Kwa hili la simu, Anne Makinda ameonewa..!

Kwa hili la simu, Anne Makinda ameonewa..!

Inawezekana kweli kuwa ameonewa kama unavyodhani, lakini suala la kujiuliza kwa upande mwingine ni Je, yeye katika utendaji wake kama Spika huwa anaonea watu anaowaongoza?

Kama jibu ni NDIYO, basi huna haja ya kusikitika kwamba ameonewa kwani yeye ndo mwalimu wa waoneaji. Na kama jibu ni SIYO, hapo kweli naungana na wewe katika sikitiko hilo.
 
Nyani haoni kundule/ je? anafanya sahihi anapo minya hoja za wabunge wa vyama vya upinzani


Na katika hili kinachonisikitisha zaidi ni ukweli kuwa, anayeumia ni mwananchi mnyonge aliyetuma sms ya matusi kwa Anne Makinda. Na sasa wanadakwa mmoja baada ya mwingine kwa vile namba zao zimesajiliwa. Hawa wanyonge watafunguliwa mashtaka na kuna watakaoingia gerezani. Kama kijana yule mwanajeshi wa Arusha, ambaye akiwa kwenye sare ya jeshi alionyesha alama ya Chadema akiwa kwenye picha na viongozi wa Chadema. Naye yuko jela sasa. Wakati haya yakiwatokea wanyonge , waheshimiwa wenye kutaja namba za simu za waheshimiwa wenzao hadharani, wataendelea ' kusakata-rhumba' - Kwa Raha Zao!

Maggid
 
Ndugu zangu,
kuna ambao hamjanielewa. Hoja yangu ya msingi ni kuwa, yale mazingira yaliyopelekea simu ya Spika na Naibu wake kutolewa hadharani yamechangia pia kuwapa wakati mgumu wahusika maana kuna waliotumia fursa hiyo vibaya na kupiga au kutuma jumbe za matusi kama wahusika ( Makinda na Ndugai) walivyolalamika. Kuna wakati tuache ushabiki wetu wa kisiasa na tuje kwenye hali halisi.

Akili ya kawaida kabisa inakwambia, kuwa kwenye kusanyiko la wafuasi wengi wa Chadema wanaokerwa na mambo mbali mbali, kuwapa namba ya simu ya mkononi ya Spika ina usitarajie wengi wa uliowapa namba hiyo wataitumia kwa kumtimia Anne Makinda salamu za ' Happy Valentine Day!'. Ukweli unabaki, Anne Makinda atavamiwa na sms na simu za wenye kumdhalilisha pia, hata kijinsia.

Na hapo ndipo tunatakiwa, kama binadamu, kumwelewa Anne Makinda anapolalamika, na kwa nini tusimwamini mpaka tumtake atuletee ushahidi wa matusi hayo. Kuna wakati Mzee Mwinyi alilalamika kuwa wanafunzi wa UDSM wamemtukana matusi ya nguoni, mbona hakuna aliyemtaka aje na ushahidi wa matusi ya nguoni?
Maggid
Kweli inakuwa vigumu kukuelewa kama huiweki hoja yako ikaeleweka moja kwa moja. Ebu fafanua kidogo, tatizo unaloliangazia ni
A. Wabunge wa Chadema kuweka namba ya Spika na Naibu hadharani au
B. Watu kuandika ujumbe wa kudhalilisha kwa Spika na Naibu wake au
C. Mazingiora ya kuwekwa hadharani kwa namba hizo? au
D. Zoye, AB na C ni sahihi?
 
Na katika hili kinachonisikitisha zaidi ni ukweli kuwa, anayeumia ni mwananchi mnyonge aliyetuma sms ya matusi kwa Anne Makinda. Na sasa wanadakwa mmoja baada ya mwingine kwa vile namba zao zimesajiliwa. Hawa wanyonge watafunguliwa mashtaka na kuna watakaoingia gerezani. Kama kijana yule mwanajeshi wa Arusha, ambaye akiwa kwenye sare ya jeshi alionyesha alama ya Chadema akiwa kwenye picha na viongozi wa Chadema. Naye yuko jela sasa. Wakati haya yakiwatokea wanyonge , waheshimiwa wenye kutaja namba za simu za waheshimiwa wenzao hadharani, wataendelea ' kusakata-rhumba' - Kwa Raha Zao!

