Amri ya RC Makalla kuhusu mlinzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa ni ngumu kiutekelezaji

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Baada ya kusikia amri ya RC Makala kwamba office zote za serikali za mitaa jijini Dar ziajiri Mgambo kama walinzi ninayo machache yanahitaji ufafanuzi:

Pia soma > RC Makalla: Kuanzia sasa Ofisi zote za Serikali za Mitaa jijini Dar zitalindwa na askari wa kikosi cha Mgambo

Kwanza amri ya RC Makala akiwa MKUU WA MKOA na MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi ya mkoa naamini amri yake inatokana na maamuzi ya kamati yake. Na kama hivyo ndivyo inabidi masuala yafuatayo yazingatiwe:

1. Kama ni LAZIMA kila Ofisi ya Serikali ya mtaa iajiri mgambo kama mlinzi wake wa kudumu ni lazima alipwe na Serikali mshahara na posho stahiki.

Kwasababu mgambo ni binadamu anastahili kulipwa kama mwajiriwa yeyote serikalini.

Mwenyekiti na watendaji wengine wa Serikali ya mtaa wote ni watu muhimu wanaofanya kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi katika mazingira magumu. Kwamfano wana uhaba wa vitendeakazi, fenicha, gharama za usafiri, umeme nk.

Kama mlinzi hatalipwa na Serikali itakuwa vigumu kwa ofisi ya serikali ya mtaa kumwajiri mgambo kama mlinzi kwa kazi ya kudumu, lakini hata kwa ajira ya muda tu, pia ni vigumu.

Mgambo kama mlinzi lazima alipwe mshahara na posho stahiki na vitendeakazi kama:
i. Sare pea mbili na boots
i. Silaha (bunduki) na vitu vingine muhimu.

Lakini katika mazingira ya serikali za mitaa yanastajili kuwa na ulinzi pote nchini Tanzania, haiwezikani kuwe na ulinzi kwa Dar pekee, kama jambo hilo ni sera ya nchi.

Vile vile kama jambo hilo si sera ya nchi itakuwa vigumu kutekeleza kwa mkoa mmoja tu wa Dar es Salaam.

Suala la ajira kwa Wanamgambo nalo ni suala la kitaifa. Kwasababu wapo mikoa na wilaya zote nchini.

Last but not least! Si lazima kila mgambo awe mwenye vigezo na tabia nzuri kuweza kuajiriwa.
Bila kuwa na mwongozo maalum wa utekelezaji wa jambo hilo huenda likazua matatizo.
 
Kwani akiajiriwa bado ataitwa mgambo?
Kwa mujibu wa utumishi wa umma serikali ya Tanzania haina mtumishi mwenye cheo cha mgambo.
Kama serikali inaweza kumlipa mtendaji wa mtaa, kata na tarafa haitashindwa kumlipa mlinzi ambaye analipwa kwa TGOS A= 300,000 kwa mwezi.
 
Kwani wanapofanya operation za kukimbiza machinga na mama ntilie huwa wanalipwa na nani? Hawana sare? Marungu?
Sasa operation ni tofauti na kazi hizi za kudumu, unafikilia mfano halimshauri ya ilala ina ofisi ngapi za s/mtaa, ?hapo uweke walinzi 2, ngumu sana!!hilo ni tukio limetokea tu basi!!
 
Unajua kuwa H/W ya Ilala inamapato makubwa kuliko MIKOA kadhaa nchi hii??
 
Wasiishie kulinda ofisini tu, walinfe hata majumbani wanapokaa hao watendaji, kwa kuwa watu wenye nia ya kuwadhuru hao watendaji walishindwa kufanya hivyo kwenye ofisini watawafuata nyumbani wanapoishi
 
Nilijua ulinzi 24/7 kama ni 8 hrs ni sawa kuajiri mgamo m1 na kumlipa kima cha chini cha mshahara.
Yah mkuu hakuna cha kulinda masaa 24 kwenye hizo ofisi,
Wanatakiwa kulindwa ni hawa watendaji aisee ,hizi serikali za mitaa zimekua kama mahakama wanasikiliza na kuamua kesi nyingi sana kwenye hizi ofisi na ukishakua hakimu utamfurahisha mtu utakera watu,imefika muda kweli wanatakiwa walindwe muda wote wa kazi.
 
