Kwa idadi ya Waafrika wanaoishi nchini China, ni wazi Afrika inazalisha nguvu kazi kwa nchi zilizoendelea

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,273
Kuna idadi kubwa sana ya Waafrika nchini China, Waghana na Wanajeria wana mpaka food joints zinazopika vyakula vyao, hii yote ni kuhudumia idadi kubwa ya watu wao waliokwenda kutafuta maisha huko.

Canada wanatoa offer za scholarships kwa undergraduates kusoma degree katika vyuo. Lengo kuu ni kupata skilled workers nchini mwao. Kutokana na idadi ya watu kupungua.

Ureno walitoa nafasi za dada/kaka wa kulea watoto, kuuza supermarkets, kusafisha mahospitali. Kutokana na Covid 19 ajira za usafi ma hospitalini zimeongezeka sana Ulaya.

Tangu nchi za Afrika zipate Uhuru kutoka kwa Wakoloni, uhaba wa ajira kwa vijana umeongezeka. Nchi huru zimeshindwa kuzalisha ajira mpya baada ya wawekezaji wengi kuondoka.

Vijana wa Afrika wanasafiri safari za hatari kuvuka bahari kutafuta ajira Ulaya. Idadi ya Waafrika katika kazi zisizo na ujuzi inazidi kuongezeka na pia Waafrika wanaoishi Ulaya ni wengi na wakiwa na familia tayari.

Tumekua wazalishaji wa nguvu kazi Ulaya, nguvu ambazo zingetumuika kuendeleza bara letu kufikia maendeleo waliyofikia Ulaya.
 
Chanzo ni viongozi wabovu wa kiafrika wenye sera MBOVU waliopo madarakani kwa lengo moja tu
La kula kwa urefu wa kamba zao

nani sasa atawatoa hao viongozi wabovu, wote tukikimbilia ng'ambo..

tunapaswa kuyapigania mataifa yetu kuleta ukombozi, hata huko ulaya walikuwa na viongozi wabovu huko nyuma, ila walipambana na kuhakikisha wanajikomboa na kujijengea mifumo bora kwa vizazi vyao..

WaAfrica tunapenda mteremko, hatupendi kujitoa kwa manufaa ya vizazi vijavyo...
 
WaAfrica tunapenda mteremko aka kitonga aka uwepesi wepesi...hatupendi kuteseka wala mateso..

Ulaya na America tunakokimbilia, mababu zao waliteseka na kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wajukuu zao wanaishi maisha mazuri... walijitoa katika kila nyanja kuhakikisha ustawi wa maisha yao unapatikana tena wakitumia zana duni na teknolojia dhaifu kufikia malengo yao....LEO hii vizazi vyao vinaneemeka na matunda ya jasho la babu zao...

Sisi na Babu zetu wote wote tunapenda mteremko na sio kufanya kazi kwa bidii, jasho na damu kutimiza malengo na kujenga miji yetu hatimaye vitukuu na vilembwe vije kuishi kwa heshima...
 
Kwa ujinga huu wa kupenda kitonga na kujiendea endea tu, kuna hatari huko mbele asili na tamaduni za mtu mweusi zinaweza kupotea..

Tutaoa, kuoelwa na weupe kwa akili ya tamaa zetu huku wao wakiwa na damu kali na kuzaliwa shombeshombe wa rangi na nywele..
Huku kutangatanga na kuomba uraia kwa tamaa za maisha wengi tutalowea ughaibuni na kupoteza asili zetu za tutokako...

Wazungu/Weupe ni watu wa mikakati ya muda mrefu sana, tayari wanamkakati wa kuitokomeza Africa kiscience maana wanajua tunaoishi huku wote ni ng'ombe na lazima tuelekee kibra kwa mikakati yao ya kiscience..
 
WaAfrica tunapenda mteremko aka kitonga aka uwepesi wepesi...hatupendi kuteseka wala mateso..

