Kwa hili Wamarekani wanatudharau

Kwa hili Wamarekani wanatudharau

Alikuja mke wa Bush Zanzibar, basi mawasiliano ya simu yakawa yanapotea, njia zilifungwa watu wasipite. Sometimes unaweza kuona kwanini waliweza kututawala kirahisi
Hawa ndio wanaofadhili chaguzi feki. Lazima waheshimiwe.
 
Rais wetu anakaribia kufunga wiki nchini mwao lakini mwenyeji wake ambaye ndiye mkuu wa nchi hajakutana na mgeni wake(Mh. Rais wetu)

Hii ni dharau...ifike mahali tuwe masikini jeuri, hivi Mh. Biden angefanya ziara nchini Tanzania, kweli Mhe. Rais wetu angekuwa bize na mambo mengine na kuicha hiyo shughuli kwa waandamizi wake???

Ifike mahali wizara ya mambo ya nje wajitafakari pia katika hili.
Rais hajaenda Marekani kwa ziara ya kiserikali (official state visit), ameenda kwa shughuli tofauti ambayo haihusiani kukutana na Rais

Kuna protokali za Marais kukutana sio tu kwa sababu ameenda kwenye nchi yao
 
Acha kubwabwaja,Magufuli ndo amemzuia Baiden asimpokee Rais Samia?mbona waziri mkuu wa UK alifanya ziara Tanzania baada ya kifo Cha Magufuli,siyo kila kitu mmbebeshe Magufuli,nyie endeleeni kuhubiri kula kwa urefu wa kamba na kulamba asali mnafikiri hao mabeberu ni wenzenu
Hili la uchafu wa awamu ya 5 halifutiki. Utekaji, uuaji, wizi wa kura, kubambika wapinzani kesi, ufisadi...itachukua muda kuirudisha sifa ya utawala bora.
 
Hivi unafanya mchezo na Putin? Baiden hana akili hata moja kichuani anamuwaza Mrusi usiku na mchana na kiukweli yupo sahihi kbs jambo muhimu ndilo hupewa kipaumbele.
 
Rais wetu anakaribia kufunga wiki nchini mwao lakini mwenyeji wake ambaye ndiye mkuu wa nchi hajakutana na mgeni wake(Mh. Rais wetu)

Hii ni dharau...ifike mahali tuwe masikini jeuri, hivi Mh. Biden angefanya ziara nchini Tanzania, kweli Mhe. Rais wetu angekuwa bize na mambo mengine na kuicha hiyo shughuli kwa waandamizi wake???

Ifike mahali wizara ya mambo ya nje wajitafakari pia katika hili.
Usidanganyike kuhusu ziara ya kikazi marekani, alialikwa na kugharimiwa kwenye uzinduzi wa royal tour na kampuni husika. Sio mgeni wa serikali. Kuonana na makamu wa raisi ni fadhira tu.
 
Katika kuheshimu utu na thamani ya raia wa nchi fulani,hakuna nchi ndogo wa kubwa...Rais wa Gambia akija Tanzania anapaswa kupewa heshima ile ile ya Raisi wa Russia akija Tanzania...hatumheshimu Raisi kwa maana ya mtu...ila thamani ya taifa na watu wake
Utasubir san juu ya huo ulinganifu unaoutaka!! Mkubwa atabaki kua mkubwa tuu, refer preparations akitaka kuja rais wa marekani hapa kwetu, na preparations akitaka kuja Rais wa Malawi!!! Kuna mamb hayahitaji kukaza fuvu mzee!
 
Mtoa mada acha unafiki, tafuta hela mkuu utakufa kwa kihiro kisicho na faida, urais ni taasisi na ina Washauri na wanajua nini wanakifanya, wewe unajua kuwa president Madiba (rip)aliishi pale Arusha for more than a week baada ya divorce na mama Nomzamo?
Alikuwa bado hajawa Rais madiba wakati anatoa talaka ndio maana 1994 alipoapishwa alikuwa na mwanae mkubwa wa kike kama First Lady
 
Mtoa mada acha unafiki, tafuta hela mkuu utakufa kwa kihiro kisicho na faida, urais ni taasisi na ina Washauri na wanajua nini wanakifanya, wewe unajua kuwa president Madiba (rip)aliishi pale Arusha for more than a week baada ya divorce na mama Nomzamo?
Hakuna tasisi hapo ni kuangalia maslai yao na kulipana posho
 
Marekani taifa kubwa,

Biden akija hapa shughuli zote zinasimama

Bodaboda na bajaji watakufa njaa kwa kizuiliwa wasikanyage mjini kupisha ujio wa kiongozi mkubwa

Tanesco ile button inayojifyatuaga Hadi umeme unakatika wataishikilia ili tu kutafuta sifa ambazo hawana.

Sisi bado ni local country

Hata Subaru na brevis ukiimiliki huko nanyamba mtwara unaonekana tajiri

Lakini njoo nayo mjini uone
 
Ni hivyo sio? Rais wa nchi uingie kwenye nchi nyingine mwenyeji wako asikutambue?
Bado Kuna uchafu wa siasa za Magufuli alizozifanya haujaondolewa kwenye taswira ya nchi kimataifa
Nchi bado inanuka
Huwa dhambi inaondolewa kwa Toba haitoki yenyewe
Asanteni.
Yani unaongea point mwenyewe alafu unaonge ujinga mwenyewe,ivi usipo mtaja Magu huwezi kupata choo?.

Magu aliharibu nini kimataifa ambacho hakijasafishwa, mnakuwa kama mazuzu msiojua mnacho taka.
Mkipata rais anaerandaranda nchizawatu kilasiku,mnapiga makelele, mkipata rais anaeamini katika kutulia nchinikwake akusanye kodi na kujenga nchi,mnapiga makelele kwamba rais kwanini hasafiri.

Mnachosha sana nyinyi majitu.
 
Niliwahi kuangalia documentary moja inahusu Ikulu ya Marekani (White House)

Rais wa Marekani hupata wageni wengi sana kwa wiki moja wanaweza kuingia Marekani Marais 50 au zaidi kutoka Nchi mbalimbali na sio wote wanaofanikiwa kukutana na mwenyeji wao..
 
Rais wetu anakaribia kufunga wiki nchini mwao lakini mwenyeji wake ambaye ndiye mkuu wa nchi hajakutana na mgeni wake(Mh. Rais wetu)

Hii ni dharau...ifike mahali tuwe masikini jeuri, hivi Mh. Biden angefanya ziara nchini Tanzania, kweli Mhe. Rais wetu angekuwa bize na mambo mengine na kuicha hiyo shughuli kwa waandamizi wake?

Ifike mahali wizara ya mambo ya nje wajitafakari pia katika hili.
Ameenda kule kama msanii muigizaji na sio kama rais
 
Hili la uchafu wa awamu ya 5 halifutiki. Utekaji, uuaji, wizi wa kura, kubambika wapinzani kesi, ufisadi...itachukua muda kuirudisha sifa ya utawala bora.
Kwa hiyo Rais wetu aliomba kuonana na Biden akakataliwa kwa sababu ya Marehemu Magufuli?au kwa sababu ulizotoa?
 
Back
Top Bottom