Kwa hili la simu, Anne Makinda ameonewa..!

Kwa hili la simu, Anne Makinda ameonewa..!

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251
Ndugu zangu,

Kwenye vyombo vya habari juma hili, moja ya habari kubwa iliyochagizwa sana ni kitendo ch viongozi wa Chadema kutoa kwa wananchi, pale viwanja vya Mwembe Yanga, namba za simu ya mkononi ya Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ngugai.

Kimsingi, viongozi wa Chadema waliofanya kitendo kile walikosea. Yawezekana kabisa kuwa madai ya Chadema kuwa Spika na Naibu wake wanaisiginya demokrasia ndani ya Bunge ni madai ya msingi, lakini, namna waliyochagua ya kufikisha madai hayo kwa wananchi haikuwa sahihi.

Ni kawaida, kwa baadhi ya viongozi wawapo majukwaani kusukumwa na jazba wanapoongea, lakini, hutokea pia, kauli za viongozi hao wawapo majukwaani zinapokosa umakini, kupelekea madhara makubwa.

Katika kazi yangu ya uandishi, nimeshawahi kutofautiana na Spika Makinda, si mara moja, mara ya mwisho ni kwenye hoja yake kuwa wabunge wawapo Dodoma wana maisha magumu, hivyo, kuhalalisha ongezeko la posho zao.

Lakini bado naamini, Spika Makinda ni binadamu kama wengine. Naye ni mzazi na mwenye familia yake inayomzunguka. Kitendo cha viongozi wa Chadema kutoa hadharani namba za Spika Makinda , za simu ya mkononi, kwenye umati wa watu wenye kero mbali mbali , na unaoambiwa kuwa watumie namba hizo kumpigia na kutuma ujumbe mfupi kwa Spika Makinda, bila shaka, kwa akili ya kawaida tu, kitapelekea Spika Makinda na mwenzake Ndugai kuwa na wakati mgumu. Maana, watu wale watakuwa wamechochewa.

Ikumbukwe, kijinsia Anne Makinda anaweza kuwa mhanga zaidi wa kupigiwa na kutumiwa jumbe za simu zenye hata kumdhalilisha kijinsia. Katika dunia hii kuna baadhi ya wanaume wenye maradhi ya kisaikolojia yenye kuhusihanisha masuala ya ngono.

Kwamba kuna wanaume ambao hutafuta namba za simu za wanawake tu. Ikifika usiku, hupiga bila kuongea, wanachosubiri ni kusikia sauti ya mwananmke ikijibu na kisha kumaliza haja zao. Hao ni wagonjwa.

Hivyo, unapotoa hadharani namba ya simu ya mkononi ya mwanamke, basi, unaweza pia kumuingiza katika hatari ya kupokea simu za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya wanaume. Wako wapi wanaharakati wa haki za kibinadamu na kijinsia wa kumtetea Anne Makinda?

Tunajifunza nini?

Viongozi wa kisiasa wawe makini wawapo majukwaani. Mambo mengine wanaweza kuyafanya na hata kuyaongea majukwaani wakidhani kuwa wameyafanya kwa dhamira njema, lakini, matokeo yake yaweza kuwa na madhara makubwa.

Ingewezekana kabisa kwa viongozi wale wa Chadema kutoa hadharani namba maalum ya simu ya mkononi, ili watu wapige na watume jumbe fupi kwenye simu hiyo. Kisha, viongozi hao wangeweza kurekodi sauti zenye maoni ya watu yasiyo na matusi wala namna yoyote ya kudhalilisha. Wangekusanya pia jumbe hizo fupi kwa kuhariri zile zenye matusi na zenye kudhalilisha. Baadae zingewakilishwa kwa Spika Makinda na Naibu wake.

Ingewezekana pia kukusanya saini kutoka kwa wananchi zenye kuonyesha kuwa wanawapinga Spika na Naibu wake, na kwamba wanawashinikiza wang'oke. Hizi zote ni njia za kistaarabu kabisa za kuwasilisha malalamiko.