Kiuhalisia swala la kuajiri mlinzi au walizi serikali za mtaa haiwezekani

1: haipo kwenye sera
2: hatuwezi mlinda mwenyekiti akiwa ofisini pekeyake kama dhima ni ulinzi
3: kama itakuwa ivo basi iwe nchi nzima
4 kama wata amua ivo basi itahitajika kuwe na mgambo si chini ya 4 ili rotatio iwepo

NB: kuna kauli zingine ziishie tu kwenye majukwaa ya siasa ila katika uhalisia ni ngumu sana
Kwasabu kama mtu alikuwa na lengo la kumdhuru anaweza mfuata hata nyumbani siyo lazma ofisini

Lakini watumishi wa uma watende haki kwa wananchi inawez saidia kupunguza vitendo vya kiuhalifu......
 
Baada ya kusikia amri ya RC Makala kwamba office zote za serikali za mitaa jijini Dar ziajiri Mgambo kama walinzi ninayo machache yanahitaji ufafanuzi:

Pia soma > RC Makalla: Kuanzia sasa Ofisi zote za Serikali za Mitaa jijini Dar zitalindwa na askari wa kikosi cha Mgambo

Kwanza amri ya RC Makala akiwa MKUU WA MKOA na MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi ya mkoa naamini amri yake inatokana na maamuzi ya kamati yake. Na kama hivyo ndivyo inabidi masuala yafuatayo yazingatiwe:

1. Kama ni LAZIMA kila Ofisi ya Serikali ya mtaa iajiri mgambo kama mlinzi wake wa kudumu ni lazima alipwe na Serikali mshahara na posho stahiki.

Kwasababu mgambo ni binadamu anastahili kulipwa kama mwajiriwa yeyote serikalini.

Mwenyekiti na watendaji wengine wa Serikali ya mtaa wote ni watu muhimu wanaofanya kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi katika mazingira magumu. Kwamfano wana uhaba wa vitendeakazi, fenicha, gharama za usafiri, umeme nk.

Kama mlinzi hatalipwa na Serikali itakuwa vigumu kwa ofisi ya serikali ya mtaa kumwajiri mgambo kama mlinzi kwa kazi ya kudumu, lakini hata kwa ajira ya muda tu, pia ni vigumu.

Mgambo kama mlinzi lazima alipwe mshahara na posho stahiki na vitendeakazi kama:
i. Sare pea mbili na boots
i. Silaha (bunduki) na vitu vingine muhimu.

Lakini katika mazingira ya serikali za mitaa yanastajili kuwa na ulinzi pote nchini Tanzania, haiwezikani kuwe na ulinzi kwa Dar pekee, kama jambo hilo ni sera ya nchi.

Vile vile kama jambo hilo si sera ya nchi itakuwa vigumu kutekeleza kwa mkoa mmoja tu wa Dar es Salaam.

Suala la ajira kwa Wanamgambo nalo ni suala la kitaifa. Kwasababu wapo mikoa na wilaya zote nchini.

Last but not least! Si lazima kila mgambo awe mwenye vigezo na tabia nzuri kuweza kuajiriwa.
Bila kuwa na mwongozo maalum wa utekelezaji wa jambo hilo huenda likazua matatizo.
Kikatiba Mwenyekiti wa Kijiji/Mtaa ana bunduki moja. Hiyo bunduki inashikwa na Mgambo. Hilo unalijua?
 
Kiuhalisia swala la kuajiri mlinzi au walizi serikali za mtaa haiwezekani

1: haipo kwenye sera
2: hatuwezi mlinda mwenyekiti akiwa ofisini pekeyake kama dhima ni ulinzi
3: kama itakuwa ivo basi iwe nchi nzima
4 kama wata amua ivo basi itahitajika kuwe na mgambo si chini ya 4 ili rotatio iwepo

NB: kuna kauli zingine ziishie tu kwenye majukwaa ya siasa ila katika uhalisia ni ngumu sana
Kwasabu kama mtu alikuwa na lengo la kumdhuru anaweza mfuata hata nyumbani siyo lazma ofisini

Lakini watumishi wa uma watende haki kwa wananchi inawez saidia kupunguza vitendo vya kiuhalifu......
Usizungumze kitu hujui. Soma katiba
 
Back
Top Bottom