Kwa hili Wamarekani wanatudharau

Kwa hili Wamarekani wanatudharau

We unajua viongoz wetu hawa wajui wazungu jinsi walivyo Sisi watu wa hari ya chini ndiyo tunazijua tabia za wazungu, wachina waarabu na wa Hindi kwasababu tunaishi nao kwa ukaribu Sanaa kwaiyo tunawajua tabia zao na jinsi wanavyo tuwaza akilini mwao na wanavyo tuchukulia wa Africa. Sasa hawa viongoz wetu hawa wajui watu weupe kiundani kwasababu hawaja wai kufanya nao kazi ujanani mwao wala kuishi nao mfano Mwinguru, Mama Samia kaanza kuwanao karibu wazungu ukubwani tena kazini tofauti masikin ambaye kaajiriwa na mzungu kama housegirl, shamba boy, mlinzi kwaiyo vijana kama awa lazima watakuwa wanajua tabia zao mfano wanaofanya kaz na wachina wanawajua wachina tabia zao za wizi tena wa vitu vidogo tena wachina wana njaa Sana Sasa mama Samia akienda China akiona magorofa anajua wachina Wana Manisha mazur siyo wezi watamsaidia nchi ipige atua kitu ambacho hakipo na hakita kuwepo, kwaiyo mkuu nakwambia watu weupe Wana tudharau Sana watu weusi Wana amini hatujui chochote na hawasikilizi ushauri wowote ule ukitaka ujue we kafanye nao kazi ambayo itakufanya uwepo nao masaa mengi au kafanye kazi kwenye familia zao ata Choo cha familia hurusiiwi kutumia .
Naunga Hoja

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Wana harakati na wapinzani hawana la maana
 
Tanzania haina political stability kama Kenya ndio maana unaona Uhuru Kenyatta alipokelewa na Biden wakati mama alipokewa na diaspora!

JB has no time.

Tuna chawa wengi wajinga hadi foreign affairs! It is neither a state visit nor official visit. Yaani ni matemebezi. It is a trip. State visit maandalizi yake yanachukua angalau six months na HoS asiwe amekanyanga the U.S, na angekua entitled to sleep at Blair house sio hotelini wnakomshikia Madelu mabango.

Hivi kesho na keshokutwa akienda tena US atakua na uzito gani?
 
Tanzania haina political stability kama Kenya ndio maana unaona Uhuru Kenyatta alipokelewa na Biden wakati mama alipokewa na diaspora!
Una maana gani na "political stability"?

Unachanganya mambo kwa kutumia lugha usiyofahamu maanha yake.

Ungesema, Kenya ni "Strategic partner" ndio maana kiongozi wa huko hupokelewa White House na mwenyeji wake hapo ungeeleweka.

Lakini hata kama ungesema hivyo, bado ningekuwa na mashaka kama unaelewa maana ya kuwa "strategic partner" ni nini.

Huyu hupewa majukumu maalum katika eneo fulani, na kuna ujira maalum anaopewa kila mwaka siyo chini ya Bilioni moja, ndiyo, bilioni moja ya hard currency kila mwaka, pamoja na marupurupu mengine chungu nzima.

Sasa huwezi ukalinganisha partner huyo na huyu kapuku mwingine anayejisomba na yeye apewe upendeleo.

Na hadi hapa, kama bado huelewi, basi kuna tatizo sehemu fulani. Jaribu kujichunguza uliondoe tatizo hilo.
 
JPM alikuwa Ni chuma jeuri,uliwai Kuona Ni Rais gani Africa anamtetemesha beberu Hadi anakuja ikulu na private Jet kupiga magoti?JPM alikuwa Ni chuma.
Eti ucheke na beberu,beberu sio mtu mzuri
 
Je Biden ana taarifa za ujio wa Mama yetu...??

Wale wana mambo mengi sana ya kufanya,,, schedule yako iko very tight..
 