Tukishindwa kuonyesha mfano sasa, wa kufuata taratibu za kistaarabu, hatari yake tunaizoesha jamii kutumia njia za ovyo na nyingine zenye maovu katika kuwasilisha malalamiko yao. Na kesho huenda Spika wa Bunge atatoka Chadema.

Itakuwaje basi, pale kesho viongozi wa CCM nao watasimama Mwembe Yanga mbele ya wananchi wenye kero zao, na kutaja namba za simu ya mkononi za Spika wa Bunge linaloongozwa na Chadema?!

Hapana, hivi tunavyoenenda sivyo inavyopaswa twende. Na hakuna aliyekamilika. Tujisahihishe.

Maggid Mjengwa,

Iringa
 
Busara miongoni kwa viongozi wa Chadema imekosekana, wao wanafikiri kwa matumbo
 
chama cha wanywa Viroba, thin minded.
 
Hivi uthibitisho wa kwamba spika ametumiwa sms za matusi ni nani hasa anao? Au ni aina nyingine tu hii ya propaganda tunaletewa? Watu kadhaa wamekuja hapa jamvini na kusema spika ametumiwa sms za kumdhalilisha na wakati huo huo, hakuna hata sms moja ambayo imeonyeshwa walau kama mfano.

Mkuu Maggid, kikubwa hapa ni uadilifu wa mtu anayeshika nafasi hiyo bila kuangalia jinsia yake,chama chake,elimu yake na kigezo chochote kinginecho. Watu watende haki kama wanavyopaswa kulingana na majukumu yao. Sipingani na wewe kwa sababu ulichokitoa hapa ni maoni yako na yanapaswa kuheshimiwa kama yalivyo, lakini hebu na wewe basi jaribu kuheshimu mawazo ya viongozi wa chadema walioona kwamba kugawa namba za viongozi hao kwa wananchi ingeweza kusaidia kuongeza mbinyo kwa watu hao kutenda haki. Viongozi wa chadema hawakuwaeleza watu wamtukane au kumdhalilisha spika na naibu wake.
 
maggid@mafilili punguzeni uswahiba na hoja nyepesi nyepesi kama za fastjet za kutanguliza jinsia kwenye kuaddress issues.Kwanza Makinda alikwisha kata kwamba alichaguliwa uspika kwa sababu ya jinsi yake ya kike.Lakini mjiulize uhaini waliofanya Makinda na mwenzake mku Ndugai kuendesha bunge kwa kanuni pori ni sawa?.Dar haina maji, baraza la mitihani kuna udhaifu,mitaala haikidhi au haipo wao wanapeta tu?. Nani aliwatuma kuwa matarishi wa serikali ?. ni ujinga tu, wananchi ndio kila kitu.
 
Last edited by a moderator:
Majidi ukimwona mende muite mende na sio mdudu atambaae.
Makinda kama mkuu wa kitengo kafanya makosa na kubwa kafunga midomo wananchi na njia rahisi ya wananchi kumwambia umetukosea ni sms ama kumpigia.
Na kwa taarifa yako tuna makakati kutoa number kila mbunge atoe msimamo wake hadharani ya juu ya msimamo wake wa bunge kurushwa live haitajalisha mwanaume ama mwanamke.
Mbona alivyokua anaomba kura aliweka simu zake hadharani na hakupata hayo madhara unayoyasema?
 
Hivi uthibitisho wa kwamba spika ametumiwa sms za matusi ni nani hasa anao? Au ni aina nyingine tu hii ya propaganda tunaletewa? Watu kadhaa wamekuja hapa jamvini na kusema spika ametumiwa sms za kumdhalilisha na wakati huo huo, hakuna hata sms moja ambayo imeonyeshwa walau kama mfano.

Mkuu Maggid, kikubwa hapa ni uadilifu wa mtu anayeshika nafasi hiyo bila kuangalia jinsia yake,chama chake,elimu yake na kigezo chochote kinginecho. Watu watende haki kama wanavyopaswa kulingana na majukumu yao. Sipingani na wewe kwa sababu ulichokitoa hapa ni maoni yako na yanapaswa kuheshimiwa kama yalivyo, lakini hebu na wewe basi jaribu kuheshimu mawazo ya viongozi wa chadema walioona kwamba kugawa namba za viongozi hao kwa wananchi ingeweza kusaidia kuongeza mbinyo kwa watu hao kutenda haki. Viongozi wa chadema hawakuwaeleza watu wamtukane au kumdhalilisha spika na naibu wake.

