Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Lowassa na Membe,woooote ni magarasa tu.
Kama ningekuwa mwanaccm,ningempigia debe jaji Ramadhan au John Magufuli.
At least they ''look like''
 
Nikimuona mtu anamsifia fisadi Lowasa anatamani nimwagie hata maji ya moto unampigiaje debe mtu mwizi kama lowasa?

Jiandae kubugia midonge ya kupunguza maumivu hali yako itakua mbaya sana kwa miaka kumi ijayo
 
1. EL anaweza kuamua mambo tofauti na hali ilivyo sasa.
2. Kujiuzulu kwake kuliondoa sigma nawa tu waliendelea na kazi zao za kujenga taifa, sio kama walivyotupotezea muda akina Muhongo na Tibaijuka.
3. Sijaona mtu mwingine CCM zaidi ya EL
4. Nchi inaangamia kwa umasikini, usalama, rushwa, dhuluma, Labda EL kutoka kaskazini anaweza kuisaidia nchi kutoka katika uangamivu huu.
5. Ni mchapa kazi hodari na pia anaipenda nchi, ni mbunifu.
6. Ni tajiri hivyo hatafukuzia vibiashara vya rushwa na wizi
7. Umri wake haumpi nafasi ya kufanya wizi na ubadhirifu wa mali ya umma atajikita zaidi katika kuongoza
 
Kwa lipi la maana alilolifanya Lowassa hadi apewe nchi?

Kuna sababu nyingi za kusema Lowassa hafai kuwa rais wa nchi hii licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.

Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu?

Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.

Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura Lowassa awe Rais wa awamu ya tano?
Mafisadi wajiandaa kuchafua Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake: Taarifa tulizozipata zisizotiliwa shaka ,Ni kwamba Genge la Mafisadi likiongozwa na baadhi ya wahariri na kijana mmoja Mwenye asili ya Kisomali anayetoka kanda ya Ziwa,limejipanga kwa vita ya kuanza kuwachafua, baadhi ya viongozi wa chama na waasisi wa Taifa hili ikiwemo Familia ya mwalimu Nyerere.

Mkakati huo ni mahususi kwa ajili ya kuhakikisha kila anayejiandaa kuchukua fomu kupambana na mgombea wao anachafuliwa kama alivyochafuka Mzee wao anayetaka Urais kwa udi na uvumba.Baadhi ya vijana hao wamepanga kuendesha mkakati huo kupitia Mitandaoni na baadhi ya Wahariri,akiwemo Mhariri aliyeshambuliwa miaka miwili iliyopita na kwenda kutibiwa Afrika kusini.

Wataanza kuendesha mkakati huo kuanzia Jumatatu hii kwa kutumia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na mafisadi hao. Hasira hizo zimekuja baada ya JK kutamka CCM haitompitisha mgombea yeyote mwenye doa,hii ni hatari sana!
Nawasilisha,
UKANA SHILUNGO.

 
Mleteni yoyote mnayeona anawafaa kwa upande wenu ili mumlete huko kwenye kikaango!! Tumewa-beep tu Serikali za Mtaa ila kwenye uchaguzi mkuu tunawapigia. Vijana wako tayari, Wazee wako tayari, kina mama nao kwa mara ya kwanza wako tayari kwa mabadiliko.

Haponi mtu October 2015 - Tunawatumia salaam rasmi ili mkae mkao wa kula.
 
watu tunaongea kwa jazba tu nahisia za kubebeshwa...Nani anafaa kutuongoza Tanzania hii kwa wote waliojitokeza na tunaowafikiria kujiokeza? Zaidi ya Lowasa?Kwasababu kura ndio mwamuzi wacha tupige kura. Kama ni wizi itajulikana hapo hapo na kama ni kelele zitajulikana hapo hapo.
 
Ndugu Masese Nakuunga Mkono sana, Edward ni kiongozi mwenye uamuzi , mtendaji na pia Fisadi (Japo ni mtenda kazi makini lakini hilo lipo) Juu ya ufisadi wake yeye anazitumia hizo pesa nchini na zinasaidi uchumi wetu, kuliko wale walioiba na kuziweka Uswisi. Ninachoogopa Jee tukimpa madaraka, ataendelea na mtindo wa kujilimbikizia mali kufidia alizotumia kuutafuta utawala kwa nguvu ya pesa zetu????

Tabia ya kuwaaminisha watu maneno yasiyokuwa kweli si nzuri. Hivi ni maamuzi gani muhimu yanayohusu nchi aliyafanya Lowassa kama Lowassa? Pia ni jambo la busara kujiuliza mazingira aliyofanya hayo maamuzi. Ni siri ambayo iko wazi kwamba Lowassa alikuwa na mchango mkubwa wa kumuweka JK ikulu na hivyo kama hayo maamuzi magumu aliyafanya rais akiwa huyo swahiba ni vyema tukayaangalia kwa mazingira hayo. Hivi mtu utashindwaje kuonekana una maamuzi kama aliye juu yako una nguvu juu yake? Wote munaosema Lowassa ana maamuzi magumu hebu tupe mifano halisi ya maamuzi aliyoyafanya kwa akili yake mwenyewe kama siyo kufuatilia plan za katibu mkuu wake?
 
Tabia ya kuwaaminisha watu maneno yasiyokuwa kweli si nzuri. Hivi ni maamuzi gani muhimu yanayohusu nchi aliyafanya Lowassa kama Lowassa? Pia ni jambo la busara kujiuliza mazingira aliyofanya hayo maamuzi. Ni siri ambayo iko wazi kwamba Lowassa alikuwa na mchango mkubwa wa kumuweka JK ikulu na hivyo kama hayo maamuzi magumu aliyafanya rais akiwa huyo swahiba ni vyema tukayaangalia kwa mazingira hayo. Hivi mtu utashindwaje kuonekana una maamuzi kama aliye juu yako una nguvu juu yake? Wote munaosema Lowassa ana maamuzi magumu hebu tupe mifano halisi ya maamuzi aliyoyafanya kwa akili yake mwenyewe kama siyo kufuatilia plan za katibu mkuu wake?

Kujiuzulu uwaziri mkuu???
 
Kila kona team Lowassa, mitandao ya kijamii hali kadhalika!
Swali: Mmemtathini vipi na kujiridhisha kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania?
 
Kwa kuangalia uchapa kazi wake na kudhubutu kutengeneza ajira kwa vijana.
 
Debe tupu halikosi kuvuma....yaleyale ya chaguo la Mungu SAA ivi mnalalamika...endeleeni tu ila mtavuna mnachokipanda
 
Nakumbuka mwaka 2005 ilikuwa hivi hivi kwa Kikwete watu ufahamu ulipotea kabisa sababu ya Kikwete ukiuliza sababu eti maisha bora kwa kila mtanzania wengine walikosa sababu wakasema eti ana sura nzuri
Kinachonishangaza bado watanzania ufahamu unapotea tena kwa kumshabikia fisadi papa yaani lowasa hana tofauti na Kikwete
 
Back
Top Bottom