Kwa hukumu ya Jerry Silaa, Bunge linategemea kuaminiwa?

Ndugai na Naibu wake wanataka kumaanisha kuwa CAG mstaafu hajui anachokizungumza au vipi?

Kama wanalipwa kodi si waje hadharani watoe mchakato mzima wa kodi.

Kitu ninachojiuliza hivi Wabunge wote hakuna ambaye anaweza sacrifice payslip yake akaiweka hapa walau kwa kuondoka jina lake Zitto, MBOWE au @ Slaa? Wote hawa ni members hapa.

Nakuunga mkono kwa 100%. Wabunge wazalendo, watuambie/watuongezee ukweli wa jambo hii. CAG mstaafu hawezi sema uongo.
 
Ili bunge liaminike liondoe kipengele cha sifa ya kumpata mbunge ni "kujua kusoma na kuandika",lakini dereva na mlinzi eti sifa ya kuajiriwa ni kuwa na "elimu ya kidato cha nne"

Sasa kati ya makundi hayo mawili nani anaweza kusimamia,kujadili na he
shimika? anayejua "kusoma na kuandika" au mwenye "elimu ya kidato cha nne"?!

Mijadala yenye tija haiwezi kuungwa mkono kama bunge halitakuwa tayari kujisimamia na kukubali mabadiliko,ukweli na haki kutendeka.
Huwa sijihusishi kabisa na siasa zaidi ya kusoma tu hoja za watu na kupita kimya kimya, ila hatimaye umejua namna ya kunifurahisha kwa hii hoja yako
 
Mkuu bora "TOZO" hizi kuliko zile za CHADEMA kuzungusha makapu na zile alizotangaza mh.Lema akiwa huko CANADA....🤣

Iendelee kujitekenya na kucheka ila mengi likiwamo la tozo yanashabikiwa na wabinafsi waliopitiliza kama wewe tu.

Mwendelezo ule wa kisebu sebu na kiroho papo.
 
Iendelee kujitekenya na kucheka ila mengi likiwamo la tozo yanashabikiwa na wabinafsi waliopitiliza kama wewe tu.

Mwendelezo ule wa kisebu sebu na kiroho papo.
Umeamua kunihukumu ubinafsi uliopitiliza kisa mitizamo kinzani juu ya TOZO 😲🤣

Haya mkuu wangu 👍
 
Hii ni kwa kutuona je?

1. Kadhia ya mbunge Jerry Silaa ambapo yeye akiwa Mbunge na bila kushawishiwa na mtu anaona wabunge akiwamo yeye hawalipi kodi stahiki.

2. Wananchi tunajua zipo njia nyingi ambazo watu wasiokuwa na uzalendo huzitumia kukwepa kulipa kodi.

3. Hukumu ya bunge kwa mbunge Silaa ni kumlazimisha aamini kuwa analipa kodi stahiki wakati dhamira yake ikimsuta.

4. Bunge hili hili linalotumia nguvu kumlazimisha mbunge kuamini kiimani kuwa analipa kodi, ndilo linalotuongezea sisi mzigo wa malipo ya kodi na tozo.

Hivi bunge hili linategemea kuaminiwa na nani?

"Mnapojitathimini, ni heri tozo za kwenye miamala mkazitoa kabisa."

Si mbaya wakajua hatutakaa tuzikubali.
Tuache utani wabunge wanalipa kodi,hayo malipo mengine wanayopewa yanakatwa kodi kulekuke yanapotumika,mfano wanaponunua mafuta,wanalipa mishahara ta wasaidizi wao, na gharama zingine,ni sheria za nchi kua posho zingine hazikatwi kodi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Tuache utani wabunge wanalipa kodi,hayo malipo mengine wanayopewa yanakatwa kodi kulekuke yanapotumika,mfano wanaponunua mafuta,wanalipa mishahara ta wasaidizi wao, na gharama zingine,ni sheria za nchi kua posho zingine hazikatwi kodi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app

Unaonaje kama watu wote mishahara yao wakiita ni posho.

Kwamba wanalipo kodi wakienda kununua vitu? Basi sisi tunalipa mara mbili mbili.



Wewe nani kama wenyewe wanakiri u fyongo huu?

Tambua tofauti ya kutolipa kodi kwa mujibu wa sheria na kukwepa kodi kwa kutengeneza sheria muafaka kukuwezesha wewe kuifikia adhma hiyo.
 
Back
Top Bottom