Wikolo,
Asante sana,
Hata kama viongozi wa Chadema hawakuwaeleza watu wamtukane au wamdhalilishe Spika Anne Makinda, lakini, akili ya kawaida tu inakuambia, kuwa baada ya namba hiyo ya mkononi kutolewa, Spika Makinda asitarajie sms za kumtakia " Happy Valentine Day!".

Hoja yangu ya msingi ni kuwa kuna njia nyingine za kistaraabu zaidi na zenye kulinda faragha ya mtu za kuwasilisha malalamiko. Ikumbukwe pia, kuwa Anne Makinda anawakilisha taasisi ya Bunge. Sasa namba binafsi ya mkononi kutolewa hadharani yaweza kuwa usumbufu mkubwa kwake. Ni mtazamo wangu tu.
 
Azilete hizo sms tuone hayo matusi usikute alinitukana mwwnyewe
 
unachoandika mkuu mjengwa ni kujaribu kuangalia maumivu ya upande mmoja, kumbuka wananchi wamechoshwa na huu uhaini wa spika, kama tutakubali huyu mama awe untouchable tutaangamiza taifa , rejea hotuba ya zitto mwembe yanga.Ni vema madamu speaker akaelewa kwamba jamii inachukizwa na utawala wake pale mjengoni.Hata wiki haijaisha tangu atoe habari kuwa ametukanwa, jana ofisi yake imetoka na single mpya NO LIVE COVERAGE ON BUNGE NEWS, hiki wanachokifanya hakina tofauti na hao wanaoandika sms kumtukana, kumbuka na yeye tayari kawatukana watanzania kwa kutunyima haki ya kikatiba ya kupata habari.Mr. mjengwa huyu madam speaker ana shida kubwa na totally ameshindwa kutoa proof kwa usemi wao kuwa Wanawake wakiwezeshwa wanaweza.Kumbe wanawake hata wakiwezeshwa hawawezi, hilo hata wanawake wenzake wamekubali kuwa HAJAWAWAKILISHA vilivyo.
 
kama papa kajiuzulu kwanini huyu mama asiachie ngazi?
 
Maggid, Haya yote wakati mwingine yanasababishwa na hao wahanga wahusika(kama Makinda). Ubabe,ulevi wa madaraka na kutosikia lolote unaloshauriwa hata kama ni jema kwa vile wewe una madaraka ya mwisho ni hatari sana kwako wewe mwenyewe.
Walichofanya viongozi wa Chadema ni kumpatia ujumbe kuwa kama tusemacho sisi ambao tumetumwa na waliotuchagua unakidharau basi ngoja upate ujumbe toka kwao directly.
Nina hakika hata kama wametusiwa( ingawa kila mtu anatafsiri yake kwa tusi) lazima watakuwa wamepokea ujmbe mwingi wenye kuonyesha hisia sahihi kuhusu wakifanyacho na ushauri mzuri tuu wafanye nini.
Mbona wewe unatoa makala zako hapa za kuelimisha na unaungwa mkono sana na wengine wanakukosoa tena kwa lugha chafu na hujaacha kuandika? Kwa sababu unajua unadili na watu yote yapo.
Watende kulingana na kanuni na busara za kiuongozi kama haya yatawatokea,na wataifurahia kazi yao ya utumishi wa umma uliotukuka sio ukibaraka dhidi ya wananchi wanyonge.
Naweza sema kama kuna malalamiko toka kwa Makinda na Ndugai basi Chadema zoezi hili wamefanikiwa maana ujumbe umefika toka kwa wenye Bunge ( wananchi)
 
Wikolo,
Asante sana,
Hata kama viongozi wa Chadema hawakuwaeleza watu wamtukane au wamdhalilishe Spika Anne Makinda, lakini, akili ya kawaida tu inakuambia, kuwa baada ya namba hiyo ya mkononi kutolewa, Spika Makinda asitarajie sms za kumtakia " Happy Valentine Day!".

