Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kwa lipi la maana alilolifanya Lowassa hadi apewe nchi?

Kuna sababu nyingi za kusema Lowassa hafai kuwa rais wa nchi hii licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.

Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu?

Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.

Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura Lowassa awe Rais wa awamu ya tano?
hivi kikwete alifaa kuwa raisi???
Au alipewa nchi kwa lipi???
 
Hitaji la Taifa.

Taifa linahitaji kiongozi wa nchi,kiongozi atakaye waunganisha watanzania nakuendeleza pale alipoishia Mh.wetu Jakaya,

Nchi inahitaji mtu mmoja,mtu atakaye aminiwa akisema,kiongozi atakaye jua na anayejua mahitaji ya wakati ya nchi katika zama hizi za ushindani wa kiuchumi,Huyu lazima alete matumaini kwa maskini katika sekta za Elimu, Afya,Kilimo na uzalishaji katika viwanda,huyu lazima awe na mikakati katika kufufua ajira na kupata masoko.

Nchi haihitaji kupewa Malaika wasio na mabawaa kuongoza,Bali kiongozi mwenye njozi hata akiwa na mapungufu akubali kuwa chini ya kivuli cha Mungu wa Abrahamu,

Rais atakayejua umoja na amani ni matokeo ya Haki kwa wananchi,Rais atakajua raalimali zetu ni Amana na akiba ya kuweka kukopa katika Dunia na kuinua uchumi wa nchi,

Kiongozi atakayefufua reli ya kati na kupunguza gharama za kuharibu Barbara,Rais atakaye saidia walimu kupata nyumba za kuishi,kutoa uhakika wa madawati kwa watoto wa maskini na kuwalipa walimu mishahara bora Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kupata makazi bora na masirahi zaidi.

Nchi inahitaji kiongozi mwenye maono kutoka hapa alipojitahidi Jakaya,

Rais wa nchi lazima awe na agenda kwa nchi,hawezi kuambiwa ndani ya miezi minne aongoze watu na nnchi,lazima yeye awe na nia binafsi ya kiutumishi na maono kwa kuivusha nchi katika bahari ya Shamu,

Huyu hawezi kuwa wa kikundi cha watu wachache kwa maslahi ya wachache,huyu atajulikana kwa matendo na mwitikio kwa umma,

Huyu lazima awe na huruma kwa watu miln 45,lazima ajue marafiki wakimsaidia akashinda wampe Uhuru wa kimkakati kulitumikia Taifa na kuleta matumaini mapya,

Rais huyu lazima ajue Mungu ni mtawala wa mbingu na nchi akubali maongozo ya kimbingu katika kuikataa laana katika nchi apewayo na Bwana Mungu wake,

Ndugu zangu huyu si mwingine ni huyu mzalendo,Edward Ngoyai Lowassa kiongozi mvumilivu na mstahimilivu,kiongozi akiyejivika ukondoo kulinda umoja wa nchi,kiongozi aliyevumilia dhihaka na kubali mwaminifu kwa chama chake,CCM leo ingekua na hofu ya Mungu huyu angetunukiwa tuzo ya mapenz na uaminifu katika chama,huyu angepewa heshima kwa kunyamaza kimya alipoimbwa kila kona ya nchi kuwa hafai,

Kama si huruma zako Mungu sisi tungeangamia Okoa nchi yetu Mungu

Edward tunakuhitaji si kwa faida yetu,lakini kwa matumani mapya kwa mama mpika mandazi juu ya Elimu ya mtoto wake,

Mungu wa Isac na Yacob yule aliyegeuza bahari kufanya njia wakati wayahudi nyuma walifuatwa na magari ya farao yakiwa na silaha nzito,pembeni mwao ilikua milima mirefu ambayo ilijaaa wanyama wakali na mbele bahari,hata lile wingu lililokua likiwapa matumaini siku farao anawafuata lilitoweka wakakata tamaa,Mungu alimuuliza Musa unanini mkononi,akaambiwa inua fimbo yako ukayapige maji,

Lowassa unanini mkononi tunajua unawatu waliokupa Imani waambie watu wako tuvuke daraja sasa.

Long live Tanzania
Uu Goshem ya Afrika EL2015 may5
 
Kweli wajinga mtasahau ya RICHMOND kwa sababu ya kuhongwahongwa vipesa vya kijinga jinga tu.
 
Id za zamani zimeanza kuwa active sasa...tumekusikia..
 
Tumechoka na hizi nyimbo zenu zenye kibwagizo cha fisadi Lowasa
 
Mods unganisheni huu uzi wa Mzee Mamvi make tumeshajadili sana tu hii saga!
 
