Live Bungeni Kamati ya Bunge maadili inasoma ripoti ya Gwajima Na Jerry Slaa

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Mwenyekiti wa kamati ya maadili na madaraka ya Bunge ipo live kusoma ripoti kuhusu mahojiano ya Mbunge Jerry Slaa na Dr.Gwajima.
....
"Mheshimiwa Spika kauli zilizotolewa na Mheshimiwa Gwajima kamati imejiridhisha kuwa Dr.Gwajima alikiuka kanuni na taratibu za bunge."

"Mheshima Spika Kitendo Cha Josephat Gwajima kuwa akitoa maneno ameshatoa ni utomvu wa nidhamu na dharau kwa ubunge."Maoni na mapendekezo ya kamati kuhusu shitaka juu shitaka hili.

Kamati inashauri vyombo vya kisheria vifatilie na kuchunguza mwenendo wa Josephat Gwajima sababu vinahatarisha usalama wa nchi.

Swala hili lipelekwe na lishughulikiwe na kamati ya maadili ya Chama chake cha CCM

Maazimio ya Kamati...

Bunge linaazimia kwamba Mheshimiwa Gwajima apewe adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya bunge baada ya kupitisha azimio hili.

Jerry Slaa..

Mheshimiwa spika Mheshimiwa Jerry Slaa akinukuliwa akiongea na wananchi wa jimbo la Ukonga kuwa wabunge wakatwe kodi kama wananchi wengine.

Mheshimiwa Spika Mheshimiwa Jerry Slaa alikiri kuwa maneno hayo ni ya kwake isipokuwa tarehe iliyotajwa sio yenyewe ni tarehe 22 na sio 23.

Mheshimiwa Spika wakati anahojiwa Mheshimiwa Jerry Slaa alikiri maneno yake uchonganishi wa Bunge na serikali Bunge na wananchi.

Mheshimiwa Jerry alipewa onyo aombe radhi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii lakini alikaidi.

Maazimio ya Kamati ..

Bunge linapendekeza kwamba Mheshimiwa Jerry Slaa asimamishwe kuhudhuria mikutano ya Bunge miwili mfululizo

Aondolewe kwenye Ubunge wa
EAC.
 
Mheshimiwa spika kwa vitendo vilivyoonyeshwa na shahidi (Gwajima) kwa kukataa kiti alichoandaliwa pamoja na kutaka kubadilishiwa maiki inaonyesha ni dharau na utomvu wa nidhamu.
 
Maoni na mapendekezo ya kamati kuhusu shitaka juu shitaka hili.

Kamati inashauri vyombo vya kisheria vifatilie na kuchunguza mwenendo wa Josephat Gwajima sababu vinahatarisha usalama wa nchi.

Swala hili lipelekwe na lishughulikiwe na kamati ya maadili ya Chama chake.

Maazimio ya Kamati....
 
Back
Top Bottom