Maggid
Ninaamini wewe siye Maggid!! Bado unatetea namba za viongozi wa UMA ziwe siri!! you are not serious!!
 
Na katika hili kinachonisikitisha zaidi ni ukweli kuwa, anayeumia ni mwananchi mnyonge aliyetuma sms ya matusi kwa Anne Makinda. Na sasa wanadakwa mmoja baada ya mwingine kwa vile namba zao zimesajiliwa. Hawa wanyonge watafunguliwa mashtaka na kuna watakaoingia gerezani. Kama kijana yule mwanajeshi wa Arusha, ambaye akiwa kwenye sare ya jeshi alionyesha alama ya Chadema akiwa kwenye picha na viongozi wa Chadema. Naye yuko jela sasa. Wakati haya yakiwatokea wanyonge , waheshimiwa wenye kutaja namba za simu za waheshimiwa wenzao hadharani, wataendelea ' kusakata-rhumba' - Kwa Raha Zao!

Maggid

Mkuu hapa nashindwa kuelewa unatetea nini na unamtetea nani...,
Ni ukweli usiopingika kwamba kutukana au kutoa matusi ni kosa kisheria na yoyote anayefanya hivyo amekosea, sasa sielewi unaposema kwamba kosa ni kwa aliyetoa namba. Je kwa sisi tuliopata namba na tukaweza kuelezea yaliyopo moyoni mwetu na kumshauri Spika huoni manufaa yoyote ?

Au sababu watu walitumia vibaya opportunity waliyopewa ndio useme kwamba kosa ni kwa aliyetoa opportunity na sio kwa aliyetumia vibaya opportunity.
 
Ndugu yangu Majjid nakuasa uwe na Taqwa ya kumuogopa Allah S.W.T...Epuka unafiki na kuhubiri unafiki Mkuu...Approach ya kistaarabu ipi unayohubiri kutumika kwa Makinda, Ndugai et al?...Siku si nyingi Watanzania tulikuwa na maadui watatu wa kuu; UJINGA, MARADHI na UMASIKINI...

Ndani ya miaka 51 ya Uhuru tumeshuhudia adui mwingine mwenye kuleta madhara kwa watanzania i.e CCM!
Thru CCM akina mama wanajifungulia sakafuni, watoto wetu wanakosa elimu bora, Walimu wamewezeshwa kufaulisha watoto wasiojua kusoma wala kuandika. Thru CCM Twiga, Tembo na wanayama wengine wanatoweka kwa kasi. Thru CCM wakaazi wa mijini wanakunywa maji ya visima vyenye kinyesi pamoja na kuzungukwa na mito mikubwa kama mto Ruvu na Rufiji.

Thru CCM Madini yenye Thamani ya matrilioni ya Dolla yanatoroshewa Ulaya na marekani na kuwaachia watanzania uchafuzi mkubwa wa mazingira. Thru CCM kunaukandamizaji mkubwa wa habari. Thru CCM Gavana wa Benki Kuu anakula bata huko majuu baada ya kufanikisha ubinafsishaji na wizi wa EPA. Thru CCM wananchi wanakufa kwa njaa maeneo mengi ya nchi ikiwemo ngorongoro!...

Thru CCM Anne Makinda na Ndugai Wananchi wa Dar Wanakoseshwa kile walicho watuma wabunge wao Bungeni BADALA yake wanazika hoja yenye maslahi mapana kwa Taifa....

Majjid ... SMS haitoshi...Soon tutaaza kuwazomea popote pale wanapoonekana hawa Mafisadi wenye kubaka Demokrasia!!!!! Mstaarabu mambo yake hutatuliwa kiustaarabu! Muuaji lazima to deal nae kwa tahadhari kuu na ikibidi ni kumpiga mshale akiwa mbali LIWALO na LIWE!
 
Ndugu zangu,

Kwenye vyombo vya habari juma hili, moja ya habari kubwa iliyochagizwa sana ni kitendo ch viongozi wa Chadema kutoa kwa wananchi, pale viwanja vya Mwembe Yanga, namba za simu ya mkononi ya Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ngugai.