2015 hatutaki hizi harufu za ufisadi. Niko na jembe langu Maghufuli.
Angalau wewe umemsema mtu, lakini siyo LOWASSA, Lowassa auchukulie urais kwingine lakini siyo ndani ya chama cha Nyerere, alikataliwa na Mwalimu siku nyingi na hakuna alipokanusha mambo aliyosema mwalimu kumhusu, wosia wa marehemu siyo wa kupuuza kabisa.
 
Jamani hata wagonjwa bdo tu mnataka nao watuongoze kweli?

IMG-20150218-WA0009.jpg
Mtu anafutwa udenda hivyo , eti awe rais? Tusije tukawa kama wazambia.
 
Kuliko kumchagua Lowassa nafuu ni mkabidhi fisi kulinda bucha ya nyama atakuwa na huruma.
 
Ndani Ya ccm hakuna kiongoz mwadilifu wote ni mafisadi kwani hakuna atakayekuwa na jipya zaid Ya kuendeleza Wizi, watanzania tubadilike ccm sio mama wala baba Ya kwamba ukibadilisha utapata dhambi, kwakuokoa taifa letu na vizazi vijazo ni lazma tuitoe ccm madarakani...
 
Juzi jumapili nilibahatika kuonana na watu wafuatao kwa nyakati tofauti; wa kwanza alikuwa ni dr. Benson Bana na wa pili alikuwa ni Nape Nnauye!

Nilipomuona Nape moja kwa moja nilijikita kwenye hoja ya joto la mbio za urais linalofukuta kwa kasi ndani ya CCM kwa sasa. Kwanza Nape alinihakikishia kuwa mgombea wao (CCM) wa urais kwa sasa hata yeye hajijui kuwa ndiye atakayeteuliwa na chama.Yupo mahali na wakati muafaka ukifika atawekwa hadharani.

"Unajua mgombea wetu wa urais hata yeye mwenyewe bado hajijui kuwa ndiye ingawa tumeshamdokezea kuhusu swala la kuchukua fomu.Wapo na wengine pia tumewadokeza ingawa huyo ndiye tunamuhitaji zaidi. Haya mambo tunayafanya kwa umakini mkubwa na hatuko tayari kuwaweka watu wetu muhimu hadharani kwa sasa" alisema Nape.

Pia sikusita kumgusia jinsi ambavyo 'adui wake' Lowassa anavyojipanga na hadi sasa hata mabango ya kampeni ameshayaandaa na ndipo Nape akaamua kufunguka;
"Kwanza kabisa mimi na Lowassa siyo maadui kama unavyodai, wote tupo ndani ya CCM ni vipi tuwe maadui? Pili ni kweli kuwa Lowassa pamoja na wafuasi wake wamejipanga sana! Wameweka matangazo ya kumpamba Lowassa kila kona na kwenye mitandao ingawa hilo la mabango sina uhakika nalo. Nataka hao wafuasi wake waelewe kuwa kuna kikao cha sekretarieti ya chama ambacho kitakaa na kuyapitia majina ya waliojitokeza na kuwapima kiutendaji, kimaadili na jinsi ambavyo tutawanadi bila kuulizwa maswali magumu. Unaweza kuulizwa mbona fulani mlisema hivi na mkavua madaraka iweje leo mmeamua kumtunuku cheo ambacho maamuzi yote yatakuwa juu yake? Sasa swali kama hilo utajibu nini! Kwa kweli tunajipanga" alisema Nape.

Mimi nikamuuliza kwa mantiki hiyo sina shaka kabisa kuwa unamsemea Lowassa na watu wa aina yake. Sasa mbona wafuasi wake hamuwaelezi hayo ili wajue moja?
Yeye Nape Nnauye akanijibu kuwa ukitaka kumuua nyoka kisha ukaanza kumpiga mkia atakuzungusha huku na kule, hapo utapoteza 'target'. Ni bora ukahakikisha unakipata kichwa sawasawa kwa wakati muafaka ili ukipiga mara moja biashara iishe. Hayo ndiyo yaliyokuwa majibu ya Nape Nnauye siku ya jumapili tulipokutana maeneo ya Boko DSM.

Kwa upande wake dr. Benson Bana yeye alijikita zaidi kwenye mambo ya tafiti za kisiasa huku akiiponda Synovate kuwa imeandaa utafiti ambao inaonyesha kuwa upinzani umeifutilia mbali CCM nchini huku akidai kuwa utafiti huo ambao utawekwa hadharani hivi karibuni ni wakupikwa.
 
Lowasa ni jembe mtu mwenye maamuzi endelevu hakuna kuchekeana mtu kama huyo anaa kabisa kupewa nchi kwani kiongozi shupavu na mwenye kuijua nchi vilivyo
 
Back
Top Bottom