Ulaya na America tunakokimbilia, mababu zao waliteseka na kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wajukuu zao wanaishi maisha mazuri... walijitoa katika kila nyanja kuhakikisha ustawi wa maisha yao unapatikana tena wakitumia zana duni na teknolojia dhaifu kufikia malengo yao....LEO hii vizazi vyao vinaneemeka na matunda ya jasho la babu zao...

Sisi na Babu zetu wote wote tunapenda mteremko na sio kufanya kazi kwa bidii, jasho na damu kutimiza malengo na kujenga miji yetu hatimaye vitukuu na vilembwe vije kuishi kwa heshima...
Unaelewa kuwa utumwa ulichangia kwa kiasi kikubw maendeleo ya Ulaya na Marekani mpaka Marekani ya Latin.
Unaposema uvivu wetu ni huu wakulima mahindi na kukosa masoko?

Sera mbovu hazijatuendeleza na viongozi kujilimbikizia mali wanaona ni haki yao.
 
tulichukuliwa watumwa kwasababu tulikuwa wajinga, leo hii tunajipeleka wenyewe kwa nauli zetu tukiwa tumesoma na akili timamu..

Hizo sera mbovu na viongozi wabovu tutawatoa kwa sisi kukimbilia Ulaya? Ni nguvu zetu na akili zetu ndio zinahitajika kuondoa hizo sera mbovu na viongozi wabovu ili akili na nguvu zipate nafasi ya kujenga msingi bora na njia bora kwa manufaa ya vitukuu na vilembwe..
 
Hapa kwetu passport ni Mali ya uhamiaji.wana kera Hawa watu.
Mama anakwambia kazi zipo nyingi labda za kuokota makopo na chuma chakavu.
Umafungua nchi passport unazikalia

utaomba pepo mbinguni utaipata utaomba passport ya tanzania hutoipata mpaka umlete babu yako aje akuthibitishe kama wewe ni mtanzania na babu kaisha kufa
 
Wenye mawazo mgando Kama wewe uwa hamkosekani.
Ila kumbuka penye RIZIKI ndo watu wanakimbilia yaani fursa Kama hizi hauwezi kuona watu wakiitana hizi ndo FURSA
Mchina hawezi kukupa kazi
Hao waafrika wengi ni wafanya biashara, hivyo vyakula ni kwa ajili ya wanaokwenda kununua mizigo,na kama ni wanaijeria wengi ni matapeli wa mitandaoni na pesa feki pale Guanzhou
 
Sawa...

Sasa nini kifanyike ili waafrika wasiende huko

Ova
Hatuhitaji wawekezaji Wazungu, wenye uwezo wa kuweka milioni 200 wanaweza kujikusanya 10 na kuanzisha mradi. Kinacho hitajika hapa sera nzuri za nchi, wanasheria wa kusimamia policies. Mnaweza kuajiri wengine.
 
Kuna idadi kubwa sana ya Waafrika nchini China, Waghana na Wanajeria wana mpaka food joints zinazopika vyakula vyao, hii yote ni kuhudumia idadi kubwa ya watu wao waliokwenda kutafuta maisha huko.

Hiyo idadi kubwa unayotaja ya Waafrika waliopo China sana sana ipo miji miwili Guangzhou na Yiwu na si kwamba ni wazalisha mali isipokuwa ni middlemen kwa ajili ya kuzungusha wafanyabiashara wageni kwenye maduka/viwanda au wafanyabiashara wanaosaidia biashara zao walizowekeza Afrika...

Hizo food joints zimefunguliwa ni vile vyakula vya kichina vipo tofauti sana na vyakula vya kiafrika na zipo kwenye miji hiyo hiyo...

Population inayofuatia kwa wingi ya kiafrika ni wanafunzi waliopo miji tofauti tofauti, na kundi hili si wazalisha mali kwa namna yoyote...

Faida pekee anayoipata Mchina kwa Waafrika huko Yiwu/Guangzhou labda Dongguan/Shenzhen na Hongkong ni kama amekuwa na uhakika wa bidhaa zake kupata direct marketing kwa soko la Afrika kwa sababu Waafrika wenyewe wapo hapo jikoni kupush kila kinachozalishwa kiletwe Afrika...
 
Back
Top Bottom