Kwa hili la simu, Anne Makinda ameonewa..!

Kwa hili la simu, Anne Makinda ameonewa..!

Ikumbukwe, kijinsia Anne Makinda anaweza kuwa mhanga zaidi wa kupigiwa na kutumiwa jumbe za simu zenye hata kumdhalilisha kijinsia. Katika dunia hii kuna baadhi ya wanaume wenye maradhi ya kisaikolojia yenye kuhusihanisha masuala ya ngono.

Kwamba kuna wanaume ambao hutafuta namba za simu za wanawake tu. Ikifika usiku, hupiga bila kuongea, wanachosubiri ni kusikia sauti ya mwananmke ikijibu na kisha kumaliza haja zao. Hao ni wagonjwa.



Hayo ni mawazo ya kitoto, usidhani watu wote wapo kama wewe......Kumbuka kuwa ujimbe haukutumwa Kwa mwanamke bali spika wa bunge la tz, ambaye amewachosha kwa kutitenda haki.
 
Nasikitika kusema wewe maggid ni pimbi wa kufikiri!
Namba za simu za spika na wabunge wengine zipo na zinapatikana kwenye website ya bunge.
Utetezi wako umejaa ujinga mtupu!
Yaani mlimweka spika mwanamke ili asiambiwe ukweli?
Siungi mkono walio mtukana,ila tupo wengi tu tulio tuma jumbe constructive,ambazo yamkini anaona ni matusi pia!
Hizo ndizo gharama za uongozi!!

Mpenda Yesu says thanks for this very kilazaful post!
 
Last edited by a moderator:
Maggid, shillingi ina pande mbili...Bunge ni la wananchi. Si busara kuendesha kama kijiwe cha watu wachache wanaolinda maslahi binafsi bila kujari nini athari zake....na lile la kutoa namba pia nakubaliana nawe sio sahihi maana litapelekea kutoa nafasi kwa abusers kuchafua hali a hewa.
Cha msingi, bunge liwe bunge...sio sehemu wana mieleka wanapopasha misuli moto.
 
Hajaonewa hata kidogo anapindisha sana mambo bungeni amelifanya bunge lizalaulike sana, kwani hasimamii hoja za msingi. wabunge wanakuwa kama wanaenda bungeni kula posho na si kuwakilisha vilio vya wananchi wao!
 
Huyu Mjengwa mtu wa ajabu sana!eti kwamba kuna wanaume wengine wanaweza kumpigia usiku wa manane ili wasikie sauti ya Anna Makinda na kutimiza haja zao?kwamba kwa sauti ya Makinda ya usiku wa manane mtu anapandisha stimu na kumwaga mzigo?kwa uzur gani wa sauti ya bibi huyu?Sishangai,mana kwa kuopoa vibibi Mjengwa ndo zako!ukafikiri na wengine wanapenda sauti za vibibi!!
 
Maggid, wewe ni mmoja kati ya vijana waandishi mashuhuri ninaowapenda kutokana na jinsi ya uandishi wao, lakini kwa hili la Makinda nahisi kama tunatofautiana kwa sana.
Katika makala yako hii umeeleza mambo mengi sana lakini la msingi likiwa la wewe kutokukubaliana na viongozi wa CHADEMA kugawa namba ya Spika na Naimu wake hadharani. Hili kwangu nasema ni HAKI tupu.

Binafsi nimeshaleta thread hapa juzi ya kusema kwa nini naunga mkono watu kuwa na namba ya kiongozi wao. Inapaswa uelewe kuwa kwa ulimwengu huu wa sasa kuwa na namba ya kiongozi wako si uhani kama ilivyokuwa miaka ile ya nyuma, bali uhaini ni jinsi gani unavyoitumia namba hiyo.

Sisi kama waathilika wa maamzi ya kiti cha Spika tunayo haki ya kupaza sauti na kusemezana naye ili ajue kuwa kukalia kwake kiti kile si kwamba amekali hata uelewa wetu wa mambo ya msingi kama anavyofikilia yeye au wewe. Kama Mungu anasema ........ "Eeee mtu wangu niite nami nitakuitika ili tusemezane". Sasa kama tunaweza kupata wasaa wa kusemezana na Mungu wetu, iweje tusisemezane na Spika wetu?!!

Mimi nina hakika kama Makinda angekuwa amewatendea mazuri wananchi, ni imani yangu kuwa angeweza kupata simu za kumfanya ajisikie yuko mbinguni hata kabla ya kufa kwake!! Mbona namba ya Mwakyembe, Magufuli, Slaa, Mnyika, Zitto na wengine wengi zipo wazi na hawajalalamika kuwa wanatukanwa?!

Kama imetokea, basi asiyaite matusi, bali aziite kuwa ni salaam na anatakiwa kuzifikisha kwa aliyemtuma. Mwambie amrudie Mungu ampe hekima ya kuweza kurirudisha Taifa hili katika mstari, la sivyo hasira zaidi za Mungu zitamshukia na itafika wakati watu wanaona mwanga, yeye ataona kama kuna giza na saa hiyo haipo mbali.

MUNGU ASIFIWE.
 
Itakuwaje basi, pale kesho viongozi wa CCM nao watasimama Mwembe Yanga mbele ya wananchi wenye kero zao, na kutaja namba za simu ya mkononi za Spika wa Bunge linaloongozwa na Chadema?!

maggid Umejuaje kuwa Chadema wakiongoza Bunge watapindisha vifungu vya sheria kama Chama Chako cha Magamba? au watakuwa na serikali dhaifu kama Magamba?

maggid unapoandika kitu uwe na majibu sio kupayukapauka kama magamba wenzako lasivyo na wewe unaonekana mpuuzi mbele ya wananchi kama wale wa chama cha magamba wanavyoonekana wapuuzi
 
Hizi namba mbona zipo open kila mtu awezaye kuzipata anaweza ?

Unapokuwa mtu wa watu kama Spika issue kama hizi ni part and parcel ya kazi yako; na kama hizi simu zitamfanya abadilike basi itakuwa ni job well done.., Kosa ni watu kumtukana lakini sio watu kutoa namba zake za simu
 
Maggid, shillingi ina pande mbili...Bunge ni la wananchi. Si busara kuendesha kama kijiwe cha watu wachache wanaolinda maslahi binafsi bila kujari nini athari zake....na lile la kutoa namba pia nakubaliana nawe sio sahihi maana litapelekea kutoa nafasi kwa abusers kuchafua hali a hewa.
Cha msingi, bunge liwe bunge...sio sehemu wana mieleka wanapopasha misuli moto.

Ndugu zangu,
kuna ambao hamjanielewa. Hoja yangu ya msingi ni kuwa, yale mazingira yaliyopelekea simu ya Spika na Naibu wake kutolewa hadharani yamechangia pia kuwapa wakati mgumu wahusika maana kuna waliotumia fursa hiyo vibaya na kupiga au kutuma jumbe za matusi kama wahusika ( Makinda na Ndugai) walivyolalamika. Kuna wakati tuache ushabiki wetu wa kisiasa na tuje kwenye hali halisi.

Akili ya kawaida kabisa inakwambia, kuwa kwenye kusanyiko la wafuasi wengi wa Chadema wanaokerwa na mambo mbali mbali, kuwapa namba ya simu ya mkononi ya Spika ina usitarajie wengi wa uliowapa namba hiyo wataitumia kwa kumtimia Anne Makinda salamu za ' Happy Valentine Day!'. Ukweli unabaki, Anne Makinda atavamiwa na sms na simu za wenye kumdhalilisha pia, hata kijinsia.

Na hapo ndipo tunatakiwa, kama binadamu, kumwelewa Anne Makinda anapolalamika, na kwa nini tusimwamini mpaka tumtake atuletee ushahidi wa matusi hayo. Kuna wakati Mzee Mwinyi alilalamika kuwa wanafunzi wa UDSM wamemtukana matusi ya nguoni, mbona hakuna aliyemtaka aje na ushahidi wa matusi ya nguoni?
Maggid
 
Ndugu zangu,
kuna ambao hamjanielewa. Hoja yangu ya msingi ni kuwa, yale mazingira yaliyopelekea simu ya Spika na Naibu wake kutolewa hadharani yamechangia pia kuwapa wakati mgumu wahusika maana kuna waliotumia fursa hiyo vibaya na kupiga au kutuma jumbe za matusi kama wahusika ( Makinda na Ndugai) walivyolalamika. Kuna wakati tuache ushabiki wetu wa kisiasa na tuje kwenye hali halisi.

Akili ya kawaida kabisa inakwambia, kuwa kwenye kusanyiko la wafuasi wengi wa Chadema wanaokerwa na mambo mbali mbali, kuwapa namba ya simu ya mkononi ya Spika ina usitarajie wengi wa uliowapa namba hiyo wataitumia kwa kumtimia Anne Makinda salamu za ' Happy Valentine Day!'. Ukweli unabaki, Anne Makinda atavamiwa na sms na simu za wenye kumdhalilisha pia, hata kijinsia.

Na hapo ndipo tunatakiwa, kama binadamu, kumwelewa Anne Makinda anapolalamika, na kwa nini tusimwamini mpaka tumtake atuletee ushahidi wa matusi hayo. Kuna wakati Mzee Mwinyi alilalamika kuwa wanafunzi wa UDSM wamemtukana matusi ya nguoni, mbona hakuna aliyemtaka aje na ushahidi wa matusi ya nguoni?
Maggid

Maggid,
Hivi Tanzania tunawawajibisha vipi power abusers? Au ndio business as usual...we ---- our hands when the talk? I am not supporting people to abuse Makinda and Ndugai....I am just shocked to see how affairs in the parliament being ran...Future problems and successes would be made by choices....Speaker and the deputy should know that as well as politicians.
Mimi si mshabiki wala wanachama wa chama chochote......ila Tanzania ni yetu sote wakiwamo viongozi wetu. Wasifane mambo atakao wezesha kuiharibu Tanzania leo na hata kesho au kesho kutwa.
 
Wikolo,
Asante sana,
Hata kama viongozi wa Chadema hawakuwaeleza watu wamtukane au wamdhalilishe Spika Anne Makinda, lakini, akili ya kawaida tu inakuambia, kuwa baada ya namba hiyo ya mkononi kutolewa, Spika Makinda asitarajie sms za kumtakia " Happy Valentine Day!".

Hoja yangu ya msingi ni kuwa kuna njia nyingine za kistaraabu zaidi na zenye kulinda faragha ya mtu za kuwasilisha malalamiko. Ikumbukwe pia, kuwa Anne Makinda anawakilisha taasisi ya Bunge. Sasa namba binafsi ya mkononi kutolewa hadharani yaweza kuwa usumbufu mkubwa kwake. Ni mtazamo wangu tu.

Mkuu maggid umepitia sheria za kuhusu maasiliano? Check TCRA kisha tujadili ndo maana welevu tupo kimyaa hili swala
 
Last edited by a moderator:
Nyani haoni kundule/ je? anafanya sahihi anapo minya hoja za wabunge wa vyama vya upinzani
 
Ndugu zangu,
Na hapo ndipo tunatakiwa, kama binadamu, kumwelewa Anne Makinda anapolalamika, na kwa nini tusimwamini mpaka tumtake atuletee ushahidi wa matusi hayo. Kuna wakati Mzee Mwinyi alilalamika kuwa wanafunzi wa UDSM wamemtukana matusi ya nguoni, mbona hakuna aliyemtaka aje na ushahidi wa matusi ya nguoni?
Maggid

Wewe Maggid sijui unatumia upande upi wa ubongo wako KUFIKIRI........Mzee Mwinyi alitukanwa (kama alitukanwa) na Mzee Punch na ushahidi ulikuwepo wazi.....sasa unafananishaje hili na issue ya huyu mama? Wakati wa Mwinyi (1992) kulikuwa na SMS?
 
Hivi ni nani amewadanganya kuwa namba za spika zilikuwa siri?
 
Ndugu zangu,

Kwenye vyombo vya habari juma hili, moja ya habari kubwa iliyochagizwa sana ni kitendo ch viongozi wa Chadema kutoa kwa wananchi, pale viwanja vya Mwembe Yanga, namba za simu ya mkononi ya Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ngugai.

Kimsingi, viongozi wa Chadema waliofanya kitendo kile walikosea. Yawezekana kabisa kuwa madai ya Chadema kuwa Spika na Naibu wake wanaisiginya demokrasia ndani ya Bunge ni madai ya msingi, lakini, namna waliyochagua ya kufikisha madai hayo kwa wananchi haikuwa sahihi.

Ni kawaida, kwa baadhi ya viongozi wawapo majukwaani kusukumwa na jazba wanapoongea, lakini, hutokea pia, kauli za viongozi hao wawapo majukwaani zinapokosa umakini, kupelekea madhara makubwa.

Katika kazi yangu ya uandishi, nimeshawahi kutofautiana na Spika Makinda, si mara moja, mara ya mwisho ni kwenye hoja yake kuwa wabunge wawapo Dodoma wana maisha magumu, hivyo, kuhalalisha ongezeko la posho zao.

Lakini bado naamini, Spika Makinda ni binadamu kama wengine. Naye ni mzazi na mwenye familia yake inayomzunguka. Kitendo cha viongozi wa Chadema kutoa hadharani namba za Spika Makinda , za simu ya mkononi, kwenye umati wa watu wenye kero mbali mbali , na unaoambiwa kuwa watumie namba hizo kumpigia na kutuma ujumbe mfupi kwa Spika Makinda, bila shaka, kwa akili ya kawaida tu, kitapelekea Spika Makinda na mwenzake Ndugai kuwa na wakati mgumu. Maana, watu wale watakuwa wamechochewa.

Ikumbukwe, kijinsia Anne Makinda anaweza kuwa mhanga zaidi wa kupigiwa na kutumiwa jumbe za simu zenye hata kumdhalilisha kijinsia. Katika dunia hii kuna baadhi ya wanaume wenye maradhi ya kisaikolojia yenye kuhusihanisha masuala ya ngono.

Kwamba kuna wanaume ambao hutafuta namba za simu za wanawake tu. Ikifika usiku, hupiga bila kuongea, wanachosubiri ni kusikia sauti ya mwananmke ikijibu na kisha kumaliza haja zao. Hao ni wagonjwa.

Hivyo, unapotoa hadharani namba ya simu ya mkononi ya mwanamke, basi, unaweza pia kumuingiza katika hatari ya kupokea simu za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya wanaume. Wako wapi wanaharakati wa haki za kibinadamu na kijinsia wa kumtetea Anne Makinda?

Tunajifunza nini?

Viongozi wa kisiasa wawe makini wawapo majukwaani. Mambo mengine wanaweza kuyafanya na hata kuyaongea majukwaani wakidhani kuwa wameyafanya kwa dhamira njema, lakini, matokeo yake yaweza kuwa na madhara makubwa.

Ingewezekana kabisa kwa viongozi wale wa Chadema kutoa hadharani namba maalum ya simu ya mkononi, ili watu wapige na watume jumbe fupi kwenye simu hiyo. Kisha, viongozi hao wangeweza kurekodi sauti zenye maoni ya watu yasiyo na matusi wala namna yoyote ya kudhalilisha. Wangekusanya pia jumbe hizo fupi kwa kuhariri zile zenye matusi na zenye kudhalilisha. Baadae zingewakilishwa kwa Spika Makinda na Naibu wake.

Ingewezekana pia kukusanya saini kutoka kwa wananchi zenye kuonyesha kuwa wanawapinga Spika na Naibu wake, na kwamba wanawashinikiza wang'oke. Hizi zote ni njia za kistaarabu kabisa za kuwasilisha malalamiko.

Tukishindwa kuonyesha mfano sasa, wa kufuata taratibu za kistaarabu, hatari yake tunaizoesha jamii kutumia njia za ovyo na nyingine zenye maovu katika kuwasilisha malalamiko yao. Na kesho huenda Spika wa Bunge atatoka Chadema.

Itakuwaje basi, pale kesho viongozi wa CCM nao watasimama Mwembe Yanga mbele ya wananchi wenye kero zao, na kutaja namba za simu ya mkononi za Spika wa Bunge linaloongozwa na Chadema?!

Hapana, hivi tunavyoenenda sivyo inavyopaswa twende. Na hakuna aliyekamilika. Tujisahihishe.

Maggid Mjengwa,

Iringa
Aisee sikutegemea haya kutoka kwako!!
Governance katika hali ya kawaida inamtaka Makinda awajibike kwa wananchi wote! Ikishindikana hiyo ndiyo njia vilevile ya kumwonyesha kutoridhika na mtu wanayemlipa kwa jasho la kodi zao! Namba za simu za public officials ni lazima ziwe kwenye mikono ya waajiri wao yaani wananchi. Tafadhali usitetee lolote hapa!! Halafu hapo kwenye nyekundu umemdhalilisha huyu "mwanamke" huyu ni kiongozi wa hali ya juu haitakiwi hata siku moja kumwita huyo "mwanamke" ni kosa kubwa sana kwa wanaharakati wa kijinsia! Hoja unayojenga ya gender discrimination/harassment haina mashiko!! Please wape wananchi haki yao ya kutoa maoni!!
 
Ndugu yangu Mjengwa, naona umejitahidi sana kutokuwa mnazi katika maoni yako. Ila mimi sikubaliani kabisa na wewe. Unamtetea Makinda kama mwanamke au kama Kiongozi? Mbona suala la Ndugai halichukuliwi kama ni tatizo, na kuna watu wanasema Ndugai alikuwa anajibu msg zao. Kwanini unataka kuwafanya wananchi tuone viongozi wetu kama watakatifu wasiopaswa kuguswa? Pale wanapotoka kura kwa wananchi wewe ndo unaona ni sawa kutoa namba zao, ila wakishapata madaraka kwako wewe unataka wafunge mawasiliano na viongozi wao.


Kwa kifupi hoja yako haina mashiko, na najua umeandika tu ili kuonyesha unasikitika naye....najua wewe ni consultancy na unatumia kalamu yako pia kwa manufaa yako na hauna tofauti na waandishi makanjanja tunaowapigia kelele (kumradhi sio kwamba nakutukana, bali nafafanua hoja yangu)


Mimi kama mdau wa maendeleo, ombwe la uongozi na maendeleo duni, uwajibikaji hafifu na umasikini tulionao unatokana na gap kubwa lililopo kati ya viongozi na wananchi wao. Mahusiano kati ya viongozi na wanachi ni ya kuombana na kupeana kura, hakuna kuwajibishana. Walichokifanya CDM, kilipaswa kiwe fursa kwa Makinda kufafanua kwa wananchi sababu za kufutwa kwa kamati.


Kumbuka kuwa ni haki ya kila mwananchi kuhoji maamuzi yeyote yanayofanywa yenye maslahi au kutumia rasilimali za umma. Sikubaliani na waliomtukana, ambao kimsingi ni sawa kuchukuliwa hatua, lakini vyema waliotumia fursa hiyo kutoa maoni yao au kuuliza maswali waheshimiwe na wapongezwe ili kujenga utamaduni wa ushiriki wa wananchi.


Namalizia kwa kusema maoni yako Mjengwa yanalenga kuwakandamiza wananchi wa kawaida, kuwaambia kuwa hawana haki ya kuwasiliana au kuhoji viongozi wao. Na ukandamizi huu unazidi kukithiri maana hata kuona bunge live sasa wanatunyima haki hiyo.


Nawasilisha
 
Maggid Mjengwa ,kwanza Spika Anna Makinda hana wadhifa wa kuitwa Mheshimiwa kajidhalilisha mwenyewe,na hastahili kuitwa hivyo.Pili ametudhalilisha wanawake watanzania kwa kuonyesha kuwa wanawake tukipewa nafasi hatuwezi kuzimudu,anahitaji kutuomba radhi wanawake.
wanawake tunajijua kuwa ni wajasiri,uamuzi wetu ni mzuri na hakuna mwanamke atakayeacha familia yake iteseke sababu hakuna chakula.Na ukimwelimisha mwanamke mmoja umielimisha jamii.
Ameona bora chama kuliko watanzania.
 
Katika nyakati hizi za teknolojia za mawasiliano, ni kazi sana kuthibiti haya, tena afadhali simu ni zake binafsi na anasoma mwenyewe kuliko kuandika makala ambayo itasomwa na wengi. Siijui kama tunaliona hili, pale mtu anapoandika makala yaa kumpinga mtu magazetini na pale mtu anapopiga simu ama kutuma sms kwa mhusika. After all, nani ana access ya kusoma sms ama kupokea simu za Spika ama Naibu wake?
 
Back
Top Bottom