Rais wetu anakaribia kufunga wiki nchini mwao lakini mwenyeji wake ambaye ndiye mkuu wa nchi hajakutana na mgeni wake(Mh. Rais wetu)

Hii ni dharau...ifike mahali tuwe masikini jeuri, hivi Mh. Biden angefanya ziara nchini Tanzania, kweli Mhe. Rais wetu angekuwa bize na mambo mengine na kuicha hiyo shughuli kwa waandamizi wake?

Ifike mahali wizara ya mambo ya nje wajitafakari pia katika hili.
Hiyo haikuwa state visit ndugu.... si ameongea na makamu wa Rais..pia na babake Rihana haukuridhika ?
 
Biden aache kushughulika na Ukraine na North Korea akapoteze muda na mtu anaepuyanga Hollywood?
 
JPM alikuwa Ni chuma jeuri,uliwai Kuona Ni Rais gani Africa anamtetemesha beberu Hadi anakuja ikulu na private Jet kupiga magoti?JPM alikuwa Ni chuma.
Eti ucheke na beberu,beberu sio mtu mzuri
Maskini Jeuri siyo !! Jirani yako akiwa na maendeleo kukuzidi dawa yake ni kumnunia hadi akome.
 
Biden aache kushughulika na Ukraine na North Korea akapoteze muda na mtu anaepuyanga Hollywood
Bidden yupo busy..kaachilia $700m kwa Ukraine juzi. Putin kanuna kasema anaachilia Nuclear...

Wacha tuone !!
 
Rais wetu anakaribia kufunga wiki nchini mwao lakini mwenyeji wake ambaye ndiye mkuu wa nchi hajakutana na mgeni wake(Mh. Rais wetu)

Hii ni dharau...ifike mahali tuwe masikini jeuri, hivi Mh. Biden angefanya ziara nchini Tanzania, kweli Mhe. Rais wetu angekuwa bize na mambo mengine na kuicha hiyo shughuli kwa waandamizi wake?

Ifike mahali wizara ya mambo ya nje wajitafakari pia katika hili.
Samia siku ya kwanza alionana na Makamu wa Rais wa Marekani. Ungejua maana ya dharau usingeandika haya uliyoandika.
 
Kwa mfano Bideni akija Tanzania kupumzika Serengeti ana weza hasikutane na Mama Samia ?
Acheni kasumba hizi, kuna safari rasmi na kuna zile za binafsi kama kaja kwa ajili ya masuala binafsi kwanini aonane na Samia?.
 
Mtoa mada acha unafiki, tafuta hela mkuu utakufa kwa kihiro kisicho na faida, urais ni taasisi na ina Washauri na wanajua nini wanakifanya, wewe unajua kuwa president Madiba (rip)aliishi pale Arusha for more than a week baada ya divorce na mama Nomzamo?
Hayo ya Mandela hawezi kuyajua,hawa ni wale pingapinga kwa kila kinachofanywa na serikali yao.
 
Ni hivyo sio? Rais wa nchi uingie kwenye nchi nyingine mwenyeji wako asikutambue?
Bado Kuna uchafu wa siasa za Magufuli alizozifanya haujaondolewa kwenye taswira ya nchi kimataifa
Nchi bado inanuka
Huwa dhambi inaondolewa kwa Toba haitoki yenyewe
Asanteni.
Unajiskia kuwashwa usipomtaja magufuli kila sehemu eti???
 
wee unafikiri rais makini kama Biden anaweza kukutana na raisi kutoka nchi ya kiafrika isiyo heshim uhuru wa kujieleza, demokrasia na haki za binadamu, na yenye kuendekeza ufisadi? wenzentu huwa wanaangalia hivi vitu kwa mapana zaidi

Are you serious? Cameroon. Chad. Kenya. Ndo utakatifu umejaa. Huko kujieleza gani unazungumzia wewe na huko hapa unaropoka asubuhi na jioni. Acheni kujidharau. Ulizeni. Wajerumani wana msemo: Die Kirschen in Nachbars Garten schmecken immer süßer.

Wewe huna Point yoyote ila unataka kumsema Rais na pengine ungependa kumsifia Lissu. Andika tu ila usipotoshe kwa matakwa ya uelewa wako finyu.
 
Back
Top Bottom