MKUU!
KUNA MAKUNDI MATATU YA WATU WANAOMSEMEA LOWASSA NA KUTAKA KUTUAMINISHA KWAMBA NI MTU MWENYE SIFA NZURI ZA HADI KUPEWA URAIS.
1. Kundi la watu amabao kwa kupitia mitandao aliyojiwekea huyu Bwana Edward wanamwagiwa pesa ili kuendelea kumpigia kampeni. Na hili huyu Bwana ameliweza sana maana ukweli ni kwamba pesa anayo. Kundi hili ni la waganga njaa, wachumia tumbo na walafi wasio na aibu.
2. Kuna kundi la watu ambao wanajiwekea matumaini kuwa huyu Bwana Edward akipita basi na wao watakumbukwa katika ufalme wake na kupata nafasi za kujinufaisha kwenye huo mfumo atakao weka wa uongozi. Huyu Bwana Edward hasiti kuwaambia hao watu, 'fanyeni kazi maana siku ikifika nanyi muingie huku kunako starehe za utawala.' Kundi hili ni la wabinafsi, wenye tamaa, na uchu uliojaa usongo kiasi kwamba hata ukweli wanaoujua kuhusu huyu Edward hawako tayari kuukubali.
3. Kundi la tatu ni la watu ambao kwa nafasi zao mbalimbali na hasa za uongozi wanalazimika kusema mara moja moja kuhusu Lowasa. Mara utasikia kiongozi huyu amemmwagia sifa Edward, mara mwingine atasema Edward ni chaguo la wengi na hata Mama mmoja kiongozi wa juu aliwahi kusema "Hakuna mwanamume kama Lowassa! "Hili ni kundi la wanafiki, na ndilo kundi baya kuliko mengine. Wengine kundini humu wanasema ya kumsifia Edward kama vile kumpooza kwa masaibu yaliyomkuta - haswa kufukuzwa uwaziri mkuu, lakini wengine ni kwa sababu tu ya kubalance mambo ya kisiasa kwenye Chama!
Makundi yote hayo ni ya watu walioingiwa na upofu, na mtindio wa mawazo kiasi kwamba hawaoni kwamba wanataka kuliuza taifa hili kwa tamaa zao, na bila hata haya wala soni, wakiendekeza mapungufu yao ya tamaa, unafiki, na ulafi usio na mfano.
Sijui sura zao watakuja zificha wapi siku uhaini wao huu ukituingiza kwenye matatizo kama taifa ikija tokea huko mbele!