Hoja yangu ya msingi ni kuwa kuna njia nyingine za kistaraabu zaidi na zenye kulinda faragha ya mtu za kuwasilisha malalamiko. Ikumbukwe pia, kuwa Anne Makinda anawakilisha taasisi ya Bunge. Sasa namba binafsi ya mkononi kutolewa hadharani yaweza kuwa usumbufu mkubwa kwake. Ni mtazamo wangu tu.

Naona kwa umbumbumbu wako unakubali kuwa huyu mwanamke ni tatizo. UTETEZI wako wa nini sasa? Wewe umeyaon au kuyasikia hayo matusi kabla ya kulalama hapa? Na lazima uelewe kuwa tusi si subjective pia!
 
Wikolo,
Asante sana,
Hata kama viongozi wa Chadema hawakuwaeleza watu wamtukane au wamdhalilishe Spika Anne Makinda, lakini, akili ya kawaida tu inakuambia, kuwa baada ya namba hiyo ya mkononi kutolewa, Spika Makinda asitarajie sms za kumtakia " Happy Valentine Day!".

Hoja yangu ya msingi ni kuwa kuna njia nyingine za kistaraabu zaidi na zenye kulinda faragha ya mtu za kuwasilisha malalamiko. Ikumbukwe pia, kuwa Anne Makinda anawakilisha taasisi ya Bunge. Sasa namba binafsi ya mkononi kutolewa hadharani yaweza kuwa usumbufu mkubwa kwake. Ni mtazamo wangu tu.

Maggid, Kimsingi huna hoja kwani namba ya/za spika Makinda ziko hadharani.. nenda kwenye tovuti ya Bunge utazikuta wala huitaji kupewa na Lema au Mnyika.

Parliament of Tanzania
 
Majid Mjengwa usiwe mjima na mfinyu wa mawazo, unachokifanya ndo tabia ya watanzania walio wengi na ndo maana mnachezewa vichwa vyenu na wanasiasa uchwara, kuchanganya huruma na taratibu, ethics na kanuni za kazi, ifike mahala tukubaliane, ili nchi iende lazima utaratibu ufuatwe, kila mtu afanya kazi yake kwa mujib wa JD YAKE then uone kama hatutaenda vizuri.

Suala la viongozi wa chadema kutoa namba za speaker na naibu wake sio kosa, ni suala la kawaida sana na huu utaratibu upo kila nchi, we ni mwana habari utakuwa unaelewa ninachosema, taaluma yako ikusaidie kungamua haya mambo, ndio maana namba za simu zimechapishwa kwenye litabu cha orodha ya wabunge wa jamhuri na hizi namba zipo public kwenye website ya bunge" maana yhake ni kwamba kila mtu anaweza kuingia na kuisave mahala na kumpigia akiwa na jambo lolote linalomsibu! ninachoweza kusema na hapa ndo tunaitilafiana ni matuimizi ya hiyo namba na si kingine! usipotoshe umma please.

Alafu kwa mtu msomi lazima uwe na utaratibu wa kufanya analysis yako mwenyewe na upate mwongozo juu ya jambo unalolifanya! angekuwa na uelewa mkubwa asingetangaza, kwani ni dhahiri kuwa unapotumiwa sms 400 za matusi lazima ukae chini ujiuliza kazi yako u=inawafurahisha wangapi? unamtumikia nani?unamridhisha nani? hizi ni dalili kuwa people are not happy and are not ready to buy her service at any costs.

She is a loser, just look public sympathy, we are fed up with these cheap politicians, we need to find other altenaltive else we are going to develop backward for the rest of our lives. achana na mambo ya mzazi huku watu wanahangamia, matatizo anayafumbia macho, hoja za msingi anazizima, watoto wangaopi wakosa huduma kwa ajili ya kuficha madhambi ya wahusika? huruma yake yeye kama mzazi iko wapi? lazima watanzania tubadilike.
 
