Ofisi za balozi wanapata taarifa moja kwa moja toka kwa wananchi hawataki taarifa za vyombo vya ccm, balozi zote wanaujua Ukweli jinsi ccm inavyowafanyizia wapinzani hata ukija na uongo wa kuwachafua Balozi za nje ni kama unajisumbua tuTangu mwanzo walio wengi walianza kuwa na shaka juu ya haya mataifa ya nje namna yanavyoitazama Tanzania.
Tukio la kuumia kwa mh Mbowe kama inavyodaiwa kuwa alishambuliwa lilileta taharuki kubwa kiasi cha mataifa haya makubwa kuja na matamko mengi.
Jambo la kushangaza ni kitendo cha Marekani na Umoja wa Ulaya kupitia balozi zao kutoa matamko yaliyoashiria kuihusisha serikali na tukio hilo.
Jambo ambalo si sawa kidiplomasia. Taarifa ya polisi imekuja kuwatia aibu baada ya kuthibitisha kuwa mh Mbowe hakushambuliwa na mtu.
Kila Jambo linalofanyika hapa kwetu wamekuwa wepesi sana kutoa matamko haraka bila kuyafanyia utafiti wa kutosha hii inatia shaka kuwa Kuna agenda za siri wanazo dhidi yetu.
Tangu Magufuli aunde serikali yenye msimamo mikali na kujiamini katika mambo mbali mbali basi imekuwa kesi kubwa kwa hawa watu.
Mifano mizuri hii:
Walilazimisha tuna Ebora kwamba tunaficha wagonjwa.
Wakatangaza Tanzania kuna magaida yatashambulia masaki bila kushirikisha serikali.
Wakazuia mkuu wa mkoa eti ananyima watu haki ya kuishi.
Kwenye corona ndio kabisaa kila siku ni kuisema Tanzania tu wakati huko kwao wanakufa maelfu.
Leo tena wamekuja na matamko kibao kuhusu kuumia kwa Mh Mbowe, wakishutmu serikali.
Haya leo wameumbuka tena baada ya ukweli kuwekwa wazi.
Kila siku wamekuwa watu wa matamko tu kwetu swali la kujiuliza ni je wanatupenda sana au ni kipi hasa?
Wana nia gani na sisi?
Wananufaika na nini na huu uzushi wanao utangaza dhidi ya Tanzania?
Watanzania tusipokuwa makini Hawa watu watakuja kutuundia vikundi vya waasi hapa kwetu kama hizi propaganda zao zitafeli.
Hawana upendo wowote kwetu hawa ni maharamia tu.