Kimsingi, viongozi wa Chadema waliofanya kitendo kile walikosea. Yawezekana kabisa kuwa madai ya Chadema kuwa Spika na Naibu wake wanaisiginya demokrasia ndani ya Bunge ni madai ya msingi, lakini, namna waliyochagua ya kufikisha madai hayo kwa wananchi haikuwa sahihi.

Ni kawaida, kwa baadhi ya viongozi wawapo majukwaani kusukumwa na jazba wanapoongea, lakini, hutokea pia, kauli za viongozi hao wawapo majukwaani zinapokosa umakini, kupelekea madhara makubwa.

Katika kazi yangu ya uandishi, nimeshawahi kutofautiana na Spika Makinda, si mara moja, mara ya mwisho ni kwenye hoja yake kuwa wabunge wawapo Dodoma wana maisha magumu, hivyo, kuhalalisha ongezeko la posho zao.

Lakini bado naamini, Spika Makinda ni binadamu kama wengine. Naye ni mzazi na mwenye familia yake inayomzunguka. Kitendo cha viongozi wa Chadema kutoa hadharani namba za Spika Makinda , za simu ya mkononi, kwenye umati wa watu wenye kero mbali mbali , na unaoambiwa kuwa watumie namba hizo kumpigia na kutuma ujumbe mfupi kwa Spika Makinda, bila shaka, kwa akili ya kawaida tu, kitapelekea Spika Makinda na mwenzake Ndugai kuwa na wakati mgumu. Maana, watu wale watakuwa wamechochewa.

Ikumbukwe, kijinsia Anne Makinda anaweza kuwa mhanga zaidi wa kupigiwa na kutumiwa jumbe za simu zenye hata kumdhalilisha kijinsia. Katika dunia hii kuna baadhi ya wanaume wenye maradhi ya kisaikolojia yenye kuhusihanisha masuala ya ngono.

Kwamba kuna wanaume ambao hutafuta namba za simu za wanawake tu. Ikifika usiku, hupiga bila kuongea, wanachosubiri ni kusikia sauti ya mwananmke ikijibu na kisha kumaliza haja zao. Hao ni wagonjwa.

Hivyo, unapotoa hadharani namba ya simu ya mkononi ya mwanamke, basi, unaweza pia kumuingiza katika hatari ya kupokea simu za ajabu ajabu kutoka kwa baadhi ya wanaume. Wako wapi wanaharakati wa haki za kibinadamu na kijinsia wa kumtetea Anne Makinda?

Tunajifunza nini?

Viongozi wa kisiasa wawe makini wawapo majukwaani. Mambo mengine wanaweza kuyafanya na hata kuyaongea majukwaani wakidhani kuwa wameyafanya kwa dhamira njema, lakini, matokeo yake yaweza kuwa na madhara makubwa.

Ingewezekana kabisa kwa viongozi wale wa Chadema kutoa hadharani namba maalum ya simu ya mkononi, ili watu wapige na watume jumbe fupi kwenye simu hiyo. Kisha, viongozi hao wangeweza kurekodi sauti zenye maoni ya watu yasiyo na matusi wala namna yoyote ya kudhalilisha. Wangekusanya pia jumbe hizo fupi kwa kuhariri zile zenye matusi na zenye kudhalilisha. Baadae zingewakilishwa kwa Spika Makinda na Naibu wake.

Ingewezekana pia kukusanya saini kutoka kwa wananchi zenye kuonyesha kuwa wanawapinga Spika na Naibu wake, na kwamba wanawashinikiza wang'oke. Hizi zote ni njia za kistaarabu kabisa za kuwasilisha malalamiko.

Tukishindwa kuonyesha mfano sasa, wa kufuata taratibu za kistaarabu, hatari yake tunaizoesha jamii kutumia njia za ovyo na nyingine zenye maovu katika kuwasilisha malalamiko yao. Na kesho huenda Spika wa Bunge atatoka Chadema.

Itakuwaje basi, pale kesho viongozi wa CCM nao watasimama Mwembe Yanga mbele ya wananchi wenye kero zao, na kutaja namba za simu ya mkononi za Spika wa Bunge linaloongozwa na Chadema?!

Hapana, hivi tunavyoenenda sivyo inavyopaswa twende. Na hakuna aliyekamilika. Tujisahihishe.

Maggid Mjengwa,

Iringa

Mbona MWAKYEMBE alitoa namba yake hajatukanwa? huyo ni utumwa wake ndo unampelekea MATUSI pamoja na kuwa si vema kutumia lugha ya matusi kumrekebisha mtu ila nae APATE funzo kama kuna viongozi wengi wametoa no zao na hawatukanwi yeye kwa nini anatukanwa?.
 
Kaka Majidd ni wewe?!Hawa viongozi wetu wa bunge hawatutendei haki watz.Wanatudhalilisha vibaya mno.wanapaswa kuulizwa.
 
Maggid, mbona mimi nilikuwa nadhani una upeo mzuri wa kuchanganua mambo?

Hivi kwenye hili, tatizo ni nini? Tena ni maelekezo ya utawala bora kuwa simu anwani kamili (simu, barua pepe na anwani) za mawasiliano kwa watendaji wote ni lazima zifahamike. Ndiyo maana siku hizi ukifika kwenye ofisi za polisi, namba za simu za RPC zimewekwa ubaoni. Au Maggid bado unaishi ulimwengu wa 'Bwana Mkubwa habughudhiwi?

Maggid kwa upeo wako, hustahili kabisa kufanyia kazi majungu. Majungu hufanyiwa kazi na wapiga majungu. Anne Makinda ametukanwa tusi gani, wewe unafahamu? Kama unayo hayo matusi tuwekee hapa jukwani ili tuyajadili. Kweli nimeamini tunapita katika kipindi kigumu, hata wale unaodhania wangeweza kuwasaidia wengine, nao wanahitaji msaada.

Makala nzima, hakuna cha maana.
 
kila mmoja yupo kwaajili ya wengine tofauti na hapo huyo mtu hajatimia. acha ubinafsi
Na katika hili
kinachonisikitisha zaidi ni ukweli kuwa, anayeumia ni mwananchi mnyonge
aliyetuma sms ya matusi kwa Anne Makinda. Na sasa wanadakwa mmoja baada
ya mwingine kwa vile namba zao zimesajiliwa. Hawa wanyonge
watafunguliwa mashtaka na kuna watakaoingia gerezani. Kama kijana yule
mwanajeshi wa Arusha, ambaye akiwa kwenye sare ya jeshi alionyesha alama
ya Chadema akiwa kwenye picha na viongozi wa Chadema. Naye yuko jela
sasa. Wakati haya yakiwatokea wanyonge , waheshimiwa wenye kutaja namba
za simu za waheshimiwa wenzao hadharani, wataendelea ' kusakata-rhumba'
- Kwa Raha Zao!

Maggid
 
ambacho hukijui wala kukielewa ni kuwa matumizi ya simu yapo kisheria. anaeitumia vibaya sheria ipo. hatuwezi kucha kutumia simu eti kwasababu watu watatumia kutukana watu
Kweli inakuwa vigumu
kukuelewa kama huiweki hoja yako ikaeleweka moja kwa moja. Ebu fafanua
kidogo, tatizo unaloliangazia ni
A. Wabunge wa Chadema kuweka namba ya Spika na Naibu hadharani au
B. Watu kuandika ujumbe wa kudhalilisha kwa Spika na Naibu wake au
C. Mazingiora ya kuwekwa hadharani kwa namba hizo? au
D. Zoye, AB na C ni sahihi?
 
Maggid umetoka kwa bi mkola morogoro?mbona unakunya na fikra pevu hivi?eti wanaume wanamaliza shida zao kwa kusikia sauti ya mwanamke tuu.kwa hiyo kama ni kiongozi mwanamkeasikosolewe kwa kuhofia jinsia yake?umeyumba baba kajipange upya
 
Mr.Mjengwa,
Pole sana na majukumu yako ya kazi na pia naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa kazi nzuri ya uandishi wa habari
nimekuwa nikiangalia blogg yako mara nyingi na ninapapenda sana Iringa:
Kabla ya kuandikia hii habari ilitakiwa ufikiri haya yafuatao maana:

Makinda anaigandamiza sana demokrasia na wewe umekuwa ukiipigania hiyo demokrasia
Utawala uliopo madarakani unaongoza si zaid ya watu laki tano kati ya 44milioni.Ni wale walio kwenye system tu
Bunge baada ya kuwa mhimili wa dola,limekuwa mhimili wa uovu na ubadhirifu na kila aina ya mabwana wa jehanamu
Hakuchaguliwa kwa ajili ya kuwasaidia watanzania alichaguliwa kulinda maslahi ya ccm.
Wewe pia umekuwa mhanga mkubwa wa ujinga huu wa serikali
Wakati ameuawa Mwangosi ni wewe uliesaidia kuchangisha lkn Makinda alisaidia jinsi wewe ulivyosaidia?
Mjengwa katika blogg inayoheshimika Tanzania kuhusu siasa na haki ya binadamu ya kwako ndio inaongoza;
Mwaka jana ilitangaza kuwa Lema aliongoza na Zito alifuatia kwa kura halali kama wanasiasa bora .sasa mbona upendi wakifanya maamuzi magumu?
Pole Mjengwa
 
Hoja yangu ya msingi ni kuwa, yale mazingira yaliyopelekea simu ya Spika na Naibu wake kutolewa hadharani yamechangia pia kuwapa wakati mgumu wahusika

Hilo la kuwapa wakati mgumu makinda na ndugai ndio lilikuwa lengo na sababu ya kutaja hadharani katika mkutano namba zao za simu. Ingawa namba hizo zilikuwa zinapatikana kwenye website ya bunge na wengine tulikuwa nazo kupitia njia nyenginezo lakini siku ile pale temeke mwisho namba hizo zilitangazwa ili wananchi wengi zaidi wazijue na wazitumie kupaza sauti zao kuwaambia kwamba waache ubabaishaji.

Kwahiyo kama unathibitisha kwamba makinda na ndugai wamepata wakati mgumu kutokana na sms pamoja na simu za watanzania basi tuna kila sababu ya kuendelea kutumia utaratibu huu kwa kila kiongozi anayevurunda. Natarajia kwamba next time raisi naye akivurunda tunairusha hewani namba yake wananchi wanamuendea hewani, waziri mkuu akivurunda naye tunairusha namba yake wananchi wanamuendea hewani.
 
Maggid, kunaweza kupatikana watu watakaosumbuliwa na polisi lakini hakuna wa kuwekwa gerezani maana mpaka sahizi hakuna hata mtu mmoja, awe ni Makinda, Ndugai au kamanda wa polisi aliyeweza kutamka au kuonesha ujumbe wa matusi aliotumiwa Anne Makinda. Mtu hafungwi jela kwa majungu au kwa habari za mitaani bila ya uthibitisho. Maggid unapoteza muda kuanzisha mjadala wa hisia badala ya mjadala wa matukio. Umeambiwa Anne ametukanwa, nawe mara moja ukainuka na kuanzisha mjadala, mwandishi makini ungefanya utafiti, utuletee na nukuu za hayo matusi. Kwa mtindo huu, nawe unaingia kwenye kundi linalojitahidi kuijenga jamii ya wapiga majungu.

Na katika hili kinachonisikitisha zaidi ni ukweli kuwa, anayeumia ni mwananchi mnyonge aliyetuma sms ya matusi kwa Anne Makinda. Na sasa wanadakwa mmoja baada ya mwingine kwa vile namba zao zimesajiliwa. Hawa wanyonge watafunguliwa mashtaka na kuna watakaoingia gerezani. Kama kijana yule mwanajeshi wa Arusha, ambaye akiwa kwenye sare ya jeshi alionyesha alama ya Chadema akiwa kwenye picha na viongozi wa Chadema. Naye yuko jela sasa. Wakati haya yakiwatokea wanyonge , waheshimiwa wenye kutaja namba za simu za waheshimiwa wenzao hadharani, wataendelea ' kusakata-rhumba' - Kwa Raha Zao!

Maggid
 
Mahakama ya umma haina makosa kama hawafuati kanuni za bunge na kupindisha sheria za utawala bora walipuliwe tu kwa wananchi
 
Back
Top Bottom