Hivyo, unapotoa hadharani namba ya simu ya mkononi ya mwanamke, basi, unaweza pia kumuingiza katika hatari ya kupokea simu za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya wanaume. Wako wapi wanaharakati wa haki za kibinadamu na kijinsia wa kumtetea Anne Makinda?

Sikuwahi kutegemea mawazo tofauti na haya hasa kutoka kwa mwanaccm anayeitwa maggid.
Hapa umetudhihirishia jambo moja tu kwamba mlimchagua spika mwanamke ili mpate kumuendesha mnavyotaka. Kama anajitambua kwamba yeye ni mwanamke na anaweza kuathirika zaidi kutokana na jinsia yake basi alitakiwa kuwa makini zaidi kuliko wanaume, na angezingatia zaidi haki, sheria na kanuni za bunge.

Tumeambiwa kwamba spika makinda hatumii akili yake kuendesha bunge bali anatumia akili za Lukuvi na Pinda. Sasa ni wakati muafaka aanze kutumia akili yake mwenyewe, nadhani baada ya wananchi wengi kumwandikia sm na wengine kumpigia simu atakuwa amewaelewa wananchi wanataka afanye nini na bila shaka kuanzia bunge lijalo la mwezi wa nne atakuwa makini sana kulinda uhuru na heshima ya bunge na wabunge kwa kuhakikisha kwamba hakiuki kanuni kwa lengo la kuibeba serikali inayoboronga hata kwa maswala mazito ya mustakabali wa taifa letu.

Ingewezekana kabisa kwa viongozi wale wa Chadema kutoa hadharani namba maalum ya simu ya mkononi, ili watu wapige na watume jumbe fupi kwenye simu hiyo. Kisha, viongozi hao wangeweza kurekodi sauti zenye maoni ya watu yasiyo na matusi wala namna yoyote ya kudhalilisha. Wangekusanya pia jumbe hizo fupi kwa kuhariri zile zenye matusi na zenye kudhalilisha. Baadae zingewakilishwa kwa Spika Makinda na Naibu wake,

Namba maalum ya kazi gani kwani huyo maalum ndiye anaongoza bunge? hatahivyo kufanya hivi unavyodhani wewe ilikuwa inaongeza gharama na mzunguko usio na ulazima, na pengine wewe ndio ungekuwa wa kwanza kuandika makala ya kusema Viongozi wa Chadema wamejitengenezea wenyewe hizo jumbe na sauti kwakuwa wananchi hawajasema hivyo, kwahiyo ni muhimu na bado itaendelea kuwa muhimu kwa spika kusikia sauti za wananchi wenyewe live wakimuelezea masikitiko yao juu ya uendeshaji mbaya wa bunge.

Itakuwaje basi, pale kesho viongozi wa CCM nao watasimama Mwembe Yanga mbele ya wananchi wenye kero zao, na kutaja namba za simu ya mkononi za Spika wa Bunge linaloongozwa na Chadema?!

Kama itatokea kuna spika wa Chadema (mataraji ya katiba mpya hatutakuwa na spika mwansiasa) na yeye anaboronga katika kuliendesha bunge itakuwa ni haki yao wanaccm kuitangaza hadharani namba yake ili wananchi wamtumie sms na kumipigia simu kumfikishia ujumbe wa moja kwa moja na kumkosoa juu ya utendaji wake usio ridhisha. Namba ya makinda na bdugai hazikutolewa kwakuwa wao ni wanaccm bali kwakuwa wao wanatumia vibaya nafasi zao za spika na naibu spika kulivuruga bunge.
 
Last edited by a moderator:
Busara miongoni kwa viongozi wa Chadema imekosekana, wao wanafikiri kwa matumbo

wenye busara ndo wanadidimiza nchi?

pima hii katika dimensions zifuatazo

1.elimu
2.afya
3.kilimo
4. miundombinu
5.demokrasia
6.uhuru wa habari na mawazo
7.rushwa

utajua viongozi wako ni wanamna gani!

kimsingi, tunapumua kwa ajli ya mabaki ya busara za mwalimu!
waliobaki wote makopo tu!nchi imepotea, wanajitajirisha wenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom