Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 3,718
- 11,708
Hili la NHIF na hospitali binafsi limeonesha uwezo mdogo wa kutatua matatizo alionao waziri wa afya pamoja na huyo bosi wa NHIF.
NHIF ina changamoto kuu mbili
1. Matumizi makubwa ya fedha kwa shughuli za kuendesha ofisi, hata ripoti za CAG zimeonesha namna wanavyotumia fedha hovyo.
2. Udanganyifu wa watoa huduma za afya.
Sasa jawabu walilokuja nalo ni kulazimisha kupunguza bei za huduma za afya jambo ambalo halina uhalisia.
Kwa jinsi walivyo wavivu wa kufikiri, likiwashinda hili basi watakimbilia kuongeza asilimia ya makato kwa wachangiaji.
Mara zote wanakombilia majibu rahisi kwenye changamoto ngumu za kimfumo.
SSH aache kulea uzembe, Waziri kazi imemshinda, aletwe mtu mwingine. Kwani Dr. Gwajima alikuwa na shida gani?