Zero One Two
JF-Expert Member
- Sep 16, 2007
- 9,346
- 3,033
maggid kila kitu kina mwanzo na mwisho wake, na hata huyo mnyonge ipo siku atazinduka na kudai haki yake na hapo ndipo nchi itakua haikariki, ukija angalia chanzo cha yote ni upuuzi unaofanyika na watu walio pewa mamlaka
Na katika hili kinachonisikitisha zaidi ni ukweli kuwa, anayeumia ni mwananchi mnyonge aliyetuma sms ya matusi kwa Anne Makinda. Na sasa wanadakwa mmoja baada ya mwingine kwa vile namba zao zimesajiliwa. Hawa wanyonge watafunguliwa mashtaka na kuna watakaoingia gerezani. Kama kijana yule mwanajeshi wa Arusha, ambaye akiwa kwenye sare ya jeshi alionyesha alama ya Chadema akiwa kwenye picha na viongozi wa Chadema. Naye yuko jela sasa. Wakati haya yakiwatokea wanyonge , waheshimiwa wenye kutaja namba za simu za waheshimiwa wenzao hadharani, wataendelea ' kusakata-rhumba' - Kwa Raha Zao!
Maggid