mkuu kuna mambo mengi mno siyo leseni peke yake,.
Tanzania mahali pazuri mno pa kuishi hata kama huna ujuzi wala elimu yoyote almradi tu uwe na shekeli kidogo, unahitaji chochote utapata iwe kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini, hati ya kusafiria vyeti vya shule, chuo nk! lakini fungakazi ya yote ni leseni za udereva, karibia kika mgeni anamiliki leseni na ukienda kwenye database ya POLISI na TRA utakuta wametimiza vigezo vyote, ila katika uhalisia si kweli. vijana wengi wa bodaboda wanazo leseni lakini hata mlango wa chuo cha udereva haujui. uzalendo umetutoka kabisa kila mtu anaangalia anapata bei gani kwenye nini! na kwa njia hii tunaimaliza nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe
Mzizi wa matatizo yote ni CCMHalafu tunashangaa tukiona ajali za kutisha kila siku?
Mzizi wa matatizo yote ni CCM
Haisaidii, kama mtanzania mmoja mmoja kwenye nafasi yake hawajibiki ipasavyo....Watanzania tuliondoe Jini CCM mara moja..
Na mfumbuzi wa matatizo ni CCM.
Imagine ingekuwa Serikali ya chadema, ikiwa Mwenyekiti anampigia simu hawara ageuze na aache safari ya kikazi aelekee Dubai kula bata badala ya kazi aliyotumwa na bunge, tena kwa gharama za bunge. Ingekuwaje?
Waswahili tuna msemo, aheri nusu shari kuliko shari kamili.
Faizafoxy waweza kuwa sahihi ukilenga individuals, lakini tukiongelea taasisi kwakweli CCM lazima iondoke sasa, tusifike mahali ilipofikia Zimbabwe! Tunahitaji mbadala wa CCM n this must be very soon before it is too late! deni la taifa linazidi kupaa, maisha yanazidi kudidimia huku kuna kilinge cha wachache wanaishi kwenye ukwasi wa kutisha, tunajiandalia bomu la nuklia
Tatizo kubwa la CCM ni upinzani mbovu.
Upinzani ukiwa na nguvu hutayaona yote hayo.
Bili kuwa na upinzani wa kweli na wenye nguvu, tukubali matokeo.
Mtakazana CCM mbovu wakati wao ndio chama pekee chenye ushawishi kwa wananchi walio wengi, unategemea nini?
Fikiri kwa rekodi ya Slaa ni nani mwenye akili timamu atamchaguwa kuwa Rais? Unataka tuongozwe na mtu hata maadili ya Kanisa lake alilosomea kanuni zake ameshindwa kuzihimili.