatoliki? ni Uislam na Ukristu ? tuendelee kubaki kwenye hoja ya mtoa mada, WHAT IS OUR WAY FORWARD ?
 
Mimi pia nina hasira sna na Mambo haya. Mwaka Fulani Mrema alipotikisa nchi kwenye uchaguzi walimchafua kwa kusema ni mchaga, mpaka leo lugha hiyo inazunguka miongoni mwa wa TZ. Cuf walipokuja juu walisemwa wanaendekeza Uisilamu, mpaka leo dhambi hiyo inatutafuna huko visiwani. Chadema wamekuja wanaambiwa wakatoliki, mpaka sasa matokeo ya dhambi hii yanazidi kuwa makubwa na mabaya. Yote haya ni CCM na siasa zao. Uchaguzi ujao tusikubali ujinga wa aina kama hizi.Tunaacha misingi ya katiba (mtu asisemwe kwa misingi ya rangi, dini, wala kabila lake) Upuuzi mtupu huu

well said mkuu,bila kuwa makini na hawa wanasiasa uchwara waliofilisika hoja kichwani tutaangamia,kila siku wanakuja na mbinu mpya ili wazidi kututawala,we have to think beyond the box,inabidi tuondokane na mental slavery ili tuweze kuwang'amua na wengine,siunajua hata kwenye mwanga huu wengine bado wapo gizani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom