Bunge lanuka dhidi ya Gwajima na Jerry Silaa

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
621
500
BUNGE LANUKA DHIDI YA GWAJIMA NA SILAA

WAKATI nchi ikisubiri kwa hamu na ghamu hatima ya tozo za mihamala ya simu, Bunge limewahukumu Wabunge Josephat Gwajima wa Kawe na Jerry Silaa wa Ukonga (wote kutoka CCM).

Hii ni kufuatia kauli za kichochezi na uongo uliovuka mawingu. Baada ya kuhojiwa na Kamati mahsusi juu ya kauli zao hatimaye wakatiwa hatiani na hivyo kusukumwa nje ya Bunge na kwamba hawatohudhuria mikutano miwili ya Bunge lakini pia watapokea nusu mishahara yao kwa kipindi chote hadi January 2022.

Akiahirisha kikao cha leo Spika Job Ndugai amesema, "sisi kama Bunge tumemaliza kazi yetu, tumenawa, sasa ni kazi ya vyombo vya usalama kufanya kazi yake". Kwa maneno mengine Ndugai atashangaa kama jua litazama kabla Gwajima na Silaa hawajaingia "behind the bars" kujibu tuhuma.

Sote tunakumbuka niliandika kuhoji kwa nini Serikali ya Rais Samia inamwogopa Askofu Gwajima? Kwamba hata Waziri Gwajima alipoagiza akamatwa IGP Simon Sirro alisubiri "kadi ya mwalimo" ndipo amkamate. Aibu!

Wabunge wameongea kwa uchungu mno kwa nini Askofu Gwajima anamdharau Rais Samia? Wabunge wanahoji ni kwa sababu Samia ni mwanamke? Nimeumia sana lakini nikafarijika kwa mnuko wa Wabunge baada ya Gwajima "kumgusa mama".

Nilisema na ninarudia, kauli ya Gwajima kwamba Serikali imehongwa na viongozi wanachanja hewa ni kashfa nzito sana katika medani ya uongozi. Gwajima alilenga kabisa kwamba Rais Samia amehongwa kuuza Watanzania. Ni wakati muhafaka kuthibitisha pasipo shaka kwamba Rais alihongwa na chanjo aliyochanja na wenzake ni maji au juisi. Asipothibitisha Gwajima atendewe haki anayostahili.

Lakini pia nilipendekeza kanisa la Gwajima lichunguzwe. Je, halitumiki kutakatisha fedha? Sijui Polisi mnanielewa! Narudia, Kanisa la Gwajima halitumiki kutakatisha fedha?

Gwajima na Silaa wamethibitika na Bunge kusema uongo na kuleta taharuki kwa nchi. Hata hivyo dhambi ya Gwajima ni zito kuliko dhambi ya Jerry ya kudai Wabunge hawakatwi Kodi kwenye mishahara yao. Amethibitishiwa kuwa hata yeye anakatwa Kodi. Jerry jitokeze hadharani kuomba radhi Watanzania walioumia kwa kauli yako!

Kwa upande mwingine CCM chini ya Daniel Chongolo hakuna busara zaidi ya kumpokonya kadi ya chama (ambayo hata hivyo najua hana) ili Jimbo la Kawe liwe wazi!

Gwajima alikuwa ni mwanachama wa Magufuli si wa Chama Cha Mapinduzi, CCM. Magufuli (chama chake) hayupo, amekufa kwa chama hicho hakipo! Basi!
#MguseMamaNinuke
 

THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,700
2,000
Bunge liseme kitaalamu usalama wa chanjo na sikutumia nadharia za kwenye kuruani na biblia. AIBU!

Bunge liseme kwanini kati ya milioni 11 ambazo ni malipo ya mbuge ni 4.6 milioni pekee ndiyo inakatwa kodi. Vipi kuhusu hizi milioni 7. AIBU!
 

Goodguy

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
404
1,000
Gwaji boy yuko sawa mbona, yeye na sirikali wote hawajui kuhusu chanjo.

Sirikali haijui ndomana wizara ya afya imejichimbia kusikojulikana, Gwaji naye hajui ndomana anahoji.

Ila tutajizungusha sana mwisho wa siku huu ugonjwa ni biashara za Watu ndomana konakona nyingi sana
 

JBITUNGO

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
1,353
2,000
Bunge liseme kitaalamu usalama wa chanjo na sikutumia nadharia za kwenye kuruani na biblia. AIBU!

Bunge liseme kwanini kati ya milioni 11 ambazo ni malipo ya mbuge ni 4.6 milioni pekee ndiyo inakatwa kodi. Vipi kuhusu hizi milioni 7. AIBU!
Mimi nafikiri bunge halijajibu hoja ya Mhe. Jerry Silaa. Hoja ya Mhe. Jerry Silaa katika mkutano wake wa hadhara na wanachi wake jimboni Ukonga alijua kwa dhati kuwa mbunge hukatwa PAYE katika Basic Salary tu kitu ambacho kama ni kweli kuna basi kuna hoja ya kujibu.

Mhe. Jerry katika hoja yake alitilia wasiwasi ni kwani sitahiki zingine kama posho za wasaidishi wa mbunge kwanini zisikatwe kodi? Kwanini posho ya mafuta haikatwi kodi maana yote hayo ni mapato kwa mbunge! Hebu tujiulize swali kama posho ya mfanyakazi isipokatwa kodi je mbunge anamlipa mshahara msaidizi wake umkata PAYE na kuiwasilisha TRA?

Huu ni mfano mmoja. Mimi ni mfanyakazi na nalipwa Basic Salary na stahiki zingine na zote hizo zinaunganishwa na Basic Salary kupata PAYE kama kodi ya mfanyakazi.

Kama hii ni kweli hoja ya Mhe. Jerry ni muhimu sana kujadiliwa kwamba kama wafanyakazi wengine serikalini na private sectors sitahiki zingine zinakatwa kodi ni kwanini za wabunge zisikatwe kodi? Hii nafikiri ndio hoja ya Mhe. Jerry Silaa.
 

Bhikalamba

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
1,113
2,000
Unatatizo la kutumia H kwenye ilabu, tafadhali rekebisha

I.e :
1.mihamala[×] /miamala[√]
2.muhafaka[×]/muafaka[√]
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
14,221
2,000
31 August 2021
Dodoma, Tanzania

'Gwajima amefanya Uhaini' - Mbunge Mariam Ditopile (CCM)Mbunge Mariam Ditopile na wengine wa CCM wamesema CCM haiwezi kuvumilia kauli na matendo ya Mbunge wa CCM Askofu Josephat Gwajima . Mbunge Mariam Ditopile asema adhabu aliyopewa Askofu Gwajima haitoshi.
 

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,737
2,000
Huu nao ni ujinga mtupu. Kama wana akili kumpita Gwajiboy, kwa nini wasitoe majibu ya kisayansi?
Hoja za Gwajiboy zipo clear, wanashindwa nini kutoa majibu ya kisayansi?
Ni aibu kiasi gani watu zaidi ya 300 wanashindwa kujibu hoja za mtu mmoja, kwa kuogopa aibu hiyo, wanaanza kujihami kwa kuleta vitisho vya kitoto kitoto.
Aiiiibuuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom