Kwa hukumu ya Jerry Silaa, Bunge linategemea kuaminiwa?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,862
35,868
Hii ni kwa kutuona je?

1. Kadhia ya mbunge Jerry Silaa ambapo yeye akiwa Mbunge na bila kushawishiwa na mtu anaona wabunge akiwamo yeye hawalipi kodi stahiki.

2. Wananchi tunajua zipo njia nyingi ambazo watu wasiokuwa na uzalendo huzitumia kukwepa kulipa kodi.

3. Hukumu ya bunge kwa mbunge Silaa ni kumlazimisha aamini kuwa analipa kodi stahiki wakati dhamira yake ikimsuta.

4. Bunge hili hili linalotumia nguvu kumlazimisha mbunge kuamini kiimani kuwa analipa kodi, ndilo linalotuongezea sisi mzigo wa malipo ya kodi na tozo.

Hivi bunge hili linategemea kuaminiwa na nani?

"Mnapojitathimini, ni heri tozo za kwenye miamala mkazitoa kabisa."

Si mbaya wakajua hatutakaa tuzikubali.
 
Hii ni kwa kutuona je?

1. Kadhia ya mbunge Jerry Slaa ambapo yeye akiwa mbunge na bila kushawishiwa na mtu anaona wabunge akiwamo yeye hawalipi kodi stahiki.

2. Wananchi tunajua zipo njia nyingi ambazo watu wasiokuwa na uzalendo huzitumia kukwepa kulipa kodi.

3. Hukumu ya bunge kwa mbunge Slaa ni kumlamisha aamini kuwa analipa kodi stahiki wakati dhamira yake ikimsuta.

4. Bungehili hili linalotumia nguvu kumlazimisha mlipa kodi asiyeona kuwa analipa kodi ndilo linalotuongezea sisi mzigo wa malipo ya kodi na tozo.

Hivi bunge hili linategemea kuaminiwa na nani?

"Mnapojitathimini ni heri tozo za kwenye miamala mkazitoa kabisa."

Si mbaya wakajua hatutakaa tuzikubali.
Bunge dhaifu. Full stop
 
Bunge limeshindwa kusema je mbunge wa Tanzania anapata Gross Pay ya Tshs ngapi...

Je inakatwa kodi kama sheria inavyosema? Si tunajua mbuge anaweka kibindobi si chini ya 12m.

Sasa walipe 30% ya hiyo kesi iishe.
 
Bunge limeshindwa kusema je mbunge wa Tanzania anapata Gross Pay ya Tshs ngapi...

Je inakatwa kodi kama sheria inavyosema? Si tunajua mbuge anaweka kibindobi si chini ya 12m.

Sasa walipe 30% ya hiyo kesi iishe.

Hao kusikia ili kesi iishe? Labda kama huyu bwana amezaliwa upya:

IMG_20210829_163746_049.jpg


Madelu alipo anayetuletea tozo za uzalendo, hayuko tayari kulipa hata ndululu.

Wana ubinafsi uliopitiliza.
 

Ndugai na Naibu wake wanataka kumaanisha kuwa CAG mstaafu hajui anachokizungumza au vipi?

Kama wanalipwa kodi si waje hadharani watoe mchakato mzima wa kodi.

Kitu ninachojiuliza hivi Wabunge wote hakuna ambaye anaweza sacrifice payslip yake akaiweka hapa walau kwa kuondoka jina lake Zitto, MBOWE au @ Slaa? Wote hawa ni members hapa.
 
Ili bunge liaminike liondoe kipengele cha sifa ya kumpata mbunge ni "kujua kusoma na kuandika",lakini dereva na mlinzi eti sifa ya kuajiriwa ni kuwa na "elimu ya kidato cha nne"

Sasa kati ya makundi hayo mawili nani anaweza kusimamia,kujadili na he
shimika? anayejua "kusoma na kuandika" au mwenye "elimu ya kidato cha nne"?!

Mijadala yenye tija haiwezi kuungwa mkono kama bunge halitakuwa tayari kujisimamia na kukubali mabadiliko,ukweli na haki kutendeka.
 
Back
Top Bottom